Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 60
- 1,237
Ndugu zangu, kutokana na usiri na harufu ya ufisadi kwenye mradi wa kilimo wa BBT nimelazimika kumuandikia barua waziri wa kilimo na kumpa siku 30 za kuweka wazi kwa umma taarifa na mchanganuo wa matumizi ya pesa za umma katika mradi huo.
Kwamba taarifa ya kutumia million 16+ kuandaa shamba la hekta moja ilinishitua na hivyo kufikiria hatua za kuchukua nikiwa kama mmoja ya watanzania wanaowajibika kukatwa Kodi, tozo na ushuru wa mazao ili kujenga taifa letu. Hivyo ndani ya siku 30 waziri wa kilimo asipo weka wazi taarifa hizo basi hatua inayofuata ni kwenda mahakamani kuiomba mahakama kuu Tanzania imlazimishe kutoa taarifa hizo kwa maslahi ya umma na ya kwangu binafsi kama mlipa Kodi.
Asanteni.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu