Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Maji wa Miji-28 kufanya kazi Usiku na Mchana ndani ya Kipindi cha Mwezi Julai na Agosti, akiagiza wananchi wa Miji ya Urambo, Kaliua na Sikonge mkoani Tabora kuanza kupata huduma ya Maji Mwezi Oktoba mwaka huu.
Wakati wa Ziara yake Wilayani Urambo leo Jumatano Julai 16, 2025 ya kukagua maendeleo ya kazi ya utekelezaji wa mradi huo, Waziri Aweso amebainisha kuwa serikali haina tatizo la fedha za utekelezaji wa mradi huo, akiagiza kuongezwa kwa rasilimali watu pamoja na kasi ya ujenzi ili kufikia Mwezi Oktoba huduma ya maji ipatikane kwa wananchi wa Tabora.
Pia soma Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Utekelezaji wa ahadi, Uzinduzi wa Miradi na utatuzi wa ghafla wa kero za wananchi
Katika hatua nyingine Aweso amebainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo wa Miji28 kutaifanikisha Wizara hiyo kuvuka lengo la Chama Cha Mapinduzi waliloliweka kwenye Ilani ys Uchaguzi ya 2020 kwani huduma ya Maji Vijijini itafikia asilimia 86 ikiwa ni zaidi ya asilimia 85 iliyowekwa na Ilani ya Chama hicho.
Aidha Mijini pia huduma ya maji itapatikana kwa asilimia 96.6 mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, huku lengo lililokuwepo awali likiwa ni serikali ya awamu ya sits kufanikisha huduma ya upatikanaji wa maji Mijini kwa asilimia 95 kufikia Mwaka 2025.
Waziri Aweso pia amebainisha kuwa ipo miradi mingine 1,000 inayotekelezwa kwenye maeneo ya Vijijini na Mijini, yote ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Gharama za mradi wa Miji28 kwa miji ya Urambo, Kaliua na Sikonge ni shilingi Bilioni 143, ukitarajiwa kuhudumua wananchi takribani 490 ambapo unahusisha ulazaji wa mambo makuu kwa zaidi ya Kilomita 190, ujenzi wa matenki 5 yenye ujazi wa Jumla ya lita 8,000,000 na mabomba ya usambazaji zaidi ya Kilomita 100- mradi ukianza Aprili 2023 na ukitarajiwa kukamilika Oktoba 2025.