Ndoa ni agano la milele

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
NDOA NI AGANO LA MILELE

Neno la Mungu linasema,
MATHAYO 19:3-12
"Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

Akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.

Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee."

NDOA ni makubaliano ya mume na mke kuishi pamoja siku zote za maisha yao.

Mume na mke wakishaingia katika ndoa ina maana kwamba wametia sign katika mkataba wa maisha ya milele.

Na ukishakubali maisha ya milele pamoja, ina maana kuwa mume au mke hapaswi kuanzisha mahusiano na mtu mwingine.

Neno linasema,
"Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

Lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe."
1WAKORINTHO 7:10-11

"Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu.

Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu."
1WAKORINTHO 7:39-40

KABLA ya kuingia kwenye maisha ya NDOA, tafakari kwa kina maandiko haya, usije ukaingia dhambini.

#No_learnig_No_earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
#kataa ndoa
#ndoa ni ukatili
#ndoa ni mateso


ndoa ilikuwa enzi hizo za mababu zetu huko
 

Attachments

  • VID-20231102-WA0012.mp4
    3.4 MB
Imeandikwa mtu asimwache mkewe isipokuwa kwa uzinzi.
 
Back
Top Bottom