Waziri Chami nae kalazwa India

Waziri Chami nae kalazwa India

Status
Not open for further replies.

Cha Moto

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
945
Reaction score
154
Wana JF,
Nimesikia uvumi kuwa Waziri Chami nae amelazwa na anatibiwa huko India, Je hii ni kweli?
Mwenye taarifa atuhabarishe.
 
Wana JF,
Nimesikia uvumi kuwa Waziri Chami nae amelazwa na anatibiwa huko India, Je hii ni kweli?
Mwenye taarifa atuhabarishe.

Maskini kikombe cha babu hakikufanya kazi wala kumsaidia.
 
Kodi zetu hizi watatibiana wao tuuuuuuuu jamani jamani tutaonana wabayaa kila mtu india mie naenda hosptali za kulipia mitaani nyie endeleeni tu
 
"Haumwi kama watu wanavyodhani, ni kwamba amejiskia vibaya kama watu wengine wanavyoweza kujiskia na hivyo amekwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi" hii ni kauli ya Naibu Waziri Kijana wa viwanda na biashara ndg Razaro Nyarandu alipoulizwa juu ya afya ya Bosi wake Dr Chami.

Hapa ninajiuliza maswali kadhaa!

Mosi, hivi Nyarandu anaposema anajiskia kama wanaweza kujiskia watu wengine, je hao watu wengine wakijiskia nao waende India?
Pili, hapa kwetu hakuna madaktari wa kufanya uchunguzi wa mtu akijiskia kawaida?

Tatu, anataka kutuambia kodi zetu zimewafanya wajisahau namna hiyo hata kama mtu akijiskia ugonjwa wa kawaida akafanye vipimo nje ya nchi?

Nne, inamaana viongozi wa nchi hii wanajua udhaifu wa hospitali zetu na hivyo hawaamini kuzitumia hata pale wanapojiskia kuumwa kawaida tu?
 
nami nimesikia leo asubuhi via rfa magazetini eti alipelekwa juzi

" MUNGU AMPONYE HARAKA "
 
"Haumwi kama watu wanavyodhani, ni kwamba amejiskia vibaya kama watu wengine wanavyoweza kujiskia na hivyo amekwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi" hii ni kauli ya Naibu Waziri Kijana wa viwanda na biashara ndg Razaro Nyarandu alipoulizwa juu ya afya ya Bosi wake Dr Chami.
These people should get serious with our country.....nashukuru sikumskia huyo naibu live akiongea huo upuuzi! :smash:
 
"Haumwi kama watu wanavyodhani, ni kwamba amejiskia vibaya kama watu wengine wanavyoweza kujiskia na hivyo amekwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi" hii ni kauli ya Naibu Waziri Kijana wa viwanda na biashara ndg Razaro Nyarandu alipoulizwa juu ya afya ya Bosi wake Dr Chami

Kama kujisikia vibaya kunamfanya aende India then, akipatikana na ugonjwa unaomfanya ajisikie vibaya anaona atapelekwa Marekani kutibiwa.. Hii ndio Tz, ukipiga mahesabu ya gharama za matibabu za mawaziri hao watatu utakuta ni zaida ya bajeti ya wizara ya Afya yenyewe
 
Hizi hospitali za bongo zina nini?. Wao India, sisi hapa hapa Tanzania. Kodi zetu wanatibiana tu.
 
Hivi serikali haiwezi kuwaleta hao madaktari wa kihindi pamoja na vifaa vyao hapa TZ kama madaktari wetu hawana uwezo wa kuwatibu wagonjwa wetu? Siyo tu viongozi wetu wanakwenda India, wananchi wengi sana wanakwenda huko kwa sababu hawana imani na na hospitali zetu.
 
hii nchi imefikia mahali inatia kichefuchefu wanaacha mahospitali yetu hakuna dawa watumishi maisha mabovu wao wanakimbilia kwenda kutibiwa nje inatia uchungu sana.
 
Mi wasi wasi wangu kuhusu wagonjwa walioko huko muda mrefu, inabidi wakae mkao wa kujilinda zaidi maana huwezi kujua hawa wagonjwa wapya ni kweli wagonjwa au wanaenda kwa kazi maalumu.

Nchi inahitaji mabadiliko ya lazima hakuna options!! we need the changes, na wazungu walishaona kipindi hiki ndo watuvune haswa mpaka tutoboke mifuko. Utasikia serikali imekopa, mara dharura, mara kampuni la kimarekani mara NGOs hadi machozi ya damu yatutoke.
 
Mimi naona kuna commission ya kutibiwa nje ya nchi ndo maana wanakimbilia huko nje
 
India ni rahisi hata hiyo Agakhan hapo Dar ni ghali. It is very cheap but with excellent matibabu. Wanavutia wateja kutoka pande zote za dunia. hata USA Australia na China wote wamo humo. Ni kwamba wale specialists mabingwa wamo kule hasa madoctor wa kutoka waCuba hawataki kulipwa ghali sana.
 
Huko India wanatibiwa bure nini?
Washenzi wakubwa, ndio maana hawaboreshi huduma za afya kwa sababu wao wanatibiwa nje. Nawashauri waanze ARV mapema na sio kusubiri mpaka waziwe. Sie wanyonge tutaendelea na miti shamba yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom