ha ha haaa jamani watu mna majibuu....
Ni kweli watu wana majibu.
Mimi nataka niwarudishe mbali zaidi.
Kwa wale walio na imani za dini wanaamini Mungu aliumba Adamu na Hawa na hawa wawili walitengeneza vizazi na kusambaa duniani. Je tunaelewa wapi Adam na Hawa waliishi na kufanya makazi yao hapa duniani?
Kwa hiyo basi ukiendana na historia hii, watu wote ni wageni katika maeneo(nchi) wanayoishi sasa hivi.
Hata wale wanaomini kuwa watu wametokana na mabadiliko (evolution) nao itawapasa wakubaliane na ukweli kuwa kila mtu leo ni mgeni hakuna mwenyeji. Samaki na manyani walitembea na kusambaa maeneo tofauti na ilipofikia kuwa watu ni wazi walikuwa wameshakata mbuga, misitu na nyika.
La msingi ni kukubaliana kuwa binadamu wana asili moja na katika dunia hii baada ya kukatiana mapande ya Ardhi na kuyaita Nchi, kuna wale waliowahi kufika eneo hilo na wengine kuhamia baadae. Uadilifu na haki ndio uongoze jamii/nchi zetu na sio kutafuta mizozo na migogoro ya kijinga.
kwa sasa ni rahisi kujua nani ni mzawa na nani ni mhamiaji. Kuna sheria za uhamiaji na uraia kwa hiyo katika hili watu watabishana na mwisho kujikuta wote ni wageni.
Mkapa ni Mtanzania lakini wazee wa wazee wake walitokea wapi?
Nyerere alikuwa Mtanganyika ambae amekufa akiwa ni Mtanzania lakini wazee wa wazee wake walitokea wapi?
Wazee wa Karume walizaliwa wapi? Karume alikuwa mzanzibari na baade alikuwa ni Mtanzania?
Ali hassan Mwinyi ni mzanzibari kulikoni kuwa mtanganyika? Kwa sasa ni mtanzania. Je Yeye ni mwenyeji wa wapi na mgeni wapi?
Karibuni linakuja Lijinchi kubwa linaitwa Afrika ya Mashariki na aliyekuwa mganda, mkenya, mtanzania, mzanzibari, mrwanda atakuwa na haki ya kumwita mwenzake mgeni au wa kuja katika nchi hiyo itayoitwa Afrika Mashariki wakti kila mmoja atakuwa na haki ya kwenda na kuishi katika eneo lote la Jamhuri ya/ au Shirikisho la Afrika Mashariki?
Hii mijadala yote ya karibuni ya uzawa, uzalendo,wageni, masultani, machotara na kuenzi mapinduzi ya mwafrika ni kwa sababu moja tu. Kutaka kuhalalisha ubakaji wa demokrasia huko Zanzibar. Wageni na wenyeji wa huko Zanzibar kwa umoja wao walipiga kura na kukipiga chini chama cha M. Ili watu waache kuzungumzia ubakaji wa demokrasia basi wanaanzisha mada na mijadala ya kuwasahaulisha watu uhuni wa chama hicho kinachobaka demokrasia.
Kama walioshinda wangepewa ushindi wao, wangetangazwa wameshinda huu upuuzi wote wa wageni, wakuja wala usingesikika. Pengine chamngamoto ingekuwa kufanya kile ambacho kimecheleshwa sana na CCM, kushughulikia Katiba mpya ya wananchi ili Tanzania ijioneshe kuwa ni Muungano wa nchi mbili ambao katika ubora wa Muundo wake ungeruhusu nchi zingine kujiunga pia.
Chronological History of Tanganyika (Tanzania)
A Modern History of Tanganyika
http://www.infoplease.com/encyclope...mous-archipelago-island-tanzania-history.html
HISTORY OF ZANZIBAR
TZIVA
RESEARCH PAPER ARAB INFLUENCE AND ITS IMPACT ON INDIAN AND EAST AFRICAN COASTLINES
Zanzibar People and Culture
Tanganyika | historical state, Tanzania