Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,798
- 2,739
Bila shaka sasa kuna haja pamoja na mambo mengine ya kisiasa pia tuwawajibishe mawaziri wetu kupitia JF hasa katika Thread hii ya "Waziri huyu hafai" Nimebuni blog hii si kwa nia ya kuwakomoa mawaziri watakao chomoka kwa ajili ya kujadiliwa kuhusu kutokufaa kwao bali pia ni kuwakumbusha kwamba wamefikia mstari mwekundu kwa hiyo watahitaji kupata usimamizi maalumu na wahusika wao. Chukulia mathalani mtoto mchanga anatakiwa kuhudhuria kliniki kila mwezi ambapo hupimwa uzito na mambo mengine na huwekwa alama ya uzito wake yule atakaye over weight itaonyeshwa pia itafika mahali ikizidi mhusika ataelekezwa hatua za kuchukua na kama mtoto ata under weight vivyo hivyo. Mawaziri watachunguzwa mali zao bila kujua na jinsi walivyozipata na huku katika JF tutatoa tathmini kwamba hapa hii ni obesity anatakiwa kupunguza uzito ama la. Lakini pia kuna mawaziri wazuri sana ambao kweli wanaipenda nchi hii wao huenda hata majina yao yasionekane humu JF. Lengo kuu ni kuwasafisha ili tubaki na Tanzania yetu ikiwa safi.