Katika hali isiyo ya kawaida leo wananchi wa wilaya ya kyela wamekutana maeneo ya viwanja vya siasa kyela mjini kujadili hatma ya jimbo lao pamoja na afya ya mbunge wao Dr.H.Mwakyembe, ambaye afya yake bado si shwari.
Wananchi hao wamejadili kuwepo haja ya kufanya safari ya kwenda kumjulia hali mbunge wao.
Mkutano huu umekuja huku kukiwa na tetesi kwamba huenda kiongozi huyo akaruhusu wananchi kuchagua mtu mwingine wakuendesha shughuli za kisiasa jimboni hapa.
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
Wananchi hao wamejadili kuwepo haja ya kufanya safari ya kwenda kumjulia hali mbunge wao.
Mkutano huu umekuja huku kukiwa na tetesi kwamba huenda kiongozi huyo akaruhusu wananchi kuchagua mtu mwingine wakuendesha shughuli za kisiasa jimboni hapa.
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
[/FONT]Na Israel Mwaisaka, Kyela FM Radio
BAADHI ya Wazee na madiwani katika halmashauri ya wilaya Kyela wameazimia kuunda tume itakayokwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kutaka kujua tatizo la ugonjwa anaougua mbunge wa Kyela na naibu waziri wa ujenzi Dkt,Harrison Mwakyembe.
Azimio hilo limefikiwa jana kwa pamoja kufuatia mkutano wa hadhara uliokuwa umeitishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kyela na diwani wa kata ya Kyela mjini Bw, Gabriel Kipija ambapo moja kati ya ajenda za mkutano huo ilikuwa ni kutaka kuishinikiza serikali kueleza uwazi wa ugonjwa unaomsumbua Dkt, Mwakyembe hasa baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya watendaji wa serikali juu ya ugonjwa wa Mwakyembe.
Akizungumza katika kikao hicho mzee Benson Mwaikeke alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona serikali inakuwa na taarifa zinazokinzana miongoni miongoni mwa watendaji wake wa serikali ambapo taarifa ya DCI Manumba iliyosema kuwa Dkt, Mwakyembe akulishwa sumu imekinzana na taarifa ya waziri wa mambo ya ndani Vuai Nahodha ikiwa ni pamoja na ile ya waziri wa afya Dkt, Mponda.
Alisema kuwa kitendo hicho cha Dkt, Mwakyembe kuugua na kwenda kutibiwa katika hospitali ya kimataifa ya Apollo kule India wao kama watu wa Kyela wameumia kiasi kikubwa sana hivyo wanaposikia taarifa zinazokinzana juu ya ugonjwa wa Mwakyembe kati ya viongozi hao wa serikali ni bora sasa wamuonae Mhe. Dkt, Jakaya Kikwete ili aweze kubeba dhamana ya kuwaambia wananchi juu ya kile kinachomsumbua Dkt, Mwakyembe.
Diwani wa kata ya Bujonde Bw,Lameck Mwambafula kwa upande wake alisema kuwa ipo haja sasa kwa Rais ya kuhakikisha anamfukuza kazi DCI Manumba kutokana na taarifa yake ambayo anadai kuupotosha umma na kutaka kuuficha ukweli uliopo katika suala zima la kinachomsumbua mbunge wao na kuwa kutokana na hilo DCI Manumba amekosa sifa ya kuwa mtumishi ndani ya jeshi hilo la Polisi nchini na ipo haja ya kumfukuza kazi.
Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi wilayani Kyela Bw,Robinson Fongo alisema kuwa umefika wakati kwa jamii sasa kuhakikisha kuwa wanafanya maandamano ya amani yatakayoishinikiza serikali kuweza kutoa taarifa sahihi na kuachana na ubabaishaji uliopo kati ya watendaji wa serikali na kudai kuwa hilo peke yake inaonyesha ni jinsi gani viongozi wa nchi hii wasivyokuwa pamoja na kufanya kazi kama timu moja inayopelekea kila mmoja kuzungumza anavyotaka yeye.
Alisema kwa hari hiyo hawataweza kupata taarifa sahihi za kinachomsumbua Dkt,Mwakyembe kwa maana viongozi wote wa serikali kila mmoja anatamka atakavyo yeye na kuacha maadili ya yanayowaongoza kwenye utumishi wa umma na kuwa njia pekee ni maandamano tu na kuunda tume ya watu kwenda kumuona mhe,Rais na kmpelekea ujumbe huo wa watu wa Kyela.
Akiitimisha hoja hizo mwenyekiti huyo wa halmashauri Bw,Kipija alisema kuwa hoja hiyo wataifanyia kazi haraka na kuunda tume ambayo itawashirikisha watu mbalimbali wa wilaya Kyela bila ya kujali itikadi za kisiasa kwani lengo ni kutaka kuunda umoja utakaoweza kumfikishia taarifa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema kuwa licha ya hoja hiyo pia watazingatia ushauri uliotolewa na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw,Fongo ya kutaka kuitishwa kwa maandamano ya amani ili kuunyesha umma wa Watanzania kuwa sasa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na nchi hii