Waziri Gwajima atoa onyo kwa Wafanyabiashara wakubwa wanawatumia Wamachinga ili kukwepa kodi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia Wamachinga wadogo kuuza bidhaa zao ili kukwepa kodi.

Waziri amebainisha kuwa katika baadhi ya maeneo rafiki yaliyotengwa kwa ajili ya wamachinga, bado wameendelea kuona baadhi yao wakiondoka na kurudi barabarani, na baada ya kutafiti zaidi waligundua wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa kubeba biashara zao na kuuza bila utaratibu.

"Niwapelekee tu salamu, hawa ambao tumepata taaarifa zao tunaendelea na uchunguzi na tunasema hiyo siyo sawa tusijifiche kwenye migongo ya wamachinga na kuwashinikiza na kuwashawishi waende wakafanye biashara kwenye maeneo ambayo tulishasema siyo rasmi kwao.

Aidha, Waziri Gwajima amewaomba wamachinga kuacha kutumiwa na wafanyabiashara hao na kuahidi kuwa mara Serikali itakapowapata watu hao sheria itafuata mkondo wake mara moja.
 
Itungwe sheria ili kumtafsiri machinga ni nani? Na yupi ni machinga, na mfanyabiashara wa kati ni yupi na mdogo ni yupi?

N. B, wapo machinga wanauza mali zinazofanana na za madukani ajabu hawaghasiwi.
 
Serikali imewabana sana wafanyabiashara kiasi kwamba wanafilisika ndio maana wanatafuta mbinu mbadala na wewe Gwajima badala ya kuficha dhambi zao kama Mungu anavyoficha zako unawatangaza sasa subiri na wewe Mungu atatangaza dhambi zako
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia Wamachinga wadogo kuuza bidhaa zao ili kukwepa kodi.

Waziri amebainisha kuwa katika baadhi ya maeneo rafiki yaliyotengwa kwa ajili ya wamachinga, bado wameendelea kuona baadhi yao wakiondoka na kurudi barabarani, na baada ya kutafiti zaidi waligundua wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa kubeba biashara zao na kuuza bila utaratibu.

"Niwapelekee tu salamu, hawa ambao tumepata taaarifa zao tunaendelea na uchunguzi na tunasema hiyo siyo sawa tusijifiche kwenye migongo ya wamachinga na kuwashinikiza na kuwashawishi waende wakafanye biashara kwenye maeneo ambayo tulishasema siyo rasmi kwao.

Aidha, Waziri Gwajima amewaomba wamachinga kuacha kutumiwa na wafanyabiashara hao na kuahidi kuwa mara Serikali itakapowapata watu hao sheria itafuata mkondo wake mara moja.
Inaonekana mmevuna kwa kiasi cha kutosha na sasa mnataka kujifanya ndio mmegundua sasa wakati taarifa tuliwaletea miaka mingi kabla hata hamjaanzisha kampeni ya kuhamisha barabarani hawa ndugu!
 
Siasa tu, hakuna wa kuwagusa machinga, hao ni watu wenu na saa hii mumechelewa sana, machinga wana nguvu dhidi ya serikali na kuna hawa wa bodaboda na bajaji nao mumewalea mpaka sasa nao wanaanza kutoa amri barabarani na wakipingwa wanaweza hata kuua kwa umoja wao,
Samaki mkunje angali mbichi
Kabla hapajaharibika sana chukueni hatua vinginevyo mtajuta
 
Back
Top Bottom