Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Kwanini UN na siyo Dodoma?
Iko wapi petition ya Wazanzibar iliyowakilishwa Dodoma, tukijua wana wabunge wao
Iko wapi petition iliyowasilishwa baraza la wawakilishi ikiwa ndani ya baraza ni wao peke yao

JokaKuu Mag3
Huko Dodoma swala la Sukari likeshindwa kupewa jibu lenye mashiko sembuse la Muungano
 
Suala la sukari ni rahisi tu

Waziri Mwijage yupo sahihi. Makonda hatoshelezi soko la znz, ya kuuza bara inatoka wapi?

Znz imetumia uchochoro wa kukwepa kodi au kodi rahisi kuingiza bidhaa za nje.
Halafu wanatumia uchochoro wa muungano kuingiza bara

Mathalani, mfanyabiashara wa bara akiingiza friji , TV au gari analipa kodi TRA kama sehemu ya mapato ya muungano ambayo znz inapata 4.5% na mzigo wa muungano

Mfanyabiashara wa ZNZ analipa kodi TRA znz, hazivuki bahari bali kutumiwa na SM
Bidhaa zinaingia bara kwa mgongo wa muungano bila kodi. Hapa kuna mambo mawili

Kwanza, mfanyabiashara wa Tanganyika atauza kwa bei ya juu kwasababu amelipa TRA
Mfanyabiashara wa znz atauza kwa bei ya chini, hakuna 'fair trade'

Pili, kupitia uchochoro wa znz, TRA itakosa mapato.
Mzigo ataubeba Mtanganyika kutoka vyanzo vingine ikiwemo mishahara au bidhaa.

Waziri Mwijage yupo sahihi, suala la sukari ni mwendelezo tu wa uchochoro wa siku nyingi

Miaka 3 au zaidi hapo nyuma wznz waliingiza makotena ya 'used' baiskeli kutoka nje
Kontena linalipiwa dola 150 znz na linalipiwa zaidi ya dola 2000 likishukia Bara
Baiskeli za znz zinaingia na kuuzwa Bara kwa kisingizio cha muungano

Kukawa na mwendelezo wa bidhaa nyingine kama sukari na maziwa
Leo ukiwaruhusu sukari, kesho wataleta nyama ingawa hawana ng'ombe, keshokutwa dawa za wanyama/ binadamu kwasababu zile zile.Utawazuiaje ikiwa umeshawafungulia mlango?

Solution ilikuwa ni TRA kukusanya kodi kwa ujumla, hapo kungekuwa na usawa kama ule wa mfanyabiashara wa mwanza kuingiza bidhaa kutoka Kenya au Uganda

Wazanzibar hawataki, wanachotaka ni kukusanya mapato yabaki kwao halafu mlango ufunguliwe kuingiza bidhaa sokoni bila kulipia kodi kwa muungano, wakimaliza wanautukana

Ikumbukwe, walitaka kuwa na biashara za nje binafsi wakisema bara inaweka kauzibe
Hii ilikuwa fursa nzuri kuuza maziwa au sukari nje bila kuingiliwa na muungano. Hawataki

Tunawaambia wznz siku ukiacha chochote cha muungano, soko la bara ni faida kwao.

Kadri wanavyoondoa na kupunguza mambo ya muungano wanajiumiza wenyewe
Tanganyika haitegemei znz kwa soko la bidhaa, ajira n.k.ni ukweli unaopingwa na punguani tu
 
Tanganyika ndiyo Tanzania kwa maana ya kwamba ndiyo imebeba muungano
Kama haipo huu muungano umebebwa na nani , na kama znz ipo inachangia nini?
Katika muungano znz inachangia 0, hata wabunge wanaokuja kwa ajili yao wanalipiwa na kodi za Watanganyika. Think about that!
Kiuchumi znz inachangia 0, hakuna unachoweza kuonyesha ni kipi mchango wake

Unazunguka zunguka lakini ukweli upo pale pale, hiyo Tanganyika ndiyo imebeba muungano kwa gharama na uendeshaji. ZNZ ipo katika muungano kwa jina tu, nzuri inapendeza
Si uoneshe hiyo tanganyika ipo wapi bajeti yake ipo wapi,bunge lake lipo wapi hatutaki ujanja ujanja
 
Suala la sukari ni rahisi tu

Waziri Mwijage yupo sahihi. Makonda hatoshelezi soko la znz, ya kuuza bara inatoka wapi?

Znz imetumia uchochoro wa kukwepa kodi au kodi rahisi kuingiza bidhaa za nje.
Halafu wanatumia uchochoro wa muungano kuingiza bara

Mathalani, mfanyabiashara wa bara akiingiza friji , TV au gari analipa kodi TRA kama sehemu ya mapato ya muungano ambayo znz inapata 4.5% na mzigo wa muungano

Mfanyabiashara wa ZNZ analipa kodi TRA znz, hazivuki bahari bali kutumiwa na SM
Bidhaa zinaingia bara kwa mgongo wa muungano bila kodi. Hapa kuna mambo mawili

Kwanza, mfanyabiashara wa Tanganyika atauza kwa bei ya juu kwasababu amelipa TRA
Mfanyabiashara wa znz atauza kwa bei ya chini, hakuna 'fair trade'

Pili, kupitia uchochoro wa znz, TRA itakosa mapato.
Mzigo ataubeba Mtanganyika kutoka vyanzo vingine ikiwemo mishahara au bidhaa.

Waziri Mwijage yupo sahihi, suala la sukari ni mwendelezo tu wa uchochoro wa siku nyingi

Miaka 3 au zaidi hapo nyuma wznz waliingiza makotena ya 'used' baiskeli kutoka nje
Kontena linalipiwa dola 150 znz na linalipiwa zaidi ya dola 2000 likishukia Bara
Baiskeli za znz zinaingia na kuuzwa Bara kwa kisingizio cha muungano

Kukawa na mwendelezo wa bidhaa nyingine kama sukari na maziwa
Leo ukiwaruhusu sukari, kesho wataleta nyama ingawa hawana ng'ombe, keshokutwa dawa za wanyama/ binadamu kwasababu zile zile.Utawazuiaje ikiwa umeshawafungulia mlango?

Solution ilikuwa ni TRA kukusanya kodi kwa ujumla, hapo kungekuwa na usawa kama ule wa mfanyabiashara wa mwanza kuingiza bidhaa kutoka Kenya au Uganda

Wazanzibar hawataki, wanachotaka ni kukusanya mapato yabaki kwao halafu mlango ufunguliwe kuingiza bidhaa sokoni bila kulipia kodi kwa muungano, wakimaliza wanautukana

Ikumbukwe, walitaka kuwa na biashara za nje binafsi wakisema bara inaweka kauzibe
Hii ilikuwa fursa nzuri kuuza maziwa au sukari nje bila kuingiliwa na muungano. Hawataki

Tunawaambia wznz siku ukiacha chochote cha muungano, soko la bara ni faida kwao.

Kadri wanavyoondoa na kupunguza mambo ya muungano wanajiumiza wenyewe
Tanganyika haitegemei znz kwa soko la bidhaa, ajira n.k.ni ukweli unaopingwa na punguani tu
Rejesheni tanganyika yenu sio kukaa na kuanza lawama,hii mbeleko ya muungano mnayo itegemea kuna siku mtakuja kulia machozi ya damu,muda utaongea.
 
Kwamba Znz yenye uchumi mdogo kuliko Mkoa mmoja wa bara inanyonywa na Tanganyika! Kwamba, kwa GDP na Bajeti ya znz mtu anakwenda kuiba nini? Bill ya umeme hawawezi, halafu wananyonywa! Fikiria mkazi wa Ilala au Muheza Tanga analipa bill ya Umeme kila mwezi, SMZ haiwezi! hadi isemwe tena ipewe miaka 2 ya kulipa
Hivi unaweza kukamua jiwe ukitaraji maziwa!

Hilo sio tatizo la Zanzibar Hilo ni tatizo la CCM. Kwanini CCM wanaendelea kulazimisha kutawala Zanzibar ikiwa tayari wameshindwa kuongoza?
 
Mkuu yawezekana nimeathirika na malezi ya CCM lakini nakuhakikishia siipendi CCM hata uniwekee bunduki kichwani
Nilivyofahamishwa kuhusu Karume na unavyoniambia ni vitu viwili tofauti.
Iwapo aliyafanya hayo ulioandika basi jamaa alikuwa mbabe
Nilivyoambiwa ni kwamba jamaa aliwakomesha waarabu na wangazija waliokuwa wakiwabagua wanzanzibari weusi

Kwani wangazija ni weupe? Tumekua tukiishi kwa mifumo ya kipropaganda sana kwenye hii nchi yetu.
 
Wangazija ni weusi lakini nilivyoambiwa ni kuwa walikuwa wakiwabagua sana waunguja wenzangu.
Sina uhakika kama ni kweli au ni porojo
 
Mzazi wangu mmoja ni wa Mrima na mwengine ni mpemba

Bila ya shaka mazingira ya unguja utakua unayafahamu japo kidogo.

Kuna Muarabu anaepata kazi ya Polisi Unguja? Jeshi? hata kazi za serkeali za kawaida vipi wananafasi yakupata kama wanavozipata watu wengine?
 
Mkuu mbona Jussa ni mjumbe wa baraza la wawakilishi?
 
hata wakiwabania waarabu kamwe hawatolala njaa na waarabu always wana hadhi ya juu kimaisha licha ya kubanwa kwenye kila aina ya fursa
 
Jussa ni muwakili wa CUF, na wa jimbo la mji mkongwe.
-Mji mkongwe zaidi asilimia 40, ya wakaazi ni Wahindi, wangazija, waarabubu au watu wenye asili ya kiarabu.
- Chama cha CUF moja ya sera yake kuu Zanzibar ni kuondoa ubaguzi. Kwaiyo kwa mazingira yake na kwa waumini wake wengi wanakua hawana imani za kibaguzi, au at least zinakua ni ndogo.Lakini je waweza amini Jussa anaweza kuwa mbunge wajimbo kama la Kwahani au Jang'ombe?

CCM umejijenga kwa mazingira ya kibaguzi. Wao ndio wabaguzi wakubwa lakini wanaishi kwa kujifanya kushutumu ubaguzi. Huwezi muamini mbaguzi wa wazi akulalmikie ati anabaguliwa.
 
hata wakiwabania waarabu kamwe hawatolala njaa na waarabu always wana hadhi ya juu kimaisha licha ya kubanwa kwenye kila aina ya fursa

Wanasumbuka sana. wanashindwa kufahamu kua MPEWA HAPOKENYEKI.
 
Back
Top Bottom