Wazanzibar waliotaka Muungano Uvunjwe Mbona Wako Kimya? Au kwa sasa ni mzuri?

Wazanzibar,

Sisi ndugu zenu watanganyika tunapenda muendelee na harakati za kuuvunja muungano yaani huu muungano mlikuwa mnasema ni koti limewabana mnaonaje sasa tuuvunjilie mbali muungano wenyewe?

Tunawaomba muendelee na harakati maana hata sisi tumeuona ni muungano mbaya sana haiwezekani watu milioni moja na laki tano tuungane na watu karibu milioni 58 hapana hii sio sawa uvunjwe kila mmoja aanze upya kabisa.
Mkuu wako wanaramba asali na kula Masega yake. Kamwe hutawasikia kwa sasa, ujue bara ni zuzuland na zenj ni janjaland
 
Zanzibar ni Tajiri kuliko Tanganyika
Umeulizwa kuhusu Pemba na Unguja wewe unaleta ya Tanganyika na Zanzibar! Na hata huko unasema uongo. GDP ya Tanzania ni USD 68 bilioni na ya Zanzibar ni USD 4 bilioni kwa hiyo Tanganyika GDP yake ni USD 64 bilioni ambayo ni mara 16 ya Zanzibar.

Amandla....
 
Uhalisia ndio muhimu
 
Zanzibari ni tajiri wakati mara kibao wanategemea mtanganyika aliye maskini amlipie mishahara na amsamehe madeni yake ya umeme!

Amandla...
 
Ipigwe kura ya maoni tuone wangapi wanaukubali au kuukataa muungano.

Mimi nitakuwa wa kwanza kuukataa muungano.
 
Back
Top Bottom