Waziri Dkt. Gwajima: Machinga wanasaidia mahitaji ya haraka

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,757
4,305
1644396747267.png

Picha Dkt. Dorothy Gwajima

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema, masuala ya changamoto za Machinga ikiwemo kuhamahama, watazungumza na Mamlaka za Mikoa ili kuona namna Bora ya kutatua tatizo hilo, na hii itakuwa ni kwa nchi nzima.

Waziri Dkt. Gwajima amebainisha hayo baafa ya kukutana na Viongozi wa wamachinga Mkoa wa Mara na kuzungumza nao kuhusu changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.

"Machinga wasingekuwepo hivi mahitaji ya haraka haraka tungekuwa tunapata wapi? Hivyo kama Serikali tunathamini sana uwepo wenu" - Dkt. Gwajima

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mara, Charles Waitara, ameiomba Serikali kuendelea kuliratibu kundi hilo ili liweze kufanya shughuli katika mazingira wezeshi.

"Mhe. Waziri sisi tunakuwa waanzilishi wa eneo, lakini likishachangamka tunaondolewa, hii kwakweli inanyong'onyeza jitihada zetu, tunaimani chini ya Uongozi wako hili halitajitokeza" - Waitara.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom