Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

HAPANA!!! Mchawi wa Wazanzibar ni Wazanzibar wenyewe!
Sir Good,
Fafanua tafadhali.
Suala la uwepo wa majeshi na watumishi mbali mbali Zanzibar ni hoja muflisi kimantiki.

Kuna watumishi na Jeshi la Wananchi waTanzania (JWTZ) katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kwa nini hujawahi kujiuliza sababu ya wao kuwepo kwenye nchi ya nje na kama ulijiuliza, ulipata jibu gani?

Ni uamuzi wa Wazanzibari kusema rasmi kupitia vyombo vyao vya kisheria kuwa hawataki kuwaona watumishi na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi nchini mwao.

Kulalamika huku wakiwa ndani ya vyumba vyao vya siri ni kuendeleza unafiki na undumila kuwili ambao nimeujadili kwenye mada.

Hakuna anayewazuia Wazanzibari kujiamulia mambo yao ndio maana waliamua kubadilisha Katiba bila kushirikisha nchi ambazo wanaziita ''nchi za nje'' kama Tanzania Bara.
Sir Good,
Mfano wa majeshi ya Tanzania kuwepo Congo ni tofauti
na kuwepo Zanzibar.

Kuchangia siasa za Zanzibar kunahitaji kuifahamu historia
ya Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi.

Ukianzia kwenye uchaguzi wa 2015 mengi utakuwa yamekupita.
 
Inashangaza sana!

Umoja wao wa Serikali ya Kitaifa ambayo ukichunguza kwa makini misingi yake ilikuwa ni kujitenga/kujiamulia mambo yao yote umegonga mwamba kwa sababu ya unafiki na ndumila kuwili.

Kwa sasa wamebaki kumtafuta mchawi nje ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa!
Kuna watu wanaiona Zanzibar ni kama Koni la Tanganyika, hawa kitendo chochote cha kuwaunganisha na kuwa wamoja wa Zanzibar hukiona kama ukorofi fulani, hawa hufurahi pale ambapo wanzazibari hawaelewani.
 
Ndio maana miye nimekaa kimya kuhusiana na Zanzibar.. baada ya kejeli, na matusi yote waliyowaita Watanganyika leo hii wote wanataka tuwaonee huruma tuingilie kati. Tanganyika imekuwa msaada kwa Wazanzibari kabla hata ya Uhuru, tukasaidia wakati wa Mapinduzi na hata baada ya Muungano lakini sasa imefika mahali na sisi tuanze kuwa fyatu tu kama wao. Na kuna siku ntawafyatukia kweli kweli. Haiwezekani miaka yote mambo ya Zanzibar wanatakiwa Wazanzibari tu ndio wayajadili lakin leo taifa zima tunaambiwa tuingilie kati! Badala ya kutaka Seif atangazwe mshindi waandamane na kudai kweli mamlaka kamili na wasimamie hilo ili vikosi vya JWTZ viondoke na watu wabara waende kule kama wageni wengine tu; tusihangaike na siasa zao...

Nimeanza kufyatuka.. Laawd have mercy!
Mwanakijiji,
Hili la ''huruma'' umelipata wapi.
Tafadhali nipe rejea na mimi nisome kwa kuwa silijui.

Hilo la kuingilia kati nalifahamu.
Maana yake ni hii...

Kuna jeshi kutoka Bara liko visiwani.
Hakuna anaetaka Tanganyika ihangaike na siasa za Zanzibar.
 
Haki walianza kutoitenda wao wenyewe kwa sababu waliamua kuwa wanafiki na ndumila kuwili.

Kinachotokea kwa sasa ni muendelezo tu wa yale waliyoyafanya kinafiki katika fikra za kibinafsi.
.....action and reactions are equal but opposite (Newton).
 
Nyinyi ni wabafiki na mandumi.la kuwili .mamvo ya muungano yalikuwa saba tu wakati wa mzee karume sasa mmeyaengeza mpaka yako 22 .kengo lenu ni kuimeza zanzibar katika koti la muungano .hivi uliwahi kumuona membe wakati wake au huyu mahiga akirudi safari za nje na kutua moja kwa moja zanzibar na kueleza yaliojiri huko alikotuwakikisha? Wakieudi wanarudi dar tu .wakati mambo ya nje ni muungano .huo ni mfano mmoja tu
Huyo Seif wako hujiulizi kwa nini kila jambo anaenda nyumbani kwa Lowasa? na kuandika mabarua kwa wazungu, kwa nini? Kila anaookutana na vyombo vya habari anakuja Dar na siyo Zanzibar kwani huko hakuna mahotel makubwa kama Serena?
Fikiri Mara 2 kama hujui uliza wahenga watakuambia kijana.
 
Mimi ni lizani sefu anakuja kwako kukukera kumbe abakwenda kwa lowasa ukawa mwenzake .mbona lowasa hajalalamika kwamba sefu anamsumbua .kuhusu barua mbona tunakusikiacwewe tu mbona hatujasikia hayo mambo ya barua .taja sheria zinazokataza mtu kwenda kwa mtu na sheria zinazokataza mtu kuandika barua .mbona shirika la posta halijafungwa.? Yaani wewe unaelimu ndogo kuliko woto duniani .wewe na madenge bora madengecanajua kuliko ww
 
Inashangaza sana!

Umoja wao wa Serikali ya Kitaifa ambayo ukichunguza kwa makini misingi yake ilikuwa ni kujitenga/kujiamulia mambo yao yote umegonga mwamba kwa sababu ya unafiki na ndumila kuwili.

Kwa sasa wamebaki kumtafuta mchawi nje ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa!
MsemajiUkweli,
Kuna msemo wa Kiingereza: ''Barking the wrong tree.''
Msisitizo unauelekeza sipo.

Tatizo si SUK.

Tatizo ni kuwa CCM Zanzibar wameshindwa uchaguzi sasa
hawakubali kushindwa.

Msimamo wao ni kuwa wao wamepindua serikali kwa hiyo
hawako tayari kutoa serikali kwa njia ya kura.

Hapa ndipo lilipo tatizo.

La unataka historia ya chaguzi za Zanzibar toka 1995 fanya
utafiti wako mwenyewe utapata majibu.

Hawajapatapo kushinda uchaguzi hata mmoja.

Ila ukiwaambia hilo huwa hawakubali na kama hukubali ukweli ni
kuwa hufanyi juhudi za kujirekebisha.

''Wake up'' call ilikuwa ile ''referendum'' Wazanzibari 66.7 walipopiga
kura kutaka SUK.

Ile ilikuwa tosha kuwaeleza CCM kuwa wapi mwelekeo wa wananchi
kuanzia pale ulikuwa unaelekea.

Bahati mbaya hawakutanabahi hata pale waliposhindwa katika uchaguzi
wa 2010.

Wamekuja kuamka kutoka usingizi mzito kwenye uchaguzi wa 2015.

Taharuki iliyowakumba imehifadhiwa katika video mtandaoni ikiwa
hujaiona itafute.
 
Mimi ni lizani sefu anakuja kwako kukukera kumbe abakwenda kwa lowasa ukawa mwenzake .mbona lowasa hajalalamika kwamba sefu anamsumbua .kuhusu barua mbona tunakusikiacwewe tu mbona hatujasikia hayo mambo ya barua .taja sheria zinazokataza mtu kwenda kwa mtu na sheria zinazokataza mtu kuandika barua .mbona shirika la posta halijafungwa.? Yaani wewe unaelimu ndogo kuliko woto duniani .wewe na madenge bora madengecanajua kuliko ww
Angalia mpangilio wako wa maneno na hoja nini unajadili
 
Huyo Seif wako hujiulizi kwa nini kila jambo anaenda nyumbani kwa Lowasa? na kuandika mabarua kwa wazungu, kwa nini? Kila anaookutana na vyombo vya habari anakuja Dar na siyo Zanzibar kwani huko hakuna mahotel makubwa kama Serena?
Fikiri Mara 2 kama hujui uliza wahenga watakuambia kijana.
Una umri gaani ww dogo? Jaribu kichangia mada zinazoendana na umri wako na elimu yako, vinginevyo utakuwa kitukko hapa. Umelewa?
 
Mwanakijiji,
Hili la ''huruma'' umelipata wapi.
Tafadhali nipe rejea na mimi nisome kwa kuwa silijui.

Hilo la kuingilia kati nalifahamu.
Maana yake ni hii...

Kuna jeshi kutoka Bara liko visiwani.
Hakuna anaetaka Tanganyika ihangaike na siasa za Zanzibar.
Hamna kitu kama jeshi la bara. JWTZ lina wazenji pia.
 
Uzi mtamu, lakini umekosa wachangiaji wenye hoja zenye mashiko. Ndugu zangu Wanzanzibar wamelikoroga wenyewe!
Kirikou Wa Kwanza,
Nachukulia kuwa ''kukoroga'' una maana wamevuruga.
Tafadhali eleza wapi Wazanzibari wameharibu.
 
Kifupi Wazanzibar ni wanafiki na ndumilakuwili.
Inahitaji jicho la tatu kuliona hili. !
Leo hii wanatuambia matatizo yao ni yetu lakini wakati wanaandika Katiba yao waliamua kuziba masikio huku wakidai, tuache kuwafarakanisha kwa sababu kwa sasa ni wamoja. Maslahi ya Zanzibar ni zaidi ya vyama vyao.

What happened?
 
Natamani Zanzibar ingemezwa tu. Siasa ingekuwa rahisi sio mara Ukawa ghafla CUF hata muda wa maendeleo unapotea.
 
Hamna kitu kama jeshi la bara. JWTZ lina wazenji pia.
Wile,
Huwa halifanyiki hivyo duniani kote.

Soma historia ya mapambano katika wenyewe kwa wenyewe
utaona ndugu hapalekwi kupambana na ndugu.

Wajerumani walipongia Tanganyika 1800s wakati wanapambana na
Abushiri bin Salim AlHarith wa Pangani na Chifu Mkwawa wa
Kalenga jeshi lililotumika na Wajerumani kuapambana na wazalendo
hawa halikutoka Tanganyika.

Von Wissman alichukua Wanubi kutoka Sudan na Wazulu kutoka
Msumbiji.

Iko mifano mingi hata ya wakati Waingereza walipokuwa wanatawala
Tanganyika.
 
Leo hii wanatuambia matatizo yao ni yetu lakini wakati wanaandika Katiba yao waliamua kuziba masikio huku wakidai, tuache kuwafarakanisha kwa sababu kwa sasa ni wamoja. Maslahi ya Zanzibar ni zaidi ya vyama vyao.

What happened?
MsemajiUkweli,
Kuna jeshi Zanzibar kutoka Bara.

This is what is happening.
 
Sijui strategy yao lakini nachojua kikatiba JWTZ lina wazenji kwahiyo sio jeshi la bara.
 
Kwa kutaa kurudia uchaguzi ndio mnawaita ndumila kuwili? Tatizo la Zanzibar sio uchaguzi, tatizo la zanzibar ni kuuitenga,
Una maana gani unaposema tatizo ni kuuitenga?

Boresha sentensi yako. Please!
 
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.

......
Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: “Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba”.

Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
......

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.
Mtoa mada mimi nimevutiwa na hiyo niliyoiweka rangi ya mapenzi(mahaba).

Hoja imetolewa kuwa sio TUME. Sio ZEC iliyofuta uchaguzi na matokeo yake. Link Msaada: Nini kitatokea iwapo CUF hawatashiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar? Ni Jecha pekee kutokana na mashinikizo ya CCM ndio alitenda batili na anaendelea kuikanyaga Katiba huku akilindwa(akiwa chini ya ulinzi) unaoratibiwa na CCM. Kwa hiyo Jecha ametenda kitu ambacho hakimo ndani ya mamlaka yake. Nisisitize tu, kutokana na hoja iliyotolewa na wanasheria ni kuwa hata kama Tume ndio ingesema inafuta uchaguzi basi bado ingekuwa batili kwa sababu Tume haina mamlaka ya kufuta uchaguzi uliokamilika. Tume(msimamizi wa kituo au jimbo) inaweza kuahirisha tu uchaguzi kama kuna dharura.
Hili ni vizuri kuliweka wazi katika mada yako ili wasomaji waelewe kuwa Katiba inataka aliyepewa dhamana aseme na atende vitu,mambo kwa mujibu wa Katiba na sio kuivunja. Alichofanya Jecha ni kuvunja Katiba.

Mimi sioni kwa nini unawaita Wazanzibari ndumilakuwili kwa kuikataa CCM kwa wingi wao. Ningekuelewa kama ungesema CCM ni ndumilakuwili kwa kutotoa tamko lolote la kutaka Jecha afikishwe Mahakamani kwa kukiuka katiba.

Mwenendo mzima wa vitendo anavyovifanya Jecha unajionesha kuwa anashurutishwa kutenda na kusema na wale wenye kushika hatamu za nguvu za dola. Nani wanaongoza serikali za Tanzania?

Uchaguzi wa 2015 hauna tofauti na chaguzi zilizopita ambazo CCM walipora ushindi wa CUF. Wewe unafikiri ni kwa nini mtu kama Balozi Amina anataka SUK ivunjwe?

Zipo kauli za viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanganyika(Muungano) mfano Balozi Mahiga, Jaji Lubuva, wanaosema Zanzibar ni nchi yenye katiba yake na utamaduni wake na mifumo yake, Je hoja ya kutaka Wazanzibar wawashirikishe Watanganyika katika kuandika katiba ya Zanzibar inatoka wapi?
Mimi nilitegemea ungeibuka na hoja ya kushajihisha watanganyika ili tudai Katiba ya Tanganyika pia.

Ingawaje umeandika kwa ufundi mkubwa mada hii lakini umeonesha kuuficha umafia wa CCM wa kubaka demokrasia huko Zanzibar. Bila ya mbeleko ya JWTZ na Polisi Dr. Shein asingeweza kuwa na kiburi cha kung'ang'ania madaraka.

Na kila mpenda haki, anaelewa kinachoendelea Zanzibar ni ubakaji wa demokrasia ulioratibiwa na unaosimamiwa na CCM. Wazanzibari walishafanya maamuzi kupitia kisanduku cha kura na waliikataa CCM kuongoza serikali.

Jeshi, JWTZ na Polisi ilitumika kubaka demokrasia Zanzibar. Nani ametuma vikosi hivi? Huyo ndiye ndumilakuwili. Ndumilakuwili huyu ndie anazuia demokrasia ya Tanzania kusonga mbele. Ndumila kuwili huyu ndiye anapigisha kura kwa fax, anachakachua Rasimu ya katiba, Anakataa Tanzania kuwa na Tume huru za uchguzi, Anakataa matokeo ya Urais hata kama yatatangazwa kwa kuvunja masharti ya Katiba hakuna mtu anaweza kukimbilia mahakamani kutafuta haki.
Je ndumilakuwili ni nani?

Link Jecha alitumwa na nani kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar
 
Aisee cwez laumu kinachoendelea wacha watafunane TU,coz nikikumbuka kipindi hicho NA sakata LA kudai bendera yao ilikuwa kasheshe pinda aliposema Zanzibar siyo nchi
 
Leo hii wanatuambia matatizo yao ni yetu lakini wakati wanaandika Katiba yao waliamua kuziba masikio huku wakidai, tuache kuwafarakanisha kwa sababu kwa sasa ni wamoja. Maslahi ya Zanzibar ni zaidi ya vyama vyao.

What happened?
MsemajiUkweli,
Kuna jeshi Zanzibar kutoka Bara.

This is what is happening.

Mzee Mohamed ni bora ukaachana na huyo Msemaji Uongo! Yeye umagufuli umemjaa kiasi ambacho anabana matumizi hata ya kutumia akili yake!
 
Back
Top Bottom