Wazazi hawataki nioe Mchaga

Wazazi hawataki nioe Mchaga

Status
Not open for further replies.

CRISTA

Member
Joined
Aug 5, 2012
Posts
82
Reaction score
36
Habari,

Nina mchumba wangu ambaye nimepanga kwenda kujitambulisha kwao mwezi huu August lakini kwa sasa niko kwenye hali ngumu kwa kuwa wazee wangu wa huku Meru hawataki nioe Mchaga na wanasema ni bora ningeoa Mmeru kuliko Uchagani wakitoa sababu tofauti tofauti.

Mchumba wangu huyu ni mchanganyiko wa Mkibosho(mama) na Mmachame(baba) ingawa nilishakuwa na uhusiano na binti wa Kimeru na ndio wamekazia hapo?

Nifanyeje? Hivi ingawa ni tabia ya mtu binafsi lakini nani zaidi kati ya Mmeru na Mchaga?
 
wakati mwingine usipokuwa mkali na kuonyesha kuwa unataka unachotaka, kila mtu atakuyumbisha na hutakuwa na maamuzi binafsi. Hatuoi kabila miaka hii. Hata hivyo kabila lako na hao wachagga hamjapishana sana kitabia (kama ni ukorofi hata wameru ni wakorofi sana).
Simamia uamuzi wako na onyesha kuwa unamaanisha..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom