Waziri aibiwa akiwa gesti

Waziri aibiwa akiwa gesti

Huyu lazima alilizwa na mchepuko eti Asubuhi ndo anagundua kama kaibiwa??? Mh Waziri baki njia kuu michepuko siyo dili
 
Hapa lazima mchepuko umemuumbua

Ujue Hakuna dhambi mbaya Kama kuchepuka, hata Waziri Malima amewahi kuonja adha ya Mchepuko huyo aliyemkwapulia Vijicent yawezekana ni mmojawapo wa wale wenye Uchungu na Ufisadi huku maendeleo hayaonekani.
 
Huyu lazima alilizwa na mchepuko eti Asubuhi ndo anagundua kama kaibiwa??? Mh Waziri baki njia kuu michepuko siyo dili
Huu ni mda wa kuvuna Maana bajeti zikipita hujivinjari na Michepuko kisha baadae waende wakavune ile Bajeti waliyoipanda huko Dodoma.
 
Na Waandishi wetu
8th June 2014
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, anadaiwa kuporwa vitu mbalimbali zikiwamo nguo pamoja na fedha, wakati akiwa amelala kwenye moja ya nyumba za kulala wageni iliyoko mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Habari zilizoifikia NIPASHE Jumapili jana zilisema uhalifu huo dhidi ya Waziri ulifanywa usiku wa kuamkia jana.

Akithibitisha habari hizo Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo, alisema Dk Kamani ambaye ni mbunge wa jimbo la Busega (CCM) pia Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, aliibiwa usiku wa kuamkia jana.

" Ni kweli tukio hilo lipo. Lakini nipigie simu baadaye kwa sababu nipo kwenye kikao" alisema Kamanda Mkumbo.

Chanzo chetu ndani ya nyumba hiyo kilieleza kuwa vitu vilivyoibwa ni pamoja na nguo, kadi za benki na fedha taslimu, lakini kilikataa kutajwa gazetini.

Inadaiwa Waziri huyo alibaini kuwapo kwa wizi huo alipoamka asubuhi, na hivyo kutoa taarifa katika kituo cha polisi kwa ajili ya ufuatiliaji.

Jitihada za kumtafuta Dk Kamani hazikufanikiwa kwa vile simu yake japo iliita kwa muda mrefu lakini haikuwa na majibu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Hajaibiwa bali wananchi wamejichukulia mali zao... I wish awe ni mwanadada aliejigawia...
 
hapa tusubiri na picha za ajabu maana mapicha yamevuma kweli kipindi hiki
 
FUNGENI MILANGO TUPIGANE.....................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!111111111111:der::der::der::der:
 
Kama kuna mtu ana gazet la mtanzania(kma sikosei)habr hii imeandikwa vzr zaidi, kuwa wazr aliingia na mtu kulala, na taarifa zilipofika polic wazr akataka zisiwe puplic!! Ili kutunza hadhi yake,,, hii nchi bwana michepuo diliiii
 
Hawa maccm sijui yamelogwa au ni mungu anayaweka hadharani?moja limehamia kwa mchepuko mpaka likapata ngoma likajiua,lingine limepiga picha na mchepuko utafikiri lipo honey moon halali na hili lingine lilitaka kupiga mpaka cha saa 11.
 
Kwi! Kwi! Kwiiii!!!!

Mboni kicheko? Hivi umesahau ukipinda kona ukachepukia barabara yenye tope na mashimo kuna faida na hasara?Utafika haraka lakini angalia spring za gari yako!

Na pili yake amechukua haki yake yaani kodi yake na part ya keki ya Taifa,upo?
 
Kama kuna mtu ana gazet la mtanzania(kma sikosei)habr hii imeandikwa vzr zaidi, kuwa wazr aliingia na mtu kulala, na taarifa zilipofika polic wazr akataka zisiwe puplic!! Ili kutunza hadhi yake,,, hii nchi bwana michepuo diliiii

Halafu wao hawafi na kale kaugonjwa ketu,wao maradhi yao ni:

1.Pressure ya muda mrefu.
2.Kisukari.
3.Pressure ya ghafla.na wengine wanaweza wakaendelea.
 
Kama kuna mtu ana gazet la mtanzania(kma sikosei)habr hii imeandikwa vzr zaidi, kuwa wazr aliingia na mtu kulala, na taarifa zilipofika polic wazr akataka zisiwe puplic!! Ili kutunza hadhi yake,,, hii nchi bwana michepuo diliiii

Nimekuwa najiuliza muda mrefu kaibiwaje? Mlango au dirisha vilivunjwa? Hiyo guest house haina ulinzi? Kumbe Waziri alikuwa mgumu kulipia huduma, halafu wakiandikwa wanasema wanapakwa vinyesi na mahasimu wao wa kisiasa kumbe wanajipaka vinyesi wenyewe.

Vipi utetezi wake hauendani na ule wa mpiga kura kupelekewa juice na fedha taslim??
 
Mkuu.
Hapo nafikiri wewe ndiye umekosea. Nipashe Jumapili ni jina la gazeti. Ni sawa na wangetumia Jina lingine badala ya Nipashe Jumapili.

Hapo kwenye RED nadhani umegeuza kalenda juu chini:A S-confused1:
 
Hajaibiwa bali wananchi wamejichukulia mali zao... I wish awe ni mwanadada aliejigawia...

Ls man-19:34 Today-
Kama kuna mtu ana gazet la mtanzania(kma sikosei)habr hii imeandikwa vzr zaidi, kuwa wazr aliingia na mtu kulala, na taarifa zilipofika polic wazr akataka zisiwe puplic!! Ili kutunza hadhi yake,,, hii nchi bwana michepuo diliiii
 
Hapo kwenye RED nadhani umegeuza kalenda juu chini:A S-confused1:

Nadhani wewe ndo hauko sawa. Gazeti linaitwa Nipashe Jumapili. Angalia hata chanzo..... Ungetulia kidogo tu, usingekuwa na haja ya hicho ulichoandika.
 
Back
Top Bottom