Waziri Charles Tizeba Live ndani ya 360 kuelezea uwepo wa chakula nchini

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Mahitaji ya chakula ni tani mil 13, serikali ilikuwa na akiba ya chakula tani mil 16, bado tumebakiwa na tani mil 3.

Mwaka jana tulikuwa na halmashauri 43 zilizozalisha chakula chini ya kiwango lakini bado tuna ziada ya chakula.

Maeneo mengi ya Tanzania yanatofautiana katika hali ya hewa, na upatikanaji wa chakula, bado hakuna njaa nchini.
 
Sasa tuelewe lipi? Hakuna njaa au kuna njaa??? Serikali isiwajaribu wananchi kama makopo. Ifikie mahali muache siasa kwenye mambo ya msingi.
7976706019606f3c0014c7375c9da873.jpg
 
Mahitaji ya chakula ni tani mil 13, serikali ilikuwa na akiba ya chakula tani mil 16, bado tumebakiwa na tani mil 3.

Mwaka jana tulikuwa na halmashauri 43 zilizozalisha chakula chini ya kiwango lakini bado tuna ziada ya chakula.

Maeneo mengi ya Tanzania yanatofautiana katika hali ya hewa, na upatikanaji wa chakula, bado hakuna njaa nchini.
Hivi nini tafsri ya njaa? Huenda mm naelewa tofaut lbda
 
mmh klauzi? ndo imekuwa shirika la kitaifa la utoaji wa taarifa hasa za kiserikali? vipi tena tbccm na radio uhuru nao wameanza kuhongwa na wafanyabiasha na wanasiasa?
 
Hii njaa nadhani ipo baadhi ya maeneo. Hapa Uyole stendi mkungu mmoja wa ndizi za kupika unauzwa elf 5 ukienda kiwila elf 4 ukiingia ndani huko buku 2
 
kwanini wasambaze huku hakuna njaa.?kwa hiyo chakula kisambazwe tu bila kuwepo njaa.

swissme
 
Wananchi wanashindia uji mitaani,waziri ana sifia mamilioni ya tani ya chakula kwenye maghala,wakati chakula cha kwenye maghala hakimsaidii mwananchi chochote.
 
Aliyesema kuna 'Zika' kinajulikana kilichompata, watu wanalinda maslahi jaman muwasamehe tu.
 
Hivi nini tafsri ya njaa? Huenda mm naelewa tofaut lbda
Kwa tafsiri ya kisukuma njaa ni pale unapokuwa huwa akiba ya chakula nyumbani hasa mahindi mtama na mpunga. Vingine vya ziada ni karanga, michembe(viazi vilivyokaushwa),kunde, mboga nk.
Haijalishi una hela au la
 
Ifikie mahali Rais wetu awe na msimamo unaoendana na matakwa ya wananchi vinginevo wananchi wataendelea kumchukia na mpaka kufikia 2020 atabaki yy na uvccm tu
 
Back
Top Bottom