Waziri apanda kizimbani: ...Kisa cha SANGAM SECURITAS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri apanda kizimbani: ...Kisa cha SANGAM SECURITAS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 18, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Waziri Valentino Madusha alishtakiwa kwa kuingilia mchakato wa utoaji na upatikanaji wa tenda ya kuchapisha vitambulisho vya Raia. Katika kesi iliyovutia Taifa Waziri huyo alisimama kizimbani kuhojiwa na upande wa mashtaka kuelezea nafasi yake na hasa jinsi alivyoitetea kampuni ya SANGAM SECURITAS: Mahakamani ilikuwa hivi katika siku ya kwanza.

  Waziri alikuwa amevaa suti kijivu yenye michirizi midogo sana ya rangi nyeusi, alivaa shati la rangi ya bluu nyepesi na kwenye shingo yake alitinga tai ya rangi nyekundu iliyowiva. Miwani yake yenye rangi ya redha ilimfanya aonekane kama profesa fulani wa vile vyuo vikuu vya watu weusi kule Marekani ambako alisoma. Mwendesha mashtaka alikuwa ni "mtu wa kawaida kawaida tu".

  Swali- Mwendesha Mashtaka: Ni makampuni mangapi yaliyolalamika kwako kuhusu mchakato wa tenda hii ya vitambulisho?

  Waziri Madusha (Jibu): Haikuwa kampuni moja bali tano.

  Swali: Kwenye barua yako kwa Waziri Mkuu ulisema kampuni ngapi zimelalamika kwako?

  Jibu: Sikumbuki mara moja nilisema ni ngapi hasa ila nilitolea mfano wa kampuni moja.

  Swali: Ngoja nikusomee barua yako hiyo ukurasa wa nne, Naomba ipokolewe kama kizibiti namba moja. Unasema hivi "baada ya kupitia taarifa ya Kamati ya tathmini (evaluation committee) na hasa kutokana na malalamiko niliyoyapokea toka Kampuni ya SANGAM SECURITAS niliona ipo haja ya kupata ufafanuzi" na pia unarudia kwenye ukurasa huo huo na kusema kuwa "Katika kikao hicho niliwafahamisha kuwa nimepokea malalamiko kutoka kwa mojawapo ya waombaji". Je, msomaji wa barua hiyo aelewe ulikuwa umepokea malalamiko kutoka makampuni mangapi?

  Jibu: Anaweza kuelewa vyovyote lakini haiondoi ukweli kuwa nilipokea malalamiko zaidi ya kampuni moja.

  Swali:
  Bw. Masha, wewe umesema kuwa umepokea malalamiko toka "kampuni ya" na pia umepokea malalamiko toka "mojawapo" ya waombaji, sasa mtu kwanini aelewe "vyovyote"? Ni lini neno "mojawapo" linamaa ya wingi?

  Jibu:
  Mimi msukuma kwetu mojawapo inaweza kumaanisha mambo mengi (ukumbi unaguna kwa kicheko).

  Swali: Je umewahi kukutana na maafisa wa kampuni ya SANGAM SECURITAS wakati wowote wa mchakato huu?

  Jibu: Una maana gani "kukutana"?

  Swali: Kwamba umewahi kuwasiliana nao aidha ana kwa ana, kwa njia ya barua, simu, barua pepe au kwa namna yoyote kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja nao?

  Jibu: Huku kukutana unakozungumzia una maana rasmi au siyo rasmi?

  Swali: Haijalishi kama rasmi au siyo rasmi! Umewahi kukutana nao wakati wowote kampuni hii?

  Jibu: Nilipokuwa Uswisi Mkurugenzi wa Kampuni hiyo alinialika kwa dakika chache kuangalia shughuli zao pale lakini sijui kama huko nikukutana!

  Swali: Mhe. Jaji naomba mahakama irekodi kuwa mshtakiwa amekubali kukutana na maafisa wa SANGAM SECURITAS huko Hispania?

  Jibu: Hapana Jaji, sijakubali! Mimi nimesema tu kuwa nilialikwa nichepukie pale mara moja wakati natoka Oman na sidhani kama ile unaweza kuiita kukutana.

  Jaji: Wakili endelea na maswali, karani, hakikisha umerekodi kuwa Bw. Masha alikutana na watu wa SANGAM.

  Swali:Umesema kwenye barua yako na umerudia mara kadhaa katika vyombo vya habari kuwa ulipokea malalamiko kutoka kampuni ya SANGAM SECURITAS na sasa umeongeza kuwa makampuni mengine pia yamelalamika kwako. Ni barua gani ulipokea kuhusu malalamiko hayo?

  Jibu:
  Sikusema nimepokea barua yoyote.

  Swali: Sasa ulipokea malalamiko hayo kwa namna gani?

  Jibu: SANGAM SECURITAS walilalamika kwangu, na mimi baada ya kuona kuwa malalamiko yao yana msingi niliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara yangu kutaka ufafanuzi kama nilivyosema kwenye barua yangu.

  Swali: Naomba nirudie tena, ulipokea malalamiko kwa njia au namna gani?

  Jibu: Kwani malalamiko yanatolewa kwa namna gani?

  Swali: Mhe. Jaji, naomba mshtakiwa yuko argumentative naomba umlazimishe ajibu swali.

  Wakili wa Utetezi: Mhe. Jaji, tayari Mshtakiwa ametoa jibu lake kuwa amepokea malalamiko sasa Wakili anachotaka kujua sijui ni kitu gani naona anataka kuipotezea mahakama hii muda tu!

  Jaji: Jongeeni hapa. (mawakili wanasogea kwenye meza ya Jaji, Mic zinazimwa na anawanong'oneza jambo huku kidole chake kikionekana kinainuliwa inuliwa juu kutilia mkazo)

  Jaji: Bw. Madusha iambie mahakama hii ulipokea malalamiko ya makampuni hayo kwa njia gani, kumbuka uko chini ya kiapo.

  Jibu:
  Nilizungumza nao ana kwa ana.

  Swali: Kwa hiyo katika wizara nzima ni wewe peke yako mwenye rekodi ya kukutana na wawakilishi wa makampuni hayo katika mazingira unayoyajua wewe ambayo unasema kuwa yalitosha kwa wewe kuandika barua?

  Wakili wa Utetezi:
  Objection your honor!

  Swali: Withdrawn naomba nilipange upya swali langu. Bw. Madusha, umepokea malalamiko kutoka kwa kampuni moja au nne, katika mazingira ambayo siyo rasmi, kwanini watu wasiamini kuwa kulikuwa na kukiuka taratibu?

  Jibu: Mimi nilifanya hayo yote kulinda maslahi ya Taifa na ni kutokana na mimi kuwasilisha malalamiko hayo mchakato ukaangaliwa upya na ndiyo maana mchakato ukaangaliwa upya, kwa hiyo mimi natakiwa kutazamwa kama shujaa na mtetezi siyo mhalifu kama unavyoashiria.

  Swali: Hivyo katika kuonesha uzalendo wako uko tayari hata kuvunja sheria ili uonekane kuwa shujaa?

  Wakili wa Utetezi: Objection your honor, Wakili anamhukumu mshtakiwa!

  Jaji: Wakili angalia mwelekeo wa maswali yako.

  Swali:Kwanini ulikubali kupokea malalamiko ya makampuni haya nje ya taratibu (informal) wakati wewe hauko kwenye mchakato wa Tenda na hakuna mahali popote ambapo ulimuita Katibu wako awe sehemu ya kusikiliza malalamiko hayo?

  Jibu: (kimya)

  Swali: Narudia tena, Kwanini ulikubali kupokea malalamiko ya makampuni haya nje ya taratibu (informal) wakati wewe hauko kwenye mchakato wa Tenda na hakuna mahali popote ambapo ulimuita Katibu wako awe sehemu ya kusikiliza malalamiko hayo?

  Jibu: Kutokana na ushauri wa wakili wangu sitopenda kujibu swali hili nikikwepa kujichongea mwenyewe.

  Swali: Kama wewe hauko katika mchakato kusimamia tenda au hata kukata rufaa, imekuwaje usikilize malalamiko ya makampuni manne badala ya kukataa kabisa kuyachukua malalamiko hayo na kuwaelekeza kwa Katibu wako Mkuu?

  Jibu: Kutokana na ushauri wa wakili wangu sitopenda kujibu swali hili nikikwepa kujichongea mwenyewe.

  Swali: Bw. Madusha unafikiri lolote ulilofanya kwenye hili linakaribiana na heshima ya uzalendo, utawala bora, na kuheshimu sheria?

  Jibu: Mimi ni Mwanasheria, nimesoma na kukulia Marekani. Nimerudi nchini kuijenga nchi yangu. Katika kufanya hivyo nimeshiriki katika mambo mbalimbali, nimeanzisha kampuni na kutoa ajira kwa watanzania wengi, nimechaguliwa na watu wa Isamilo na kuwa Mbunge, Rais ameamini katika uwezo wangu na amenidhamini wadhifa huu wa Uwaziri.

  Hivyo katika yote ambayo nimefanya hadi hivi sasa naona fahari kujiona mzalendo kitu ambacho wakosoaji wangu hawaamini. Watu wananionea wivu kwa sababu mimi ni kijana tena msomi, na wapo wanaoona natishisha maslahi yao. Kwa hiyo ndiyo mimi ni mzalendo wa kweli!

  Swali: (wakili ameongeza sauti na anazungumza kwa haraka huku akimkazia macho Waziri Madusha) Kwa hiyo ni huo uzalendo ndiyo umekufanya uwe tayari hata kuvunja sheria kutetea kile unachoamini ni maslahi ya nchi hata kuingilia mchakato wa tenda za wizara?

  Jibu: Mimi ni mzalendo (huku naye anaongeza sauti na uso wake uko serious na anagonga kingo ya kizimba kwa jazba). Yote niliyoyafanya hadi sasa ni kwa ajili ya nchi yangu!

  Swali: Hivyo kwa ajili ya nchi yako uko tayari kuvunja sheria Mhe. Madusha? Jibu swali!

  Jibu: Ndiyo!!! Niko tayari kufanya lolote kama maslahi ya nchi yangu yanatishiwa, niko tayari kukutana na mtu yeyote mahali popote na wakati wowote, niko tayari hata kuvunja sheria ya tenda na manunuzi ya serikali kama nikiona sheria hiyo ni kikwazo kwangu! Ndiyo.. now you have it!

  Wakili: Sina maswali ya ziada Mhe. Jaji!

  Waziri Madusha anatoka kizimbani huku akitengeneza tai, na akiiweka sawa miwani yake ya jua. Kipara chake ambacho kinaonekana kinang'ara kama kimetiwa samri kiliakisi taa za ukumbi huo. Anajipangusa mdomo huku baadhi ya watu wakinong'ona. Wanasubiri kesi hiyo itapoendelea tena kesho!!

  Disclaimer:
  Kisa hiki ni cha kutunga, mfanano wowote wa majina ya watu, mahali, na matukio halisi ni mambo ya kinasibu na matokeo ya ubunifu wa mtunzi.
   
  Last edited: Feb 19, 2009
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,495
  Trophy Points: 280
  haya Mkuu. Ngoja tusubiri hiyo kesho tuona vile itakuwa...naona kama picha kali sana hili...ngoja nivute popcorns hapa taratibu...LOL
   
 3. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri alishtakiwa na nani na lini hii mbona kienyeji enyeji hakuna kwenda bungeni kuhojiwa kwa undani moja kwa moja mahakamani hii imekaaje hatutaki kujifunza kosa kwa undani na kulitungia sheria for future generation huu si mchemsho.


  SAHIBA.
   
 4. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Man, This is Classic!, very beautiful indeed lol!, You've gotta make money out of it. as the matter of fact, Tanzania need a new generation of writers, Man you could be among of them!!!!!
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji, this is great man. Unajua hata kama jambo linapita hivi hivi bado tunapata nafasi ya kujifunza upande mwingine (mzuri) ungekuwaje. Congrats mpiganaji.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha... tutaona kesho mahakama itasema nini..
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  thank you for your kind words.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  asante.. the imagination of an imaginative person is sometimes very imaginary!
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hongera sana mkuu kwa kisa hiki..natamani iwe kama ulivyoandika,ngoja tusubiri na tuone....,hope itakuwa hivi..Uzidi kubarikiwa kwa kipaji chako hiki cha kucheza na maandishi......Bravo MMK
   
  Last edited by a moderator: Feb 19, 2009
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  MMKJJ,
  Siku zote nasema uandishi wako umekwenda shule. Mara nyingine ni vigumu sana wengi kukuelewa.
  Hapa tena unastahili pongezi zangu za dhati kwa ubunifu wako.
  Masha anatakiwa asome hapa na kuona jinsi anavyoweza kusimama mahakamani.
  Kama si leo au kesho, asubiri awamu ya rafiki yake Kikwete iishe ili tumsulubu wakati wewe umegombea 2010 na kufanikiwa. LOL
   
 11. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKJJ kwa nini usingewatumia jamaa wa Clouds FM watakapokuwa na huyu bwana live kesho?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wameshakuwa naye mapema leo, na nilijaribu lakini haikuwezekana. Nadhani, nitafanya mimi mwenyewe Masha akikubali ananikwepa kwa sababu nimeshamuandika vibaya!
   
 13. J

  Japhet Member

  #13
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 26, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du, wewe Noma!!!! Motoooo!!! Naona kama kweli vile. Tusubirie hukumu tu. Hapa hachomoki mtu. Hata wakili wa utetezi ameshindwa kumtetea...amebakia kusema.."objection your honour"! kila wakati. Kwenye kesi hii, jamaa huyu hatobebeka, haka akileta staff yake nzima (Including na wale ambao wameishazawadiwa ujaji) kwenye kampuni yake kumtetea!!!! hahahahahahaha...nomaaaa...balaaaaa...motooo....
   
 14. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  John ''Mwanakijiji'' Grisham in the making...
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Washushie Zecomedy!
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mzee Mwanakijiji!
  Awesome, dude!! Kumbe visa vya mawaziri wetu vinaweza kutengenezewa vitabu au movie kabisa. 'kukutana' siyo? Tunasubiri busara za jaji!
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hii nilikuwa sijaiona......yaani hapa imebidi mpaka wanangu waniulize Baba unacheka nini..........MMKJJ....safi sana Mkuu.....keep it up
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...Mkjj, wiki mbili hizi umekuwa na mashambulizi makali sana katika battleground-fikra. Pongezi nyingi. NN amekupatia a little portion of that hypersupernanoconcentratepimpasonic potion nini?!

  ...Kwenye hiki kisa, nadhani kungelileta ladha nzuri zaidi kama usingetoa jina la mhusika katika hayo majibishano. Ni kisa cha kujitungia hivyo si budi kuwa na majina ya kujitungia pia, hata kama sote tunaelewa kinachoendelea na wanaohusika. Just a little note on separation of real life characters from those on stage when pre-conceiving drama!!!!!
   
 19. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  angekuwa msafi asingekukimbia mkuu. Thanks for the beautifull art. Tutasambaza kama kawaida mkuu.
   
  Last edited: Feb 19, 2009
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  done!
   
Loading...