Chapakazi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2009
- 2,874
- 310
Baada ya kutokea mshangao mkubwa kwa wanaJF na maswali mengi kubaki wazi kutokana na kitendo cha Wazee wa Chadema kumwomba Mh Zitto kutogombea Wenyekiti wa Chadema, nadhani walifanya kitendo hicho kwa busara kutokana na Katiba ya Nchi. Ningependa kuweka kifungu husika:
39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.
Nadhani kama Zitto angeshinda uchaguzi wa kuwa mwenyekiti wa Chadema, ina maana Chadema isingeweza kuweka mgombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Lakini inawezekana kupitia Katiba ya Chadema, mgombea Urais sio lazima awe Mwenyekiti wa Chama. Lakini sijaona pendekezo hili katika Katiba ya Chama!!
Sina uhakika kama Wazee wa Chadema walikuja na jibu husika, au kama kuna watu wengine walioshatoa jibu 'sahihi' humu. Kwa maoni yangu, hii ndo ingekuwa sababu yao. Kama nimekosea...tujadili na kupata shule.