Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Mkoa maada una nzito sana. Wenzetu hawana msimamo kamili hupima upepo unaenda wapi.

Kwenye mafuta ni masuala yao. Rais wa JMT hana madaraka. Kwenye vurugu zao za uchaguzi wanakumbuka madaraka ya Rais wa JMT.

Inabidi wachague moja. Haiwezi kuwa sawa kwa hili ikawa hapana kwa lile wakati Rais wa JMT ni huyo huyo.
Sibonike,
Mambo si mepesi hivyo.
Bara wana majeshi ndani ya Zanzibar.

Wakitoa jeshi Zanzibar na kuwaacha Wazanzibari wamalize
matatizo yao wenyewe hutosikia lawama.

Wa kuchagua moja ni Bara.
Waingilie kuweka uwanja sawa au waondoe jeshi.
 
Mtoa mada huna hoja zaidi ya chuki zako tu kwa wazanzibar,adui wa wazanzibar tayari amekwisha fahamika,leteni majeshi na vifaru mtuuwe sote lakini huku zanzibar haturudi nyuma kudai haki ya maamuzi yetu ya tarehe 25-10-2015 iliyoporwa na mkoloni.
Mimi sina chuki na Wazanzibari na wala sina sababu ya kuwa na chuki nao.

Nimeishi na Wazanzibari, nimefanya kazi na Wazanzibari lakini sijawahi kushirikiana kwenye unafiki na undumila kuwili wao!

Kama hamtaweza kufahamu au kujifahamu mapungufu yenu, mtaendelea kutafuta mchawi nje ya nyumba yenu.

Mlipoamua kukaa ndani ya chumba na kutoka na maamuzi ya kubadilisha katiba, Watanzania Bara walikaa pembeni na kuangalia movie/mission yenu kwa sababu walifahamu hatima yake.

Kimetokea nini kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ambayo mlijitahidi kutuaminisha kuwa ni mwarobaini wa matatizo yenu?
 
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.

Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini katika mlengo wa kutaka kujitenga na Tanzania Bara. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la Wawakilishi na kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.

Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila kuwashirikisha wananchi wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya kubadilisha katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo kwa sasa inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki mkatuaminisha kinafiki kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea katika kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa sababu ina wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM. Mjumbe MMOJA aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na Mahakama Kuu na pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona inafaa.

Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: “Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba”.

Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa sasa limetoka na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa! Mmebaki kulaumiana kuhusu nani aliyelitoa jini kwenye chupa!

Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.

Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?

Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga kama mnavyofanya kwa sasa kwenye mazungumzo yenu ya siri ambayo Watanzania Bara hawafahamu na hamtaki wafahamu kinachoendelea.

Fasaha ya maneno unafiki na undumila kuwili, wazanzibari hawaaminiki ktk mambo Pinda aliwaambia Zanzibar siyo nchi wakamtukana matusi ya nguoni na kukaa haraka haraka kubadilisha katiba uchwara yao, masikini yule mama wa hela za mboga akaenda umoja wa mataifa kutaka watuongezee eneo la maji wakavuruga wakadai watadai wao kama nchi sijui iliishiaje.

Seif nae kwa unafiki wake kama alivyomfukuza mwenye chama mzee mapalala kamuweka kando Professor. Kila kukicha mabarua huku na huku kujikomba kwa wazungu na kwa Lowasa vikao wanakutana nyumbani kwake kiongozi gani huyu. Hongera #msemajiUkweli
 
Mkuu Msemaji wa Ukweli napenda nikupe hongera kwa hii `analysis`yako nzuri kuhusu Zanzibar! Inavyonesha ya kwamba kumbe Wazanzibari tayari wamevunja muungano wetu na wala hatuna sifa tena ya kuitwa JMT! Mimi nakubaliana nawe kabisa na unaonaje tukaanza kuwahukumu Wazanzibari kwa kuwaondoa wale majeshi yetu kule zenji, Uhamiaji, TRA, polisi na mambo yote yanayohusu Muungano kule Zanzibar! Hata vyama vya siasa tukagawana na kuwa CCM Zanzibar na CCM Tanganyika! Tufanye uchaguzi mwengine pia wa Tanganyika tumhalilishe Magufuli awe ni Rais wa Watanganyika! Tuwaachie wazanzibari wajiamulie mambo yao wenyewe bila ya kuwaingilia. Hayo si mawazo yangu bali ni mwendelezo wa hicho ulichokiandika hapo juu!
Suala la uwepo wa majeshi na watumishi mbali mbali Zanzibar ni hoja muflisi kimantiki.

Kuna watumishi na Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ) katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kwa nini hujawahi kujiuliza sababu ya wao kuwepo kwenye nchi ya nje na kama ulijiuliza, ulipata jibu gani?

Ni uamuzi wa Wazanzibari kusema rasmi kupitia vyombo vyao vya kisheria kuwa hawataki kuwaona watumishi na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi nchini mwao.

Kulalamika huku wakiwa ndani ya vyumba vyao vya siri ni kuendeleza unafiki na undumila kuwili ambao nimeujadili kwenye mada.

Hakuna anayewazuia Wazanzibari kujiamulia mambo yao ndio maana waliamua kubadilisha Katiba bila kushirikisha nchi ambazo wanaziita ''nchi za nje'' kama Tanzania Bara.
 
Mtoa mada huna hoja zaidi ya chuki zako tu kwa wazanzibar,adui wa wazanzibar tayari amekwisha fahamika,leteni majeshi na vifaru mtuuwe sote lakini huku zanzibar haturudi nyuma kudai haki ya maamuzi yetu ya tarehe 25-10-2015 iliyoporwa na mkoloni.
.....ni vizuri kama adui kajulikana...ila kujiua jiueni wenyewe...na hakutakuwa na cha kushangaza...labda ni jinsi mnavyochelewa..
 
Haya watoto wa Nkuruzinza kazini
Kama unatambua uwezo wako kifikra katika kujenga hoja nadhani usingefikiria hata kuweka comment yako.

Comment yako inaonyesha hajitambui kama huna uwezo katika masuala yanayohitaji fikra pana!

Jaribu kwenye jukwaa la Jokes and also Mahusiano, Mapenzi na Urafiki, Haya ni majukwaa ambayo ninaamini yatakufaa sana!

Ni ushauri tu!
 
Well said....JPM Anaanza anzaje?wakati mliweka solidarity kuwa ZEC ni tume 'huru'hakuna mtu kuingilia.Aaah mi naona mshalikoroga sasa hamna namna mlinywe tu.!!!
Waliweka jini kwenye chupa halafu wakalifungua, eti kwa sasa wanatafuta mtu wa kuwasaidia kulirudisha ndani ya chupa!
 
Kifupi Wazanzibar ni wanafiki na ndumilakuwili.
Inahitaji jicho la tatu kuliona hili. !
...ni watu wazuri,ila ikiingia siasa, wanageuka kuwa wanafiki wa kiwango cha barcelona kwe la liga!
 
Yes, wana Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Tume huru ya Uchaguzi!

Ukitaka kuwatawala, Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa itakusambaratisha!



Waliweka jini kwenye chupa halafu wakalifungua, eti kwa sasa wanatafuta mtu wa kuwasaidia kulirudisha ndani ya chupa!



Ukitaka kuwatawala, Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa itakusambaratisha![/QUOTE]


Mkuu pamoja na kutokwa na povu jingi mdomoni basi kuna jambo umesahau! Zanzibar pia wana Nkurunziza wao (Shein) ambapo yeye ni kama waziri huku kwetu! Huyu analipwa mshahara na serikali ya JMT! Sasa jee hii ni haki kweli au kwa vile yule huwa anavaa green ndio hatumsemi!
 
Watanganyika kwao niwasaliti na watu wasio faa. Ila wakiwa tanganyika wao ndio wenye thaman kununua mashamba na ardhi pasipo baguliwa. Kwa hakika nasubiri kuona dhambi yao inawatafuta hata siku ya mwisho.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Maalim Sefu mpeni ushindi wake hizo porojo za kisenge baadae.
 
Mkoa maada una nzito sana. Wenzetu hawana msimamo kamili hupima upepo unaenda wapi.

Kwenye mafuta ni masuala yao. Rais wa JMT hana madaraka. Kwenye vurugu zao za uchaguzi wanakumbuka madaraka ya Rais wa JMT.

Inabidi wachague moja. Haiwezi kuwa sawa kwa hili ikawa hapana kwa lile wakati Rais wa JMT ni huyo huyo.
Inashangaza sana!

Umoja wao wa Serikali ya Kitaifa ambayo ukichunguza kwa makini misingi yake ilikuwa ni kujitenga/kujiamulia mambo yao yote umegonga mwamba kwa sababu ya unafiki na ndumila kuwili.

Kwa sasa wamebaki kumtafuta mchawi nje ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa!
 
Hii mada ni mkakati wa kuhamisha fikra toka kwenye hali halisi. Huwezi kuutenga mfumo wa utawala wa JMT (au Tz bara) na mustakabali wa Z'bar. Ni chama kilekile (CCM) kinachotawala pande zote za muungano na siku zote maamuzi yake hutolewa kwa pamoja Dodoma. Sijawahi kusikia kutolewa kwa maamuzi tofauti kati ya "CCM Z'bar" na "CCM bara". Na CCM pamoja na serikali yake imeshaweka lengo na dhamira ya kuulinda muungano kwa gharama yoyote ile - kama wanavyoisemea "amani".

Hivyo kauli ya "mchawi wa waZanzibari ni waZanzibari wenyewe" ni zuga ya kisiasa. Kama kweli sisi wa bara hatutaki kuhusika na matatizo ya Z'bar, basi tujiweke kando tuwaache waamue mambo yao wenyewe. Tunapomsikia mwenyekiti wa CCM JK akidai "kuhuzunika" kuahirishwa kwa uchaguzi wa "Z'bar" wakati wao walijiandaa kusherehekea "ushindi" si rahisi kuiona mantiki ya mtu kuwanyooshea kidole waZanzibari kwamba mgogoro wao ni "wao pekee" - wasitusumbue. Ina maana CCM hawaoni hiyo mishkeli inayowahusisha wanachama wake wakishirikiana na CUF huko Z'bar? Wao wanajiandaa kusherehekea "ushindi" tu?
 
Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.

Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?

Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.

Ndio maana miye nimekaa kimya kuhusiana na Zanzibar.. baada ya kejeli, na matusi yote waliyowaita Watanganyika leo hii wote wanataka tuwaonee huruma tuingilie kati. Tanganyika imekuwa msaada kwa Wazanzibari kabla hata ya Uhuru, tukasaidia wakati wa Mapinduzi na hata baada ya Muungano lakini sasa imefika mahali na sisi tuanze kuwa fyatu tu kama wao. Na kuna siku ntawafyatukia kweli kweli. Haiwezekani miaka yote mambo ya Zanzibar wanatakiwa Wazanzibari tu ndio wayajadili lakin leo taifa zima tunaambiwa tuingilie kati! Badala ya kutaka Seif atangazwe mshindi waandamane na kudai kweli mamlaka kamili na wasimamie hilo ili vikosi vya JWTZ viondoke na watu wabara waende kule kama wageni wengine tu; tusihangaike na siasa zao...

Nimeanza kufyatuka.. Laawd have mercy!
 
Fasaha ya maneno unafiki na undumila kuwili, wazanzibari hawaaminiki ktk mambo Pinda aliwaambia Zanzibar siyo nchi wakamtukana matusi ya nguoni na kukaa haraka haraka kubadilisha katiba uchwara yao, masikini yule mama wa hela za mboga akaenda umoja wa mataifa kutaka watuongezee eneo la maji wakavuruga wakadai watadai wao kama nchi sijui iliishiaje.

Seif nae kwa unafiki wake kama alivyomfukuza mwenye chama mzee mapalala kamuweka kando Professor. Kila kukicha mabarua huku na huku kujikomba kwa wazungu na kwa Lowasa vikao wanakutana nyumbani kwake kiongozi gani huyu. Hongera #msemajiUkweli
Nyinyi ni wabafiki na mandumi.la kuwili .mamvo ya muungano yalikuwa saba tu wakati wa mzee karume sasa mmeyaengeza mpaka yako 22 .kengo lenu ni kuimeza zanzibar katika koti la muungano .hivi uliwahi kumuona membe wakati wake au huyu mahiga akirudi safari za nje na kutua moja kwa moja zanzibar na kueleza yaliojiri huko alikotuwakikisha? Wakieudi wanarudi dar tu .wakati mambo ya nje ni muungano .huo ni mfano mmoja tu
 
Back
Top Bottom