Wazazi wenye watoto waliohitimu vyuo tusemezane kidogo

Tlmau

Member
May 12, 2019
11
14
Habari, natumaini uko salama na Leo nataka niongee na wazazi ambao Wana watoto ambao wamemaliza chuo na wako nyumbani bado hawajapata kitu maalumu cha kuwaingizia kipato.

Uzi unaanza..wazazi wengi ambao wana watoto waliomaliza chuo sasa hivi wengi wao ni wazazi ambao walikua wanaamini sana katika elimu,walikua wanaamini kwamba mtoto akipata elimu ni wazi kuwa kwa namna moja au nyingine wataweza kuendesha maisha yao kwa kuwa na kazi nzur pindi watakapomaliza masomo yao.

Kitu ambacho kwa miaka ya 2000 kweli watu wenye degree labda walikua ni watu wa maana sana kwenye nyanja zote kimaisha,kijamii pia walikua wanaheshimika sana, kitu ambacho kilipelekea wazazi wengi kuwaasa watoto wao wasome kwa bidii kwa kudhania ndio itakuwa ufunguo wa maisha Kama ambavo ilionekana kipindi hicho cha zamani kidogo.

Nadhani wengi tulikua hatutajajii Kama mambo yatakuja kubadilika Kama ilivo sasa ..kwamba wale watoto tuliowakazania wasome angali hata wengine walikua hawapendi kusoma walilazimika kusoma kwa kuamini maisha yao yatabadilika baada ya kusoma

Elimu yetu iko na mchanganyiko wa vitu vingi sana ambavo mwanafunzi anasoma kwa wakati mmoja,sio elimu ambayo inanfanya mwanafunzi ajitambue yeye ni nani na anataka kufanya nini katika maisha yake na ndio maana unaweza ukakuta mtu amesoma hadi kidato cha sita ukimuuliza unaenda kusomea nini chuo anakwambia bado nafikiria au sijui (usisahau sio yeye ni mfumo ambao amejengewa kwa miaka zaidi ya 13) ambao inanfanya mtoto kuwa Kama hajui dhumuni lake maishani ni nini na inabidi ufahamu kitu ambacho kimetengenezwa kwa miaka 13 akilini kwa mtu kukitengua ndai ya mwaka au hata miaka miwili ni ngumu sana na binadamu tumetofautiana, mtu anajaza zile form za kuenda chuo anajaza course tano tofauti kwamba kitakacho kubali ndo ataenda kusomea,hii ni ishara kwamba Kuna shida sehemu na hii yote shida kubwa ni mfumo tulionao, muda mwingine wazazi wanapenda watoto wao wasome vitu ambavo mzazi unataka sio mtoto anachotaka na pia wazazi hatuwasaidii watoto wetu kujitambua. Tusiwalaumu sana watoto wala kuona Kama wanakula bure tu hapo nyumbani

Mtoto kajitahidi kasoma vizuri kwa miaka 17 la kwanza hadi chuo kamaliza na vyeti vizuri hii yote kwasababu ulimsihi asome na kumuaminisha kwamba elimu ndo kila kitu kwake, kitu ambacho kimenifanya niandike hivi ni, limekua na wimbi kubwa la wazazi ambao Wana waendesha vibaya watoto wao baada ya kumaliza chuo na kukaa nyumbani kwa muda bila ajira na kuwaona kwamba hata kujiongeza hawawezi, ngoja nikwambie kitu watoto wako wanjiongeza sana inawezekana hauoni lkn me naamini wanapambana sana, hamna mtoto ambae amemaliza chuo na anafurahia kula kulala nyumbani bila kuwa na shughuli ya maana ya kufanya, vinaja wanapambana;

Kama aliweza kusoma kwa miaka 17 kwa elimu ambayo sio rafiki kwa dunia ya sasa unshidwa vipi kumvumilia hata kwa miaka mitano ajitafute ajipate afanye mambo yake,ikiwezekana kaa nae mwambie tu mwanagu unataka nikusaidiaje,unataka kufanya nini nikusupport, wazazi tuache kukimbia majukumu naamini huyo mwanao hakuja gafla duniani ulimleta wewe, mwanao ni jukumu lako.

Kama wanyama pori wakizaa watoto wao wanawafundisha hadi kuwinda kwanza wakijua ndo wanaachana nao, ww mzazi ni kweli mnyama pori anakuzidi uelevu wa kulea watoto wao...msaidie mwanao asimame Hilo ni jukumu lako asanteni.
 
Sentensi ya mwisho ndo ya maana kwa yoote uliyoyaandika hapa. Kwamba tunashindwaje na wanyama ambao huwafundisha watoto wao maisha, kujitafutia maisha.

Na ukumbuke kuwahimiza watoto kusoma ni njia ya kufundisha jinsi ya kutafuta maisha pia usibeze elimu
 
Mkuu umeongea points sana kutokana na hali ya maisha wazazi hawajui kitu kuna kitu kinaitwa kulinganisha hapa watu wanafeli japo ni ngumu sana kuepuka ila inachangia katika wazazi kuwalaumu watoto wao mbona fulani yuko japo alimaliza miaka ya 2005 huku ila anafananisha na mwanae aliyemaliza 2019

usione watu wanajazana hapa dar hyo ndo sababu wanaogopa buguzi ila ni wazazi wa kisasa
 
Elimu ni ya muhimu sana nadhani wewe pia umesoma ujuzi wa chochote una kuwa na ufanisi mkubwa ukiwa vizuri kichwani
 
Ni kweli but elimu ya 17yrs +second class gpa at varsity havijawahi kunipa pesa 😄
 
Back
Top Bottom