Waziri atumia madaraka vibaya

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
16,314
24,197
Copy and paste from Majira

(http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=7116)

Ashirikiana na mtoto wa kigogo kuvunja sheria za Uhamiaji
*Ala njama kuwakamatisha kwa rushwa maofisa Uhamiaji, afeli

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Wizara nyeti katika Serikali ya Awamu ya Nne anadaiwa kutumia madaraka yake kutoa amri zisizo halali kwa kumlinda mtoto wa kigogo na kusababisha maofisa kadhaa wa Uhamiaji kukamatwa wakisingiziwa kupokea rushwa.

Tukio hilo anadaiwa kulifanya hivi karibuni baada ya maofisa wa Uhamiaji kukamata raia 12 wa Kenya na mmoja wa Ufilipino wanaodaiwa kufanya kazi katika kiwanda cha mtoto wa kigogo huyo ambaye ni Mbunge bila kuwa na vibali vya kuwaruhusu kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kinaaminika, tukio hilo lilitokea Juni 14 mwaka huu wilayani Kinondoni ambapo raia hao wa nje walikuwa wanajihusisha na ajira katika kiwanda cha Huawei ambacho kinadaiwa kumilikiwa na mtoto wa kigogo.

"Baada ya maofisa hao kufika hapo na kuwakamata watuhumiwa hao nao walipiga simu kwa bosi wao (mtoto wa kigogo), ambaye kwa muda huo inadaiwa alikuwa na Waziri huyo, hivyo walichofanya ni kupiga simu kwa ofisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Polisi na kutoa maelekezo na Waziri ya kukamatwa kwa maofisa hao kwa tuhuma za rushwa," kilidai chanzo hicho.

Wakati ukamataji huo ukiendelea, ghafla gari la askari Polisi lilifika mahali hapo na kuwakamata wale maofisa Uhamiaji ambao waliwapeleka moja kwa moja katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni, wakiwa na hao wahamiaji haramu.

Chanzo kilidai kuwa wakiwa pale na mahojiano yakiendelea, jopo la upelelezi lilibaini kuwa wale maofisa hawakuwa na hatia yoyote na wala hapakuwa na ushahidi wa rushwa, hivyo ilikuwa ni vigumu kuwalaza rumande.

"Huwezi kuamini, yule Waziri alifika kituoni hapo tena akiwa amevaa kaptula na alipofika aliwauliza wale maofisa kama wanamfahamu yeye...mimi ni Waziri wa...," kilisema chanzo chetu.

Kutokana na hali hiyo maofisa hao walibaki wanalalamika na kusema wanapoteza ari ya kufanya kazi kwani walikuwa kwenye kazi zao za kawaida, lakini Waziri kwa kumlinda mtoto wa kigogo mwenziwe alilazimika kuwasaliti wafanyakazi wake.

Wahamiaji ambao walikuwa wamekamatwa na maofisa hao ni Bw. Emmanuel Mkuro (35), Bw. David Mwinzi (34), Bw. Benjamin Gitau (28), Bw. Felix Mositeti (26), Bw. Bernard Owiti (28), Bw. Raphael Nzyuka (30) na Bw. Joseph Ntini (23).

Wengine ni Augustine Kimanzi (34), Bw. Samwel Gichiengu (33), Bw. Muteiti Kingesi (35), Bw. Justus Njogu (27) ambao ni raia wa Kenya na Bw. Rufino Martin (43) raia wa Ufilipino.

Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. John Msafiri, na kudaiwa kuwa Juni 14 mwaka huu, walikutwa wakijiingiza kwenye ajira katika kampuni ya Huawei bila vibali vya kuishi nchini.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo walikiri kutenda makosa hayo na mahakama iliwaamuru kulipa faini ya sh. 50,000 kila mmoja na walilipa faini hiyo.

Jitihada za kuwapata wahusika katika sakata hilo zilifanyika lakini simu zilikuwa zikiita tu bila majibu yoyote huku zingine zikijibiwa kuwa mmliki wa simu hiyo hayupo.
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
62

Mwandishi hajiamini kutaja jina la Waziri. Lord help us!

Udaku....
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,346
38,995
good point Kuhani.. ndio maana JF iko hapa..! si watupenyezee sisi wengine tuwaandikie kama vyanzo vyao ni vya kuaminika? Kuna Polisi yeyote Oysterbay nibeep!
 
Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,955
4,388
Jamani kwani hiyo Huawei ni ya mtoto gani wa kigogo?
Alafu tunaomba ambaye anadata tumumlike huyo waziri anaye lingia kazi yake.
 
Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,776
203
Naamini huyu mwandishi wa Majira ana news zote, na anatembelea humu, hebu mwaga kila kitu, hapa JF we talk openly, haya mambo ya mtoto wa fulani awe abave the law ndo kati ya yale tunayo yapigia kelele. Muanike hapa ili fahamu zimrudie kwamba naye ni mtanzania tu kama wengine, na hako ka cheo ka uwaziri ni dhamana tu!
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
Huyo waziri aanikwe, kama ni kuaibika ameshajiaibisha mwenyewe, aanikwe halafu awajibishwe na aliyempa huo uwaziri, la sivyo huo upuuzi hautakaa uishe! Mtu umepewa dhamana ya uongozi tayari ushajiona nusu-mungu, ovyo kabisa!
 
Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
May 24, 2008
3,736
2,135
MMh!! Hii habari naona ina utata, june 14 ni jumamosi na kampuni ya Huwawei ni kampuni ya wachina iko masaki ndio inayosambaza network ya 3G kwa makampuni ya simu hapa TZ kulikuwa na mtoto wa kigogo alishafanya kazi ktk kampuni hiyo ila ameshaacha kazi. kama kuna mtu ana taarifa zaidi na anamjua huyo waziri aliyehusika naomba atupe mwanga zaidi kuhusu hilo.
 
Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,866
2,433
msituletee habari za udaku ktk jf kama hamuwezi kutaja jina lake sasa mnataka tujadili hewa? au hii habari ni bora mngeituma uwazi labda wangewasaidia
 
Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
752
62
Habari zisizodhibitishwa waziri ni Masha na mtoto wa kigogo ni Kinjekitile.

Namkumbuka David Blunkett alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani, kisa! aliandika memo kuharakisha permit ya housegirl wa girl friend wake. Bongo peponi, anything which is impossible, ndani ya bongo is possible na watu wanaendelea kudunda.
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
Kutokana na hali hiyo maofisa hao walibaki wanalalamika na kusema wanapoteza ari ya kufanya kazi kwani walikuwa kwenye kazi zao za kawaida, lakini Waziri kwa kumlinda mtoto wa kigogo mwenziwe alilazimika kuwasaliti wafanyakazi wake.
Hiyo hapo bila shaka ni hint, Waziri ambaye polisi ni "wafanyakazi wake", could it be Mambo ya Ndani au? Just speculating here... mwenye habari yote aimwage humu ndani basi....
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
Habari zisizodhibitishwa waziri ni Masha na mtoto wa kigogo ni Kinjekitile.

Maktauwo, duh! kumbe ni Mheshimiwa sana Masha! Kama kweli ni yeye basi naona anapalilia katabia ka kutetea watoto wa vigogo... kaazi kweli kweli
 
Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
752
62
Habari zisizodhibitishwa waziri ni Masha na mtoto wa kigogo ni Kinjekitile.

Ni kweli habari habari zisizothibitishwa, kwani habari inasema mtoto huyo wa Kigogo ni mbunge hivyo anaweza kuwa Thomas Apson, na sio Kinjekitile ambaye sio mbunge kama unavyotaka ionekane.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
938
Masha sio waziri wa nyeti, huyo atakuwa ni Simba, unless mwandishi naye haelewi vizuri nyeti ni nini.

Badala ya kurusha majina ya watu ambao hatuna uhakika nao labda tunaganza kujaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo.
 
socrates

Member
Jun 26, 2008
15
0
Kwa hiyo mwandishi anataka sisi tubuni ni nani? Hii sio habari maana haijakamilika. If you can,t disclose him you are like him. 'The witness of a rat is another rat'
 
Sekenke

Senior Member
Mar 3, 2008
132
29
Masha sio waziri wa nyeti, huyo atakuwa ni Simba, unless mwandishi naye haelewi vizuri nyeti ni nini.

Badala ya kurusha majina ya watu ambao hatuna uhakika nao labda tunaganza kujaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo.
FMES, Heshima mbele, hapo kuna utata hapo... Huyo Mhishimiwa alikwenda na Bukta, hiyo Juni 14... haraka haraka, japo Simba aweza kwenda na bukta, kete inajilengesha zaidi kwa Masha... au...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom