Wazee wa CHADEMA walifanya vyema kumweka Zitto kando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wa CHADEMA walifanya vyema kumweka Zitto kando

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chapakazi, Sep 17, 2009.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Baada ya kutokea mshangao mkubwa kwa wanaJF na maswali mengi kubaki wazi kutokana na kitendo cha Wazee wa Chadema kumwomba Mh Zitto kutogombea Wenyekiti wa Chadema, nadhani walifanya kitendo hicho kwa busara kutokana na Katiba ya Nchi. Ningependa kuweka kifungu husika:
  39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
  Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
  (a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
  mujibu wa Sheria ya Uraia.
  (b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
  (c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
  chama cha siasa;
  (d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
  wa Baraza la Wawakilishi,
  (e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
  Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
  Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
  kodi yoyote ya Serikali.


  Nadhani kama Zitto angeshinda uchaguzi wa kuwa mwenyekiti wa Chadema, ina maana Chadema isingeweza kuweka mgombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Lakini inawezekana kupitia Katiba ya Chadema, mgombea Urais sio lazima awe Mwenyekiti wa Chama. Lakini sijaona pendekezo hili katika Katiba ya Chama!!  Sina uhakika kama Wazee wa Chadema walikuja na jibu husika, au kama kuna watu wengine walioshatoa jibu 'sahihi' humu. Kwa maoni yangu, hii ndo ingekuwa sababu yao. Kama nimekosea...tujadili na kupata shule.
   
 2. E

  Engineer JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pumba tupu! Nani kakwambia lazima mwenyekiti wa chama ndiye awe mgombea wao urais?

  Mbona Mtei na Makani hawakuwahi kugombea urais?

  Kweli JF ina vihiyo maana kama hujui hilo kweli una hata uwezo wa kuchangia JF? Inaelekea hata kunyonya hujamaliza.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - What a great thinking!, ndani ya the home of the Great Thinkers! it is incredible!

  Respect.

  Kamanda FMEs!
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hahahaha...Una hasira mh. DUH!! inaelekea hukusoma post vizuri. Ningeomba hiyo sehemu inayotoa tamko hilo basi. Mimi sijaiona katika Katiba ya Chadema.
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Engineer,

  vipi umesoma vizuri msg ya mtoa mada..........?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sijaona connection yoyote jinsi katiba ya nchi ilivyowapa busara wazee wa chadema, pamoja na vifunvu ulivyovinukuu kwa sababu hata wewe mwenye umeshajijibu kuwa si lazima mwenyekitiw a Chadema ndiye awe mgombea urais
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Umekurupuka kujibu rafiki yangu. Ndo maana kuna msemo usemao "Hasira hasara". Yawezekana umejibu tu ukiwa na hasira zako na kumshambulia mwenzako na badala yake sasa wewe ndo unaonekana kuwa ni mtu wa ajabu katika ukumbi huu wa great thinkers. Mara nyingine hata kama mtu ametoa hoja ambayo wewe unaiona ina makosa jaribu kutumia lugha nzuri utaeleweka zaidi. Naomba kutoa hoja.
   
  Last edited: Sep 18, 2009
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mh, inaelekea sikueleza vizuri. Nilijaribu kupitia Katiba ya Chadema kabla ya kuweka hii post nikiwa naangalia kama wao kumnyima kugombea urais kupitia ticket ya chama ilikuwa ni uvunjaji wa Katiba ya Nchi. Lakini mpaka sasa sijaona kwenye Katiba yao jinsi wanavyomteua Mgombea wao. Basi i thought this might be the reason behind the decision. Na ndio maana nikasema kama nimekosea, fresh tu au sio? It's simple my reasoning might be wrong.
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Unajua uzuri wa hii post, na JF kwa ujumla, ni ukweli kwamba hii post inatuelimisha kwamba katiba yetu iko inconsistent and incoherent.

  What we need badly than anything else is constitutional reform.
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Expand comment yako zaidi basi mh. Mimi kitu ninachoona Katiba inaongelea avenue ya Urais lazima ipitie kwenye Chama, alafu papo hapo hai-regulate Vyama. Chama kikimnyima mtu uhuru wa maoni (kama CCM ilivyojaribu kumbinya Spika), hali inakuwaje?
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona ulikuwa unapata safari baridi nini?? Manake umemfyatukia mchangiaji bila kusoma vizuri alicho kiandika. Vipi lakini kyela hawajambo??
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa ufupi katiba ya Tanzania inahitaji marekebisho makubwa kwani ilitengenezwa wakati wa chama kimoja na ukiisoma maelezo mengi yanalenga mwongozo wa chama kimoja.

  Halafu hivi suala la mgombea binafsi limeishia wapi?? kwa sababu nilitaka nipambane na JK mwakani.
   
 13. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu nafikiri ingekuwa bora kupunguza munkari, kumwambia mwenzako kuwa hajamaliza kunyonya wakati na yeye ana uhuru wa kuchangia kile anachofikiria sidhani kama ni uungwana. Nafikiri mchangia mada aligusia kuwa Mwenyekiti wa chadema si lazima awe mgombea urais.
  Tafadhali muombe radhi, That's how JF works.
   
Loading...