JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Hamis Ulega amesema suala la maji ya kuoshea maiti kudaiwa kutumika kuhifadhia Samaki halina uhakika na kwamba ni hisia tu.
Akijibu swali Bungeni kuhusu taarifa hizo ambapo inadaiwa matumizi ya maji hayo yanasababisha Saratani kwa walaji, amesema “Siyo kweli na ndio maana Makamu wa Rais (Phillip Mpango) ameagiza Wizara ya Afya ifanyie utafiti ili kama kuna kitu cha aina hiyo kizuiwe mara moja.
“Niwatoe hofu Watanzania, wapo salama na hakuna shaka yoyote juu ya taarifa hizo.”