Wa tano ni basil P. Mramba
Na wa sita ni Kingunge
Nasema kingunge kwa maana ya kwamba huyu jamaa amekuwa waziri toka enzi ya Nyerere, ni kikongwe pekee aliyebaki ndani ya Govt, ni heri basi angekuwa na Busara lakini hakuna ni politics tu.
Huyu jamaa hana msimamo kabisa, enzi za nyerere alisimamia siasa za ujamaa kumliko hata Mwalimu, tukajua huyu ni mjamaa kweli kweli, Akaja Mwinyi, hatukusikia hata siku moja akipingana na mwinyi kama ilivyokuwa kwa mwalimu JK Nyerere, akaja Mkapa na sera za ubinafsiji na uwazi na Ukweli,NBC, TCC etc wameuza, yeye kimya, Kaingia JK naye yu mstari wa mbele kwa usanii badala ya kukemea. Huyu mtu yupo kwa maslahi yake tu na ndiyo maana sasa hivi ni bepari mkubwa.
Salim, Ng'wandu, kahama wamestaafu yeye yumo tu, hata kama unateuliwa si useme mi basi. Huyu hatufai, hana msimamo ni BENDELA FUATA UPEPO, leo akija mwingine na hili na yeye yumo.