Waziri agiza watumishi watatu Redio Sengerema kuwekwa ndani kwa ubadhirifu wa Milioni 28

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mathew Kundo ameagiza watumishi watatu wa Redio Sengerema ya wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kuwekwa ndani kwa muda usiojulikana kutokana na ubadhirifu wa Sh28 milioni

Wafanyakazi hao ni ofisa habari Halmashauri ya Sengerema, Silvanus Mdalami, meneja wa kituo hicho, Sostenes Tangalo pamoja mwanasheria Ilambona Mahuba.

Amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea kituo hicho na kubaini kuwepo kwa ubadhirifu huo.

Amesema wizara ilikipatia Kituo hicho Sh103 milioni kwa ajili ya kukisaidia Kituo hicho lakini katika uhakiki walibaini Sh28 milioni hazijulikani zilipo.

Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu amesema watumishi wa Halmashauri ya Sengerema si waadilifu kutokana na kutafuna fedha za Serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Daa! wataalam wetu wa siku hizi wanaburudisha sana.

Wahasibu wanalamba mbio!

Wengineo: "Aaa hiyo simpo mbona! Mimi mwenyewe nitaitolea maelezo, we nipe!!" Mwisho wa siku, majambo.
 
Redio sengerema? Iweje waziri aingilie kati redio ya kibinafsi, au ni ya serikali? Bila shaka itakua ni redio ya halmashauri. Sasa kama kila halmashauri itakua na redio vipi ubora wa vipindi vyao? Haitashangaza kijiji nacho kumiliki redio yake
 
Sasa si uchunguzi ufanyike kwanza.

Huyo mbunge mnafiki
Ukiona hivyo auditing imeishafanyika na mapungufu kuonekana wazi na auditors. Wahusika wameisha pigwa kitu kinaitwa "audit query" hata mara tatu, lakini maelezo yao hayakujitosheleza.

Hapo unasimamishwa kazi ili ujiandae kisaikolojia wakati HR akiandaa hatua zifaazo za kinidhamu
 
Ukiona hivyo auditing imeishafanyika na mapungufu kuonekana wazi na auditors. Wahusika wameisha pigwa kitu kinaitwa "audit query" hata mara tatu, lakini maelezo yao hayakujitosheleza...
Huu upigaji wa aina yake, hakuna mhasibu kati yao...hizi hela walizichota kwa njia gani
 
Redio sengerema? Iweje waziri aingilie kati redio ya kibinafsi, au ni ya serikali? Bila shaka itakua ni redio ya halmashauri. Sasa kama kila halmashauri itakua na redio vipi ubora wa vipindi vyao? Haitashangaza kijiji nacho kumiliki redio yake
Kwani ni kosa Halmashauri au kijiji kumiliki Radio?
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mathew Kundo ameagiza watumishi watatu wa Redio Sengerema ya wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kuwekwa ndani kwa muda usiojulikana kutokana na ubadhirifu wa Sh28 milioni

Wafanyakazi hao ni ofisa habari Halmashauri ya Sengerema, Silvanus Mdalami, meneja wa kituo hicho, Sostenes Tangalo pamoja mwanasheria Ilambona Mahuba.

Amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea kituo hicho na kubaini kuwepo kwa ubadhirifu huo.

Amesema wizara ilikipatia Kituo hicho Sh103 milioni kwa ajili ya kukisaidia Kituo hicho lakini katika uhakiki walibaini Sh28 milioni hazijulikani zilipo.

Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu amesema watumishi wa Halmashauri ya Sengerema si waadilifu kutokana na kutafuna fedha za Serikali.

Chanzo: Mwananchi

Waongeze Tozo tufidie hasara, sisi ni wazalendo tunaipenda serikali, waangalie kiasi gani twaweza waongeze kwenye tozo za miamala!
 
Back
Top Bottom