Wazazi Miss Tanzania wadai chao

Wazazi Miss Tanzania wadai chao

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,309

Arusha. Wazazi wa Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania iwape maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa hadi sasa wako njiapanda.

Kauli hiyo ya Eva na Deus Kamazima imekuja siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam.

Wakizungumza nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.

Walisema kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.

“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti.

Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika.

“Sijapewa taji wala zawadi , lakini kitendo cha kupewa kiti cha umalkia nimeridhika,” alisema Lilian.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema kuwa ni kweli bado hawajamkabidhi fedha na zawadi kwa kuwa kuna taratibu za kiofisi bado zinafanyika.

“Ni kweli, tulimwambia atuachie akaunti yake kwa kuwa kuna taratibu zinafanyika, tutamwekea pesa na kuhusu zawadi huyo alirithi taji, hakuwa mshindi wa kwanza, lazima mwelewe,” alisema Lundega.

Chanzo:Mwananchi

wasipopewa million 18 waachane na huo umiss na hajiuzulu.

tuone kama watampa wa 3

Dinazarde njoo uku movie inaendelea
 
Last edited by a moderator:
Hii kauli yalundenga ni dharau, binti aachie huo umiss eti anaambiwa amerithi? kwa hiyo hakustahili sio, bora aachie mapema maana akiboronga miss world lundenga atatupia lawama watanzania, kwa hiyo huyu ni mrithi tu, kapewa hisani hilo taji hakulifanyia kazi, du lundenga kweli umezeeka.
 
Arusha. Wazazi wa Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania iwape maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa hadi sasa wako njiapanda.

Kauli hiyo ya Eva na Deus Kamazima imekuja siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es Salaam.

Wakizungumza nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.

Walisema kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.

“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti.

Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika.

“Sijapewa taji wala zawadi , lakini kitendo cha kupewa kiti cha umalkia nimeridhika,” alisema Lilian.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema kuwa ni kweli bado hawajamkabidhi fedha na zawadi kwa kuwa kuna taratibu za kiofisi bado zinafanyika.

“Ni kweli, tulimwambia atuachie akaunti yake kwa kuwa kuna taratibu zinafanyika, tutamwekea pesa na kuhusu zawadi huyo alirithi taji, hakuwa mshindi wa kwanza, lazima mwelewe,” alisema Lundega.

Chanzo:Mwananchi

Hivi lundenga anataka siti aachie taji peke yake ila zawadi abaki nayo..!? hamna kitu kama hicho ukiachia unaachia kila kitu, na sio amerithi taji kama anavyosema huyo ndie alistahili kuwa miss tz siku ile mlimani city, na sio zawadi za miss tz peke yake na huko mwanzo alipotoka azirudishe...!!!
 
Hivi Lundenga huwa anatoa hayo majibu akiwa kalewa..katoka usingizi au ana kuwa kwenye hali gani...maana binafsi simuelewagi huyo anko Lunde
 
Tena afanye haraka kurudisha hizo zawadi
 
It should not come as a suprise for an organisation which is ran by a person who seem to come from lower intelect and with questionable moral ground like Lundenga. His capacity to handle issues which attract interest in public is now out because he has part ways with his partners. Need not to say that the partners where the brain and he(Lundenga) the face. I think it is the reason why he bleaches his face.
 
Hivi Lundenga huwa anatoa hayo majibu akiwa kalewa..katoka usingizi au ana kuwa kwenye hali gani...maana binafsi simuelewagi huyo anko Lunde

Lazima aseme vile kwani zawadi iliyokabidhiwa ni 10M, zile 8M alitia kibindoni kama fadhira ya kumpendelea Miss Kikongwe. Sasa kuzitema zile 8M ni issue, atazing'ang'ania liwalo na liwe hatazitoa.
 
Mmh!!!!! Kuna umuhimu hicho cheo kiwe kama mbio za vijiti....kupokezana la sivyo anko Lunde atafanya maajabu ya nane ya dunia kwenye cheo hicho
 
majibu ya lundenga yanatufanya tuanze kuamini maneno ya mitaani kuwa washindi huwa hawapewi zawadi kamili!
 
Back
Top Bottom