Ushauri: Ndugu wamsusia majukumu

Ushauri: Ndugu wamsusia majukumu

puker

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
1,057
Reaction score
2,195
Kuna binti nipo nae kwenye mahusiano kwa muda kidogo. Kipindi chote tulichokuwa kwenye mahusiano tumepita kwenye nyakati tofauti ngumu na nzuri.

Ukweli ni kwamba, mwenzangu kwa bahati mbaya amepoteza wazazi wote wa wili angali akiwa mdogo.

Hvy kwa malezi amelelewa na ndugu zake mpaka kufikia umri wa kujitegemea. Changamoto ni kwamba mwaka 2017. Dada yake mkubwa alipata tatizo la ajira...lililosababista kupata tatizo la kiharusi (strock) ya mwili mzima. Hali iliyomfanya kuhudumiwa kwa kila kitu.

Balaa ni kwamba ndugu wamemsusia huyu dada jukumu la kumlea mgoja toka 2018..jambo lililomfanya ashindww kabisa kuendelea na mambo mengine binafsi ikiwa ni pamoja na swala la yeye kupata kazi.

Upande wangu tulipanga kuoana toka mwaka 2019. Lakoni hii changamoto imekuwa kikwazo katika jambo hili muhimu...nimeshindwa kuendelea na taratibu muhimu nikihofia jambo hili kama ndugu wenyewe hawatoi ushirikiano naona kama inaweza niletea shida.

Kama ni kuvumilia na kujitoka nimejitahidi sana lakini naona kabisa jambo hili linakwenda kunishinda ndugu...zangu naombeni ushauri katika hili...[emoji120]

Natanguliza shukrani.
 
Unajitesa na kubeba misaraba ya watu wengine ....bible inasema kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe...Sasa unataka sisi tukushauri Nini
 
na usikute una mdogo wako ana hustle hujawahi kujitoa km kwa huyo.



anyway


toa kwa muda muafaka huenda pesa unayoitoa ni baraka za huyo mgonjwa utazitambua pindi utapoacha kumhudumia na zenyewe zikakukimbia.
 
Sa unasubiri nn maana kuanzisha Uzi tu ni jibu lako tosha
 
Umechaguliwa yeye kumlea huyo mhitaji .. Ni kipimo unapimiwa.. Ni mtihani unatahiniwa..

Endelea kumsaidia malipo yake utayaona.. Si kutoka kwa ndugu bali ASILI ITATENDA
 
su muweke beki 3 ishue kwishaaa.....hv kwann siku hizi JF una uzi za kijingaa
Hata beki tatu akiwepo lazima awepo na ndugu yake maana kuna mambo beki 3 hawez yafanya kila kitu anafanya hapo hapo anahitaji intensive care and love sio rahisi kupata mtu wa hivyo ambae sio ndugu yake
 
Back
Top Bottom