Wazee wa Kigoma wamuonya Spika Ndugai

Wazee wa Kigoma wamuonya Spika Ndugai

Huko Meru wazee wanavunja Chungu jumapili.
577af5c6cd173345993b08dfbece3e59.jpg
[/QUOTE DAB
Huko Meru wazee wanavunja Chungu jumapili.
577af5c6cd173345993b08dfbece3e59.jpg
Hii ndiyo silaha ya wanyonge dhidi ya kibri ya viongozi wanaojifanya nchi hii ni mali yao
 
Naona sasa viongozi wanaishi kwa kutishiana Nguvu za giza..
 
Hahaha kwa hiyo Zito kabla ya kufanya chochote kama kuhojiwa na hiyo kamati sijui ya maadili lazima apate kibali cha Wazee wa Kigoma? Wazee wakikataa?


Ndugai siku sio nyingi huo mdomo utapinda
 
huu mwaka huu

chondechonde hao wanaoenda kuvunja chungu kwa kilugha kubaja nyungu... ni hatari sana itapuputisha ukoo mzimaaa ... naomba wahusika wasitishe maana hio ni zaidi ya nyuklia balistick, tena wakitumia ile stail ya kuivisha ndizi kuwa mbivu... yaani sijui...

tusifike huko..
Hahahah nimecheka sana eti hicho ni zaidi ya ICBM...
Haki ya Mungu watu wamekata tamaa na Mungu wao maana wameomba weee Mungu hajibu
Sasa wamekata tamaa na serikali yao na kilichobaki ni kurudi kwenye asili kuongea na mizimu nao wakigoma sijui kimbilio litakuwa wapi
 
....tatizo la Ndugu Gai ni kufikiri kuwa Wabunge wako Bungeni na si wawakilishi wa Wananchi walio wachagua. Kwa sababu yeye ni Supika, haoni dhana ya Uwakilishi kwa sababu hasiami kuwasemea walomchagua. Ubunge ulukuwa NGAZI ya kukwea juu.
Ifike wakati sasa Katiba itenganishe kazi za Wabunge na madaraka mengine kama U-Supika, Uwaziri, U-RC na majukumu mengine yasiyokuwa ya Kibunge..
 
Zitto%20Kabwe.jpg

Wazee hao wanasema kitendo cha Spika kumzuia Zitto Kabwe kuongea bungeni ni sawa na kuwazuia wao wasiongee na shida zao zisiweze kutatuliwa na kudai inaonekana hiyo kauli imeshafanyiwa kazi na kitendo cha kumwita Zitto kwenye Kamati ni sawa na kupoteza muda tu na kudai jambo hilo halimtendei haki kijana wao Zitto Kabwe na wao wenyewe.

Aidha wazee hao wamemtaka Spika Job Ndugai na viongozi wengine wasiwe na kibri na watazame mambo ambayo yanawaonganisha kwa pamoja.

Chanzo.EATV

My take.

Ndugai kuwa makini usiwaudhi hao wazee wa kigoma,ukiwaudhi wakakasilika tafadhali usiwalaumu.

=====

Wazee wa Chama cha ACT Wazalendo, Mkoa wa Kigoma, endapo Spika wa Bunge, Job Ndugai atatekeleza azma ya kumkataza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuzungumza bungeni watamshtakia Mungu.

Pamoja na mambo mengine, wazee hao wamesema wamesikitishwa na kauli hiyo ya Spika na wamemruhusu Zitto kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya kumsikiliza kwa kina na kujiridhisha.

“Baada ya kusikia kauli za Spika dhidi ya Zitto, tulihitaji kufahamu sababu na kiini cha tatizo lililotokea, hivyo tulimuomba kijana wetu kurejea nyumbani Kigoma kuja kutueleza kabla ya kwenda kwenye kamati ili tupate fursa ya kufahamu kilichotokea,” imesema sehemu ya taarifa ya wazee hao.

Kwa mujibu wa taarifa yao waliyoitoa leo Septemba 15, wazee hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusema kitendo cha Spika kutoa kauli ya kumzuia Zitto kuzungumza katika kipindi chote cha ubunge wake ni kuwazuia wao na wananchi wa Kigoma kusemewa ndani ya bunge.

“Kitendo cha Spika kutoa kauli hiyo kinaashiria kwamba ameshamhukumu mbunge na kiongozi wetu, kwa hivyo kuitwa kwake kwenye kamati ni kupoteza wakati tu, jambo hili halimtendei haki kijana wetu na halitutendei haki sisi wazee tunaomtegemea atusemee.

“Tumesikitishwa na kauli za Spika Ndugai kwani siku zote sisi wazee wa Kigoma tumekuwa tukimuona na kumchukulia Job kama alivyo mtoto wetu Zitto, wawili hawa wamekuwa na mahusiano mema hata kufikia hatua ya kushiorikiana kwa karibu kwenye mazishi ya mama zao,” wamesema wazee hao.

Spika Ndugai alitoa kauli ya kutishia kumzuia Zitto bungeni kwa kipindi chote cha ubunge wake na asiende popote wakati akizungumza bungeni wiki hii kwa kile alichodai Zitto amemdhalilisha Spika na Bunge kuhusu ripoti ya Tanzanite na Almasi kuwasilishwa serikalini.
View attachment 588885



Hao wazee watakuwa alosto tu.....Zitto anaongea nini bungeni kwa niaba ya wananchi wake wa Kigoma? Yule ni mtu wa umbea tu na uchochezi.
 
Kiburi cha Ndugai is unprecedented kwa kiongozi wa uma.Lakini who did not foresee this coming?Mnakumbuka what happened wakati wa kinyang'anyiro cha ubunge kwenye jimbo lake?Sina haja ya kukumbushia, nadhani wafuatiliaji wa mambo watakuwa wanakumbaka.Kwangu Mimi tukio lile baya kabisa lilitosha kabisa kumuengua Ndugai kwenye kinyang'anyiro kile cha ubunge and consequently utumishi wa uma of such a high profile kama Uspika.Tulipiga kelele sana hapa JF,lakini nobody listened to us.Sasa,the real him is coming to the open,tusilalamike.
Kweli mkuu....na pia huko india wanakoendaga akili zingine huwa zinabaki hospital ya apollo...refer mwakyiembe harrison.
 
Wewe unajitoa ufahamu kwa kutoona kibri ndani ya Zitto! Basi vijana wenzagu ni majanga, huwezi kutaka uheshimiwr wewe huna nidhamu, tweets za Zitto kwa Ndugai hazikuwa za kiungwana kabisa hasa ukichukuli Zitto ni kijana msomi lakini nikisoma hicho kinachoitwa Tamko, naona ameegemea sokolewe na nguvu za giza! Aibuuu!!
Ni mwendo wa albadiri tuu....kama mumetenda haki halitokukutenibla kuwakuta bali litaturudia sie na zitto wetu tuliowakoseeni.
ALBADIR NDIO MKOMBOZI WETU DHIDI YA JAMUHURI YA WATU WASIOJULIKANA NA VIBARAKA WAO.
 
Kweli mkuu....na pia huko india wanakoendaga akili zingine huwa zinabaki hospital ya apollo...refer mwakyiembe harrison.
No,Ndugai ni mtu rough sana,na alikuwa hivyo hata kabla ya kwenda India.Kwa tabia yake, hastahili kuwa kwenye high profile job kama uspika na kuhudumia watu.
 
Back
Top Bottom