Nyanya mbichi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 3,716
- 2,220
Hasa waliojazia kama mama zao
sasa wamama wawe makini au wababa wawe makini kukemea huyu ibilisi asiwavae??
hapa baba anapaswa kulaumia japo hatuwezi kumuacha binti bila lawama. baba ni mzazi ambaye tunaexpect kwamba yeye ajenge misingi imara katika makuzi ya mtoto kama mzazi, sasa kama yeye anjiruhusu hata kumuingilia duuh hii ni abomination.
dah haya ni matokeo ya kutoheshimiana ndani ya nyumba upendo na kuleana leana kumezidi mno,watoto wa kike hawana haya mbele ya baba yako unavaa kimini kifupi na vikanga vya hovyohovyo ila all in all baba ndo mwenye kosa coz yeye ndo anapaswa amlee mtoto wake katika misingi ya kiafrika ilo mosi pili mtoto wa kike ukishapevuka na kujielewa lazima ujue jinsi ya kuishi na wazazi wako si muda wote unajipitisha na kuvaa mavazi ya ajabu
kwa upande wa binti ndo nnashindwa kuelewa sana ila mara nyingi inaweza ikachangiwa na ukaribu wa kupitiliza na mzazi wake wa kiume wataalamu wa kisaikolojia wanaiita 'Oedipus Complex' ni hali ya mtu(in ths case mtoto)kuvutiwa kimapenzi na mzazi wake, jina hilo linatokana na hadithi ya kufikirika 'myth' ya kigiriki ambapo Oedipus kijana wa kiume alimuua babaye kutokana na wivu aliokua nao kisha akamuoa mama yake, yes you heard me akamuoa mama yake. . .so naona bado chanzo kikuu cha incest kiko kisaikolojia zaidi.
Kila unalolisikia likihusisha wazazi kuzini na watoto wao lina story yake na sababu zake zilizopelekea.
Kuna wanaohusishwa na imani za kishirikina,kuna tamaa hasa kwa watoto wa kike,kuna laana tu ya kushindwa kuweka mipaka na kukubali kuwa kuna usivyostahili kuonja,kuna mila na desturi [nilishuhudia baba alitembea na bint zake wa3 kila bint alipochumbiwa mkewe akadai ndio mila zao],kuna ukaribu wa kupitiliza kati ya mzazi na mtoto hasa kwa single parent families na zile zilizotekwa na umagharibi.
Kwa sababu zozote zile hii ni kumkasirisha Muumba na kukaribisha mikosi na mabalaa kwenye familia.
Duh..na mama karidhika kabisaa! Watoto watatu..that is too much!!
Kuna mama alisema hana imani na mwanaume yeyote ikija kwa binti yake...nikamuuliza hata mumeo; akasema hata yeye ni mwanaume; Nikabaki na maswali...lakini leo naanza kupata majibu aiseee.
Lakini nikichukulia mfano wa baba yangu mi hiyo naona ni tabia ya mtu binafsi ...ni wale wenye ugonjwa...sisi baba alitulea kidhungu na hajawahi tembea na binti yake...ndio maana sikumwelewa huyu mama alokuwa anamuogopa mpaka mumewe...
Wengine wanakuwa woga kwa kuwa wameona kwa baba zao hivyo hawawezi ku risk....
Kwa nyakati tofauti pengine hata wewe mwana MMU umewahi kusikia juu ya jambo hili, au pengine limemtokea mmoja wa watu wako wa karibu.
Hili lina pande mbili
a) Ule wa hiari/makubaliano (voluntary). Japo injustifications zinaweza kuifanya aina hii kuchukua sura tofauti, mfano:
-hoja ya 'kurubuni'..japo haibadilishi ukweli kuwa ni kitu kilichofanyika kwa makubaliano.
-Ikiingia hoja ya umri hasa akiwa chini ya miaka 18 nayo pia inahafifisha swala la hiari au makubaliano.
b) Kubaka.
Hili wala halina maelezo mengi.
Baadhi ya mifano hai:
*Nimewahi kusoma shule moja na binti mmoja ambaye alikuwa anasimulia uhusiano wake wa kimapenzi na baba yake mzazi. Na akasema 'hakuna mwanaume yeyote anayeweza kunibabaisha'. Sikuweza kujua walianzaje maana kila ukimuuliza anakuuliza 'na wewe unataka nikupe'?
*Pia imekuwepo habari ya muda kidogo kuhusu mama aliyefunga ndoa na mwanae wa kumzaa huko Ruvuma.
*Kuna kipindi kimoja katika 'radio ya watu'..mama alikuwa anamshutumu baba anatembea na binti yao.
Swali:
Kwa nini mambo haya? Ina maana utu umeisha kiasi hiki? Ni tamaa za mabinti au wababa?
Ninaungana na wewe kumlaani baba kwa kuthubutu kimlala binti yake huu ni ushetani ulio ota sugu, sasa bi DEMBA kwanini tusiwalaani pia wanawake wanao funga ndoa na watoto zao walio wazaa? Juzi kati kuna mkasa ulitokea huko pwani baba mmoja kujiua kwa kunywa sumu baada ya kunfuma mkewe wa miaka 50 akipewa kichapo cha kitandani na mwanae wa kumzaa. Kwanini tusiwalaani nao?
Jamii nayo inahusika hasa kwenye ubakaji...
Mjomba wako wa mbali kidogo miaka miwili iliyopita alimbaka mwanae wa kumzaa....
Mkewe akaamua kuondoka na wanae watatu akarudi kwao...kila mtu eneo lile alijua lile tukio kuanzia ndugu majirani mpaka viongoz wa serikali ya mtaa hakuna hata mmoja aliyechukua hatua ya kuhakikisha huyu bwana anafikishwa kwenye vya sheria..
Tatizo siku hizi ule umoja na ushirikiano hakuna kila mtu kivyake ile dhana ya zamani mtoto wa mwenzio ni wako hakuna.
Ushirikina nao una mchango mkubwa sana katika hili.