Waziri Dkt. Kijaji: Serikali Haiko Tayari Kuwakwamisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kushindwa Kufikia Malengo Yao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI - SERIKALI HAIKO TAYARI KUKWAMISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUFIKIA MALENGO YAO

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali inatekeleza jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kutatua changamoto walizonazo.

Dkt. Kijaji amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Magodoro cha TANFOAM kilichopo Jijini Arusha kujionea shughuli za uzalishaji magodoro na kisikiliza changamoto walizonazo.

Aidha, Amesema Wizara yake inatekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambapo moja msingi yake ni kuondoa majukumu yanayofanana kati ya Taasisi ili kurahisisha ufanyaji biashara na uwekezaji nchini

Akiongea na uongozi wa kiwanda hicho, Dkt. Kijaji amezitaka Taasisi kuacha kufanya majukumu yanayofanana na kuzitaka kushirikiana katika kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao bali itawasaidia kukua na kuendelea kibiashara, kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha ufanyaji biashara wao unakuwa na tija na manufaa kwa Taifa .

Amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vishikwambi cha Tanztech kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza changamoto zao.

Aidha Dkt. Kijaji amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA katika mitaala ya elimu.

F2eJf1mWwAA2Qf2.jpg
F2eJf2GaMAAJTjO.jpg
F2eJf2OasAA6R6O.jpg
F2dmQtvXUAUkpcG.jpg
F2dmQtqWcAABpsm.jpg
F2dmQtzWsAELDW_.jpg
F2dmQtpXgAAHa-D.jpg
 
Back
Top Bottom