Wazee na madiwani Kyela kuunda tume kumuona rais juu ya ugonjwa wa Mwakyembe

I like this.

Huu ni upeo wa uelewa wa hali ya juu sana kwa watu hawa. I wish them all the best.

Mapambano yanaendelea.
 
Dah,

Hizi story tumezisikia sana nafikiri huu muda kama tumeshindwa kufuatilia hi tumuachie mungu pekee. Maana kuna sheria za kitabibu ambazo zina govern disclosure of patient info, KWANZA UNAWEZA KUTOA TAARIFA YA MGONJWA KWA MTU ANAYEMUUGUZA,KWA JAMII KAMA HUO UGONJWA UNAWEZA ULETE MADHARA KWA HIYO JAMII, KAMA KUNA KESI MAHAKAMANI NA INAHITAJI USHAIDI WA DAKTARI, nje ya hizo conditions mwenye ugonjwa anakuwa kwenye position ya yeye binafsi kusema kinachomsibu ko ugonjwa wa mtu inakuwa siri yake na daktari wake. Lakini kinachoshangaza hapa ni kuwa mh yeye anajua anaumwa nini, kama ameona serikali haiwezi kusema anaumwa nini si aseme huo ni ugonjwa wake mwenyewe.

Halafu napata taabu kwani nadhani dr alifika Kyela na hao wazee walikuwa na muda wa kujua na kumuuliza anasumbuliwa na nini. Personally nimemwona dr kama mbunge wangu na kumjulia hali (mzaliwa wa Kyela). So, hili suala naona tulitazame vizuri sio kila siku media zinataka kuuza kisa to discus ishu hizo bila kufikia solution. Hata ungekuwa ww mwandishi unaumwa daily unazungumziwa unaweza upoteze maisha haraka coz of ANXIETY(FEAR, HOFU).

Mimi ningewaomba wazee wangu watulie mpaka jamaa mwenyewe atakapoamua kusema maana kuendelea kuuza magazeti kwa kupiga kelele ambazo mimi nahisi ni za kinafiki haina maana ni kwa nini nasema za kinafiki (DR KAUGUA ALMOST 7months walikuwa wapi). Halafu hata kama sikai sana Kyela but at least naijua, imetawaliwa na MAKUNDI,VISA, UNAFIKI, NDO MAANA HATUENDELEI.

Mwisho nasisitiza mimi ni mzaliwa wa Kyela
 
WAZEE wilayani Kyela wametoa tamko zito kuhusu utata uliojificha juu ya ugonjwa usiojulikana unaomtafuna, Mbunge wao, Dk. Harrison Mwakyembe, na kufikia hatua ya kutaka kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete awaambie Watanzania endapo mtoto wao kapewa sumu au ni ugonjwa wa Mungu.
...Kabla hawajaenda, wamemuuliza Mhe. Mwakyembe? Kama kweli ni wazee, nategemea watakuwa angalau na busara ya kufanya hilo kwanza.
 
Watu waliohudhuria huo mkutano hawakuzidi hata 50 japo ulitangazwa kwa muda mrefu.

Kweli kyela sasa siasa zimewachosha sana. Sio tena Kyela ile ya Mwakyembe kupata ajali 2009 ambapo watu walijazana makanisani kuomba apate nafuu. Kyela ya 2012 kila mtu anaangalia mambo yake na ugumu wa maisha.

Mkuu utagombea tena kupitia CCM?
 
Wazee hawana kazi ya kufanya,badala ya kwenda kumuona mgonjwa na kujua anaumwa nini eti wanaunda tume kumuona rais!!!
 
Kuna mkuu mmoja hapa JF aliwai kuleta uzi mmoja makini sana kuwa "Hakuna haja ya kumuonea huruma Dr Mwakyembe,kwani anavuna alichopanda" kwa hiyo nyie watu wa Kyela tulieni...

Mkuu, unanukuu hata wendawazimu? Nina wasiwasi na wewe pia ...
 
Kuna mkuu mmoja hapa JF aliwai kuleta uzi mmoja makini sana kuwa "Hakuna haja ya kumuonea huruma Dr Mwakyembe,kwani anavuna alichopanda" kwa hiyo nyie watu wa Kyela tulieni...

Ule uzi unaouongelea niliusoma na kuufuatilia. Haukuwa na lolote jipya wala la msingi, bali kejeli za kisiasa zilizokosa upeo stahili wa uelewa mpana wa katiba. Uzi ule ulimlaumu Mwakyembe na wenzake "kushindwa kulimalizia suala la Richmond" na kuisambaratisha Serikali. Kwa upande wangu, Mwakyembe na wenzake, tena kwa ujasiri mkubwa, walileta mapinduzi ya fikra nchini kuwa inawezekana kumwondoa hata Rais mkidhamiria kuuweka ukweli mbele. Kazi yao haikumwondoa Waziri Mkuu na mawaziri wawili wa Nishati (Msabaha na Karamagi) tu, bali vilevile ulivunja Baraza la Mawaziri la Kikwete kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi. Vilevile, kazi yao ilivuka mipaka ya uwajibishaji katika jumuiya ya madola ambako viongozi wa serikali walioko madarakani huwajibishwa na vyama vya upinzani tu, si Wabunge wa chama tawala au chama chao! Akina Mwakyembe walituonesha kuwa wajibu wetu wote ni TAIFA KWANZA na siyo CHAMA KWANZA!
Sisi wengine, pamoja na Mkuu niliyemnukuu hapo juu, tunatakiwa tuendeleze hayo mapambano kwa vitendo siyo kwa blabla za kwenye JF huku tukificha hata majina yetu - eti "Only83", "Parachichi" n.k. Ni aibu kwa watu wazima kumtegemea mtu mmoja au wawili wafanye maajabu kwa niaba yetu huku sisi tukiwa waangaliaji, halafu anaugua Mwakyembe leo tunamdhihaki bila aibu! Subiri uugue wewe Bwana au Bibi "Only83", utakumbuka maneno yangu. God Bless Tanzania
 
Hawana lolote hao wazee wa kinyakyusa nao wanataka kitu juice ya whte house,kwa nn wasiende kwa mwakyembe mwenyewe au mkewe kumuuliza?
 
Dah,

Hizi story tumezisikia sana nafikiri huu muda kama tumeshindwa kufuatilia hi tumuachie mungu pekee. Maana kuna sheria za kitabibu ambazo zina govern disclosure of patient info, KWANZA UNAWEZA KUTOA TAARIFA YA MGONJWA KWA MTU ANAYEMUUGUZA,KWA JAMII KAMA HUO UGONJWA UNAWEZA ULETE MADHARA KWA HIYO JAMII, KAMA KUNA KESI MAHAKAMANI NA INAHITAJI USHAIDI WA DAKTARI, nje ya hizo conditions mwenye ugonjwa anakuwa kwenye position ya yeye binafsi kusema kinachomsibu ko ugonjwa wa mtu inakuwa siri yake na daktari wake. Lakini kinachoshangaza hapa ni kuwa mh yeye anajua anaumwa nini, kama ameona serikali haiwezi kusema anaumwa nini si aseme huo ni ugonjwa wake mwenyewe.

Halafu napata taabu kwani nadhani dr alifika Kyela na hao wazee walikuwa na muda wa kujua na kumuuliza anasumbuliwa na nini. Personally nimemwona dr kama mbunge wangu na kumjulia hali (mzaliwa wa Kyela). So, hili suala naona tulitazame vizuri sio kila siku media zinataka kuuza kisa to discus ishu hizo bila kufikia solution. Hata ungekuwa ww mwandishi unaumwa daily unazungumziwa unaweza upoteze maisha haraka coz of ANXIETY(FEAR, HOFU).

Mimi ningewaomba wazee wangu watulie mpaka jamaa mwenyewe atakapoamua kusema maana kuendelea kuuza magazeti kwa kupiga kelele ambazo mimi nahisi ni za kinafiki haina maana ni kwa nini nasema za kinafiki (DR KAUGUA ALMOST 7months walikuwa wapi). Halafu hata kama sikai sana Kyela but at least naijua, imetawaliwa na MAKUNDI,VISA, UNAFIKI, NDO MAANA HATUENDELEI.

Mwisho nasisitiza mimi ni mzaliwa wa Kyela

Mkuu,
Toka kuanza kuumwa Dr. Mwakyembe hajafika Kyela.

Mwenyekiti wa halmashauri na baadhi ya wana Kyela walimtembelea nyumbani kwake Dar.

Nakubaliana na wewe magazeti yanatumia ugonjwa Wa Dr kuuza magazeti yao.

Tumpe mgonjwa amani na nafasi ya kupumzika na sio kila siku habari zake magazetini.
 
Wanajanvi mimi kidogo natatanishwa na uamuzi wa wazee wa Kyela kutaka kwenda kwa Rais ili awaeleze juu ya ugonjwa unaomsibu mbunge wao!! Hivi kweli Rais anawezaje kujua maradhi yanayowasunbua wananchi [ hata kama ni mawaziri]; nauliza hivyo kwasababu ugonjwa unaomsibu mtu ni siri yake yeye na daktari wake na kama ni hivyo Rais atawezaje kwa nafasi yake kujua kitu kinachomsibu Mwakyembe bila mgonjwa mwenyewe kutoa taarifa.? Nina hakika Mwakyembe mwenyewe kisha waeleza wazee wa huko kwao vile vilivyogunduliwa na madaktari huko India na sidhani kama kumuona Rais kutabadilisha ukweli wa yale aliowaeleza.
 
Hawa wazee sasa wanatia aibu, mmoja amesikika akisema "tunataka Rais ajue kwamba wazee wa Kyela wamechukia", hapo hapo wanadai lengo la kwenda kwa Rais ni kujua kama Mwakyembe amepewa sumu au laa...sasa sijui kipi kilichowachukiza?....na huyu Rais anahusikaje na ugonjwa wa waziri wake? Kwanini hawakumuuliza/wamuulize huyo mgonjwa anayewafanya wachukie?
 
Wazee hawa wana haki ya kujibiwa,unataka ku2aminisha kuwa manumba alishawaeleza watanzania wakti ali2hadaa,nadhani wewe ni mmoja wa mamvi suppoters
 
Wazee hawa wana haki ya kujibiwa,unataka ku2aminisha kuwa manumba alishawaeleza watanzania wakti ali2hadaa,nadhani wewe ni mmoja wa mamvi suppoters

tumia ubongo wako hata chembe, sidhani kama kuna tatizo la kuwa mamvi supporter....we unaona kuna logic ndani ya kauli za hawa wazee?
 
Hao sio washili, wanaubongo, ngoja uone watakavyokuwa chachu ya mabadiliko nchini. Nawahusudu kwa uelewa wao.
 
Hao wazee wapuuzi kweli. Sasa wamuone rais kwani yeye ndio daktari wa Mwakyembe? Si wamfate Mwakyembe mwenyewe? Nakumbuka waliwahi kufunga safari kumuona Mkapa wakimpigia debe Mwandosya miaka ya nyuma so sishangai ndio tabia zao.
 
Mkweree toka wampopoe na mawe ana usongo na watu wa mkoa wa Mbeya hawezi kuonana nao!!
 
Siasa za tz, ni vigumu kutpinga maovu ukiwa ndani ya watawala, watakugeuka tu.
 
tumia ubongo wako hata chembe, sidhani kama kuna tatizo la kuwa mamvi supporter....we unaona kuna logic ndani ya kauli za hawa wazee?

Hawa Wazee Bure kabisa! Si wamuulize mgonjwa wao anachoumwa! Mwakyembe should stop use his illness as a political weapon! Aje aseme anaumwa nn! Kama ni sumu aseme! Sio kupiga siasa!
 
Sooner or later Itajulikana anaumwa nini na sidhani kama atakuja kutuambia ukweli.
 
Back
Top Bottom