Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Hili ni andiko bora sana kwakweli limeibua ishu muhimu sana ambapo kama jamii inabidi tujifunze sana

Mimi mchango wangu ni kwa ndoa ambazo zimeshindikana, wazazi mlio achana muwalew watoto mkijua kwamba tofauti zenu haziwahusu watoto wenu,wap wanastahili maisha yao yaendelee kama kana kwamba hakuna lolote ambalo limetokea

Mambo ya kuanza kuwatia watoto sumu ili mzazi mmoja aonekane ni mbaya,tambu kwamba haumkomoi mzazi mwenzako ila unawaharibu wanao na kuwafanya huko mbele ya safari wawe na mitazamo tofauti kwenye ndoa zao

Mfano mtoto wa kike akikua huku akipata sumu mbaya kuhusiana na baba yake,basi jua hatamchukulia vizur mume wake,atajua ndio wale wale tu

Na mtoto wa kiume akipata sumu kuhusu mama yake,hata akioa hata mchukulia vizur mke wake kwakuja ndio wale wale,kwahiyo kikubwa tuwajengee msingi mzuri watoto wetu

Na baba hakikisha baadhi ya mambo wanao ambao wamebaki kwa mama yao wanajua kwamba unayafanya wewe,nazungumzia watoto ambao ni wakubwa kidogo

Mathalani wanamahitaji fulani basi kupitia mama yao uongee nao ama kwa simu au ana kwa ana,wajue kuwa ni wewe ndio unasimamia mahitaji yao

Maana kuna mambo baba anafanya lakini mama hasemi baba yenu ndio amesimamia show,matokeo yake wababa huko mbeleni tunaonekana hatuja changia chochote kwenye malezi yao,hivyo watoto kupoteza upendo kwa baba yao

Najivunia sana my baby mama,though tumetengana lakini tunalea vijana wetu vizur sana,anaishi na wanangu lakini tunashirikiana vizur sana kwa malezi,na yeye kwa mapenzi yake huwa anawafanya watoto wajue baba yao nasimamia show nzima

Kwa kila mahitaji yao wananipigia simu na kuniambia nami naweka mambo kwenye mstari,kwahiyo hii inawajenga kujua kwamba ingawa baba yupo mbali nasi lakini anatupenda na kutuhudumia

Mwisho usisahau kuwaambia wanao japo mara moja moja kwamba unawependa,ina maana kubwa sana kwao.
Safi sana mkuu.
Hapo kutengana kwenu sio hindrance tena kwa malezi ya watoto wenu
 
Trauma huwa fanya watu kufanya vitu vya ajabu sana na wakaona wako right kwa namna yao

Kwa kipindi kirefu cha utoto nililelewa na shangazi yangu, tulilelewa vizuri alihakikisha tunakula na kwenda shule na kupata mahitaji muhimu
Changamoto ilikuja pale ambapo nilikua nikifanya makosa nilikua napigwa sana kupitiliza, nilikua napigwa fimbo za kila kona ya mwili isipokua kichwani ndio kulikua kunasalimika
Pia kugombezwa na kufinywa ilikua sana kwa makosa ambayo ni ya kitoto tu maana sikuwa hata mdokozi,
Kutokana na vile vipigo nimekua nikimuogopa sana kiasi kwamba ilipofika wakati natoka pale nyumbani nilipata ahueni
Changamoto ipo sasa hivi ukubwani hata nikiona simu yake inaita moyo unastuka japokua hakuna jambo lolote
Hii imepelekea hata mimi kupiga simu pale nyumbani iwe ni jambo zito kwa sababu ya ile hofu ambayo ilijengwa nikiwa mtoto na hili nimeligundua recently
Sasa wanalalamika sipigi simu home na mimi moyo ukitaka kunyanyua simu kupiga kiukweli nakua na hofu

Elevenn lost files
Pole mkuu,. My blood sister alipokua mdogo hata hajaanza shule alichukuliwa na ndugu yetu akaishi nae huyo mama aliemchukua mtu mkubwa sana kiuchumi,fame and all,sister akapelekwa shule nzuri,

Me nakua sister anakuja home kila likizo kama mgeni,mazingira ya home hayawezi vyakula sio vya kitajiri kama alipokulia,but kila December anakuja home,ana nguo mabegi 10 anagawa Kwa kila mtoto wa jirani,.maisha bora right?mama mkubwa wetu hanaga roho mbaya,sister hatukuhisi kama alikosa kitu..

Two years ago nipo na mama na sister sebuleni sister tayari ana watoto,anamuuliza mama kwa uchungu "Hivi mlikua na akili gani kunitelekeza mtoto ugenini???nyie wazazi bure kabisa sababu hakuna namna itakayofanya nimuache mtoto wangu kwa mtu mwingine,na nitawalaumu kwa dhambi yenu siku zote"
 
Ila mkuu hata hao transgender kuna ambao ni trauma jumlisha kukaa kwenye mazingira ambayo hivyo vitu vinahubiriwa sana. Kuna huyo niliona stori yake yeye alikuwa mdada, alikua mazingira ambayo wanawake wanateswa sana huku Afrika, akawa amechukia kuwa mwanamke yaani sana. Alivyoenda mambele kusoma hizo itikadi za transgender zikamuingia haswa akaamua kujibadili, alifikia hatua hadi ya kukata maziwa na alikuwa anaelekea kuondoa ovaries. Kupona kwake na kurudi kawaida ni kama muujiza na alibahatika kupata mume huko huko akaolewa. Sasahivi anapambana na madhara ya madawa na operesheni alizofanya wakati anahangaika kubadili jinsia.
Yes, kuna watu wanafanya surgery na kuchoma sindano za hormones out of trauma pia...

Aisee hii issue ni mbaya sana.

Na wengi hawana Emotional support
 
Sio sawa kabisa, nilishapigwa fimbo zaidi ya ishirini matakoni, matako yalivimba yakawa kama ukuni nilikua nakaa upande kwenye kiti kwa wiki mbili, worse enough sikuwa na wa kumwambia sio walimu wengine hata wazazi nyumbani
Ooh, pole jamani. Naelewa hiyo ya kukosa mtu wa kumwambia, ni feeling mbaya sana kwa mtoto kuhisi ameumizwa na hana mtu wa kumsikiliza. Ukiwa tu mtu mzima hivi halafu ukutwe na hiyo hali ya kutoona kuna mtu atakayekusikiliza huwa inaumiza sana,sasa hapo kwa mtoto ni mara 1000.
 
Asante kwa ushauri mzuri sana, bahati nzuri wote tupo dar hapa,kwahiyo huwa tunaonana,yani umepiga mule mule jana tu nilitaka niwafuate niende nao Beach wakafurahi lakini mambo yaliingiliana nimepanga next week inshallah

Kuna ishu my son kaniambia wanasafari ya Shule kwenda Ngorongoro tour,ingawa nimepata taarifa in short notice na inahitaji hela nyingi kidogo,lakini napambana aende ili awe na kumbukumbu nzuri zaidi,kwamba baba yake nimefanikisha safari yake ambayo itakuwa kumbukumbu nzuri kwake
Uza hata TV kama unayo nyumbani mtoto aende tour, hata suruali yako uza😂😂😂.
 
Asante @Elevenn en kwa bandiko zuri
Nowadays unazidi ku glow kwenye mabandiko yako
Really? Thanks 🙏
Na bado naona I still have to work on my writing
Hii issue ya wazazi kuonesha upendo kwa watoto ni kizungumkuti

Kwa sababu mzazi mwenyewe hakupewa upendo wa kutosha kwenye makuzi yake na hakupata ushauri nasaha akapona

Mf: Mama angu mzazi alikua mkali kupitiliza saiv kapunguza kwa sababu ya umri

Unadhani ataweza kutoa upendo kwa kiwango gani kwa mtoto?

Utasikia mzazi anasema, Mi nilikuwa napigwa na kijinga cha moto, alama hii hapa (ishara kwamba ana uchungu hajasahau &hajapona)

Anaona kukalipia bila mipaka, kutotoa muda wa kutosha kwa mtoto ni swala la kawaida kwa sababu hata hakupewa

Mzazi kama huyu hawezi kutoa upendo wa kutosha au muda kwa mtoto kwa sababu yeye hana mfano wa hilo

Lakini kwa sasa hivi kuna vitu tunafanya wala sio kwamba tulifundishwa nyumbani
Pole sana, walio umizwa maumivu sio physical tu.. Majeraha huenda mpaka kwenye nafsi, the pain body kwenye mwili hujuengeka na mtu huishi maisha yake yote ndani ya hayo maumivu...

Just know that and forgive her kwa yeye pia aliimizwa na just shukuru ya kuwa she's done her best raising you mpk kufikia leo.. Ni baraka pia

Sasa kwa wewe kugundua hilo ni kuanza kujiponya mwenyewe na fix kwa watoto wako yale mambo uliyokosa utotoni upendo, muda na nk....

Kwanzia kwako sasa kinaanza kutengenezwa kizazi kipya chenye history nzuri, huku kile kizazi chenye mtazamo hasi kuhusu muda na upendo kikizikwa

Sorry kwa kuchelewa kuja kuchangia, mdogo wangu, mambo yalikuwa mengi. 🙏🙏
Yes, atleast am trying. Najua sijafika ila with all I got now.. I can help build a strong and peaceful future generation.

Na unavyopenda kunidogosha sasa daah😂.
 
Pole mkuu,. My blood sister alipokua mdogo hata hajaanza shule alichukuliwa na ndugu yetu akaishi nae huyo mama aliemchukua mtu mkubwa sana kiuchumi,fame and all,sister akapelekwa shule nzuri,

Me nakua sister anakuja home kila likizo kama mgeni,mazingira ya home hayawezi vyakula sio vya kitajiri kama alipokulia,but kila December anakuja home,ana nguo mabegi 10 anagawa Kwa kila mtoto wa jirani,.maisha bora right?mama mkubwa wetu hanaga roho mbaya,sister hatukuhisi kama alikosa kitu..

Two years ago nipo na mama na sister sebuleni sister tayari ana watoto,anamuuliza mama kwa uchungu "Hivi mlikua na akili gani kunitelekeza mtoto ugenini???nyie wazazi bure kabisa sababu hakuna namna itakayofanya nimuache mtoto wangu kwa mtu mwingine,na nitawalaumu kwa dhambi yenu siku zote"
Umenikumbusha siku nimetembelea kituo cha kulelea watoto yatima, nilipata hisia kali sana kiasi kwa sasa kutembelea kituo cha watoto yatima siwezi. Niliwaangalia wale watoto halafu nikajiuliza, kwahiyo hawa ndo hawana wazazi ,babu, bibi, mjomba ,shangazi, mamdogo ?. Mimi binafsi nilikuwa napendwa sana na wajomba, bamdogo zangu pamoja na babu yangu ingawa walikuwa mbali na sisi. Nikajiuliza ina maana hawa sio tu kwamba hawajui upendo wa wazazi upoje, hata upendo wa bibi ,babu na wajomba au bamdogo hawaujui?. Wale watoto ndo wana trauma ya viwango visivyomithilika.
Mbaya zaidi kuna watoto walinambia wamepelekwa kituoni hapo na wazazi wao wa kuwazaaaa😭😭😭
 
Yes, kuna watu wanafanya surgery na kuchoma sindano za hormones out of trauma pia...

Aisee hii issue ni mbaya sana.

Na wengi hawana Emotional support
Na hiyo transgender ideology ni business inayozalisha mabilioni ya pesa maana ukishaanza kuchoma hayo madawa unaharibu ubongo kwahiyo unakuwa mteja wa kudumu wa dawa zao. Ndio maana wanaipush sana,wanataka kutengeneza wateja wengi wa kudumu wa hayo madawa.
 
Wanaume kweli mnapitia mengi na mnaambiwa ni mwiko kusema.
Mimi niko tufauti kidogo... Na wengi hunichukia kwa hiloo..
Mimi huwa nakuwa muwazi kihisia... Nionapo kitu hakija kaa sawa, huwa ni nasema tu.. Imenifanya niwe mpweke mwanzoni ila baadae nikajua issue sio mimi, ni mfumo.

Masculinity imekuwa toxicarsd Sana, hasa na capitalism. Healthy masculinity haiweki emotions pembeni
 
The same inakuwa kila mahusiano wanataka partner wao a play uhusika wa mama... Au kwasababu mtu alikosa upendo wa mama basi atamtreat huyo mwanamke na hostility kwa sababu hajawahi kushihudia baba akimtreat vyema mama yake.

Inaweza kuwa tofauti na hayo yote kulingana na how trauma imejijenga kwa muhusika
Ndo kitu napitia kwenye ndoa, Mume hajawahi kupata malezi ya mama....wazazi waliachana akalelewa na mama wa kambo kuanzia 4years old....nyieee balaa lake ni kubwa...ila Alhamdulillah nimepona, nimemjulia.
 
miaka mingi nyuma kulikuwa na mtu anayetumia jina kama hilo
naona mnafafana mapigo kwa kiasi kikubwa.
Hata mimi nahisi nilisha wahi kuona hiyo ID..
Ila sio mimi na mabandiko yake hata sikuwahi kusoma, au labda nilisema na sikuzingatia ID yake
 
Really? Thanks 🙏
Na bado naona I still have to work on my writing
Good job
Pole sana, walio umizwa maumivu sio physical tu.. Majeraha huenda mpaka kwenye nafsi, the pain body kwenye mwili hujuengeka na mtu huishi maisha yake yote ndani ya hayo maumivu...
Ya kale yamepita tunaishi leo
Just know that and forgive her kwa yeye pia aliimizwa na just shukuru ya kuwa she's done her best raising you mpk kufikia leo.. Ni baraka pia
We’ve forgiven them
We’ve taken the good from them and left the bad behind
Yes, atleast am trying. Najua sijafika ila with all I got now.. I can help build a strong and peaceful future generation.
✔️
Na unavyoenda kunidogosha sasa daah😂.
Tulia mtoto 😊
 
Good job

Ya kale yamepita tunaishi leo

We’ve forgiven them
We’ve taken the good from them and left the bad behind

✔️

Tulia mtoto 😊
Haya mshangazi Wacha niendelee kujihisi hivyo, nani asiyependa kuitwa mtoto? 😂
 
Ndo kitu napitia kwenye ndoa, Mume hajawahi kupata malezi ya mama....wazazi waliachana akalelewa na mama wa kambo kuanzia 4years old....nyieee balaa lake ni kubwa...ila Alhamdulillah nimepona, nimemjulia.
Pole kwa changamoto kipenzi,ila hakikisha na yeye anapona. Hiyo itakupunguzia mzigo wa kihisia unaobeba kwa Sasa. Kuwa mke na mama tu ni shughuli pevu, kuongezea mzigo mwingine sio poa. Pia akipona itasaidia asije kupeleka maumivu kwa watoto bila kujua.
 
Back
Top Bottom