K-killer
Senior Member
- Nov 14, 2011
- 147
- 28
Ndugu zangu wanaJF
Nimekuwa kwenye mahusiano na binti mmoja wa kichagga kwa mwaka mmoja sasa,na kama mjuavyo siku zote mahusiano ya watu wazima wawili yanahitimishwa na ndoasasa ishu yenyewe ipo hivi .
Wazazi,ndugu,marafiki kwa asilimia kubwa hakuna anayeniunga mkono katika suala la kumuoa binti huyu,na sababu yao ya msingi ni kwmba ni MCHAGGA.wamejaribu kunieleza kwa mifano hali halisi na tabia za watu wa kabila hili waliowahi kuolewa na ndugu zetu na effects walizozileta kwenye familia zao.
Ukweli ni kwamba yote niliyoelezwa ni sahihi na mifano ninaiona pamoja na matatizo yao kweli yanaonekana kwa mtu yeyote mwenye uelewa mzuri katika kutafuta ushauri nikashauriwa kwamba ni vema nimweleze mwezangu hali halisi na kutowezekana kwa ndoa kuwepokwa manufaa yetu wote yaani mimi nay eye,
Tatizo limekuja katika kuipokea habari yenyewe,dada wa watu kaipokea negatively na anadai namzingua,ukweli ni kwamba mimi sipo tayari kuwa nae kulingana na sababu nilizomweleza ambazo ni za msingi Kabisa,sasa jamani nahitaji ushauri wenu wa dhati jinsi gani niweze kumwelewesha dada huyu ilia aache kulia lia na kuangalia mambo yake mengine hasa shule maana ndo kwanza yupo mwaka wa pili katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini
Nawasilisha wakuu
Naamini kabisa kua thinking capaacity yakoo nii zero.Wakati unaantongoza hadi ukakubaliana nae utamuoa ni wazi kua mlikaa kipindi cha mwaka na unamjua tabia zake kiundani zaidi,iweje leo mzazi na ndugu wakuambie kua hafai na wewe ukubaliane nao?akili yako itakua haipo sawa.
Hao ndugu zako watAkuchagulia mke wamtakao wao au itakuaje?maana katika dunia hii hamna mwanamke perfect inabidi ukubali mapungufu yake of wich najua ulishayakubali ndo maana mmedumu mwaka,iwaje leo umuone hafai kisa ndugu na wazazi?au ukimuoa na wao watakua wanakusaidia ku jig jig?ndo maana wanamuona hana mvuto kwao.Mapenzi ni ya wawili hayahusishi ndugu wala wazazi,wao wanatakiwa tuu wakupeni baraka kwenye ndoa yenu muishi kwa amani na upendo.
Ni dhahiri kabisa hukumpenda huyu dada na unamchezea tuu,maana kama kweli unampenda basi ungeachana na mawazo finyu ya familia na kutengeneza familia yako na huyo msichana,Maisha yA hao ndugu zako na wazazi kwa upande wao yashaishA wanakaribia kuuacha ulimwengu,huu ni wakati wako wewe sasa kuanza yako ili kutengeneza maisha yako yenye furaha na amani.Usiwe mpumbavu wakufikiri,kabila si kitu we kijana.Alafu kesho unamlalamikia MZUNGU anaku discriminate because wewe mtu mweusi!To hell with you,acha aku discriminate mjinga kama wewe ambaye una discriminate kabila tuu wakati wote weusi.Nitashangaa sana kama utakua ni msomi alafu upeo wako wakufikiria na maamuzi ndo huu.