Wazazi wa NILSA watofautiana ishu ya michango

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2024
Posts
647
Reaction score
1,141
“Baada ya Kifo cha Nilsa: Wazazi Watofautiana Kwa Pesa za Michango!” 🤔💔

Inadaiwa kuwa kwa sasa kuna sintofahamu kubwa kati ya Baba na Mama wa marehemu Nilsa, kufuatia tuhuma nzito za matumizi mabaya ya fedha za michango ya matibabu ya mtoto wao.

Mtoto Nilsa, ambaye alizaliwa na kuishi na changamoto za kiafya kwa muda mrefu, alifariki dunia Januari 18, 2026, tukio lililogusa hisia za wengi waliokuwa wakifuatilia hali yake.

Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo, chanzo kikuu cha mgogoro huo ni fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya matibabu ya Nilsa. Mama huyo anadai kuwa Baba wa mtoto alitumia sehemu kubwa ya fedha hizo kwa manufaa yake binafsi, ikiwemo kununua gari na kuanzisha biashara, huku yeye akipewa kiasi kidogo sana.

Taarifa hizi zimezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku wengi wakitaka ukweli ujulikane na haki itendeke kuhusu michango ya wananchi.

#tanzania #fblifestyle
 
Ukiona watu wanagombana ni pesa inahusika, amove on kugombea pesa za michango sio deal
 
Ndio Nani naye tena huyo huko Dar..
Mbna umeandika kama wote tupo huko?!
 
Nilsa ni huyu mtoto mdogo hapo kwenye picha akiwa na baba ake
IMG_7763.jpeg

Wakati anaumwa baba ake aliomba kwa jamii hela ya MCHANGO wa matibabu ya mwanae

Jamii ikachangia na inavyosemekana ilipatikana milion 17 kwa mujibu wa mama wa mtoto

Wakati anaendelea na Matibabu Nilsa akafariki (RIP)

Sasa shida imekuja kwenye hela ya MCHANGO Mama analalamika kuwa kwenye hela alipewa milion 3 peke ake na Akaambiwa nyengine imetumika kwenye matibabu

Kwahiyo ugomvi wao Upo hapo kwenye kugombea hela ya MCHANGO wa matibabu ya mtoto
 
Hii itafanya hata wenye moyo wa kuwasaidia wenye matatizo ya kweli, warudi nyuma
 
Back
Top Bottom