Wazee wa lugha: SIJAMBO

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Wazee wa lugha, unapoulizwa 'hujambo' huwa unajibu 'sijambo'.
Hiyo inamaanisha upo mzima hakuna tatizo.
Vipi kama kuna tatizo?
Kuna kinyume cha sijambo? Neno lenyewe naliona kama lipo kwa kinyume tayari.
 
Duh! man, hakuna kinyume cha sijambo. mimi nadhani umejaribu kutenganisha "si-jambo" ukitenganisha inaleta maana tofauti.
 
Duh! man, hakuna kinyume cha sijambo. mimi nadhani umejaribu kutenganisha "si-jambo" ukitenganisha inaleta maana tofauti.

kiswahili huwa tunatamka hvyo hvyo. Hata vitabu vinaandika sijambo.
Hujambo mtoto mzuri, unajibu ' sijambo shkamoo'.
 
Mikorogano mingine hii! Mi nimeamua kulipotezea tu hili neno!! nalitumia inapobidi lakini huwa halipambi kiswahili changu kabisa.
 
Mikorogano mingine hii! Mi nimeamua kulipotezea tu hili neno!! nalitumia inapobidi lakini huwa halipambi kiswahili changu kabisa.

unatumia neno gani badala yake unapouliza hujambo?
 
Unapoulizwa hujambo na kama huna-jambo ndio unajibu sijambo,na kama una jambo,kwa mfano unaumwa utajibu,naumwa! au wakati mwingine mtu anajibu,aah wapi bwana hivyo hivyo sijambo ya kiswahili.
 
kama sio shwari hakuna neno moja litakaloelezea hiyo hali?

Husninyo,

Hujambo ya kiswahili inatumika kukuuliza hali yako.
Una hali gani? pia inaweza kuwa ni njia ya kukuuliza; una tatizo lolote?

Huyu mchangiaji ameiweka vizuri sana hapa.
Unapoulizwa hujambo na kama huna-jambo ndio unajibu sijambo,na kama una jambo,kwa mfano unaumwa utajibu,naumwa! au wakati mwingine mtu anajibu,aah wapi bwana hivyo hivyo sijambo ya kiswahili.

Sasa unapoulizwa ,hujambo? unajibu vile ulivyo. kama ..sijambo...naumwa...nina njaa. sijisikii vizuri, sina hela.

kwa tafsiri ya neno kwa neno ni kuwa...hujambo? maana yake Una jambo?
sijambo....sina jambo
sasa kama una jambo basi unamueleza huyo muulizaji jambo ulilonalo, au jambo lililokusibu, linalokusumbua..
 
Wazee wa lugha, unapoulizwa 'hujambo' huwa unajibu 'sijambo'.
Hiyo inamaanisha upo mzima hakuna tatizo.
Vipi kama kuna tatizo?
Kuna kinyume cha sijambo? Neno lenyewe naliona kama lipo kwa kinyume tayari.

Kipo kinyume chake lakini huwa kinahitaji maelezo au ufafanuo wa hilo jambo lenyewe.
kama ni kinyume tu ni hivi:-
Sijambo ---- Nijambo inamaanisha Nina jambo.

Una jambo...sina jambo
Hujambo ...Sijambo au nijambo.
 
hiyo nijambo inaleta maana ingawa sijawahi kuitumia wala kumsikia mtu.
Mara nyingi hata sehemu zenye matukio kama msiba, ukiwauliza hamjambo watakujibu hatujambo baada ya hapo ndio utapewa habari za msiba.
 
Wazee wa lugha, unapoulizwa 'hujambo' huwa unajibu 'sijambo'.
Hiyo inamaanisha upo mzima hakuna tatizo.
Vipi kama kuna tatizo?
Kuna kinyume cha sijambo? Neno lenyewe naliona kama lipo kwa kinyume tayari.
Sina ujambo.
 
Hujambo ni maamkizi tu na mara nyingi hujibiwa sijambo. Kiheshima, kiutamaduni na kimaadili hata kama mtu anaumwa taabani ukimwuliza "hujambo" atajibu "sijambo".
Lakini kwa kawaida maamkizi yetu hayaishi hapo tu, mengine mengi hufuata. Mfano:
A: Hujambo Ninyo?
Ninyo: Sijambo
A: Vipi watoto/jamaa/ nyumbani, hawajambo?
Ninyo: Hawajambo
A: Hali yako?
(Sasa hapa kama Ninyo anaumwa au ana shida ndo ataanza kuzungumza juu ya hali yake).

Kuhusu kinyume cha "hujambo", ingawaje inatumika mara chache sana hasa baina ya watu wenye ukaribu mkubwa, hutamka "Ah mwenzangu, "sina hujambo" yoyote. Hapo tarajia msululu wa magonjwa au matatizo yake.
 
Huyu atakuwa anatumia.....Mambo? jibu ni poa kama mambo mazuri,safi. Na nuksi tu kama mambo si shwari

hahahaha! Au shwari, barida, shkopa, mzuka, neto, shwanga!
Hapo mambo yamenyooka. Lol!
 
Wazee wa lugha, unapoulizwa 'hujambo' huwa unajibu 'sijambo'.
Hiyo inamaanisha upo mzima hakuna tatizo.
Vipi kama kuna tatizo?
Kuna kinyume cha sijambo? Neno lenyewe naliona kama lipo kwa kinyume tayari.
Walioliingiza neno hilo tokea mwanzo walifanya makosa kwani walitakiwa kuangalia sarufi ya kiswahili na kanuni zake. Neno lolote hata kama ni la kukopa ni lazima likubali kunyumbulika kwa kutumia viambishi awali na tamati. Pia, viambishi vikanushi kama si-jambo na hu-jambo vinaenda kinyume kabisa na unyambulikaji wa maneno ya Kiswahili.
Nilikuwa napita kuona kuna nini huku lakini nimbaini kumbe ndiko kwenye fani yangu, tupo pamoja
 
Back
Top Bottom