Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Wazanzibar acheni unafiki na ndumilakuwili

Ni sawa kwa tabia ya kwetu kuita pikipiki zote Honda

Might is not right
 
Sheikh mbona Zanzibar wana majeshi yao pia huku bara? Askari polisi pia wafanyikazi wa forodha warudishwe kwao Zanzibar
Lancashire,
Zanzibar haina jeshi ukiacha KMKM na sasa Zombie ambao wanachukuliwa
kama ''Polisi Shirikishi.''
 
Unafiki na undumila kuwili kwa sasa umewaumbua. Mlificha magonjwa kwa unafiki na sasa kifo cha serikali ya umoja wa kitaifa kinawaumbua.

Mlimtumia Abubakar Khamis Bakary Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni kuwasilisha hoja binafsi kulitaka Baraza la Wawakilishi kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu kuanzishwa kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lakini katika mlengo wa kutaka kujitenga na Tanzania Bara. Hoja hiyo, ilikubaliwa na Baraza la Wawakilishi na kupelekea kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni Nam 6, 2010.

Mliamua kujifungia kwenye vyumba vya siri bila kuwashirikisha wananchi wa Tanzania Bara na mkafikia makubaliano ya kinafiki ya kubadilisha katiba yenu kwenye Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ambayo kwa sasa inasema, Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

Mbaya zaidi, kwa kupitia katiba yenu ya kinafiki mkatuaminisha kinafiki kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa ni huru na inayojitegemea katika kutekeleza majukumu yake kupitia Kifungu cha 119 (13) kwa sababu ina wajumbe WANNE waliopendekezwa na vyama vya CUF na CCM. Mjumbe MMOJA aliyependekezwa na Rais. Jaji MMOJA aliyependekezwa na Mahakama Kuu na pia Mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais kwa kadri anavyoona inafaa.

Mkasema wazi katika kifungu cha 119(13) kuwa: “Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba”.

Hamkuishia hapo, mkatuambia kupitia Kifungu cha 119(4), kuwa pindi Mjumbe wa Tume anapoteuliwa, hakuna mtu/kiongozi mwenye mamlaka ya kumuondoa au kumfukuza Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi mpaka atakapotimiza miaka mitano tokea kuteuliwa kama Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi mkaifanya kama Jini ndani ya chupa, kwa sasa limetoka na hamuwezi kulirudisha ndani ya chupa! Mmebaki kulaumiana kuhusu nani aliyelitoa jini kwenye chupa!

Mkatuambia mmechoka kufanyiwa maamuzi na watu wa Tanganyika na kuanzia sasa vyenu ni vyenu wakati wa raha lakini wakati wa shinda, vyenu ni vyetu. Tuliwaambia haiwezekani vyenu viwe ni vyenu pekee wakati wa raha lakini wakati wa shida, vyenu viwe vyetu.

Mkasema Watanzania Bara wanachochea mtengane lakini kwa sasa mmeamua kushikamana. Tuliwaambia hiyo ndoa yenu haitadumu lakini mkabisha. Yamefika wapi?

Unafiki na undumila kuwili kwa sasa unawatafuna!

Maji mliyavulia nguo mkiwa mmejifungia ndani ya chumba cha siri, hamna budi vile vile kuyaoga.

Hapo kwenye bold inathibitisha kabisa kuwa kila wazanzibari wanapokuja katika mustakbali wa kushikamana nyinyi mnajitahidi kuwavunjia umoja na mshikamano wao hi ni fitna na chuki kubwa kutoka kwenu na ndio msingi wa majanga yatakayo warudi wenyewe na kuwakumba sio muda mrefu.

Might is not right
 
Hii Makala ya Mohamed Said nayo ni RUBBISH pia!!!
Ngida1,
Hapana haja ya kutoa matusi.
Ungeweza ukasema hayo ulosema kwa lugha ya kistaarabu.

Huu ni mjadala tu.
Hakuna sababu ya mtu kughadhibika na kutukana watu.
 
Sio visiwani tu hata huku bara wanafiki wapo wengine tu kwa jina lingine ni makajanja na bahati nzuri tuliwashitukia mapema tukahamua kuwakata
 
MsemajiUkweli,
Kuvunja muungano tutakuwa sisi kama Waafrika tunajihujumu wenyewe.
Dunia ya leo ni mataifa kuja kuwa pamoja.

Angalia Wazanzibari wanavyoneemeka hapa Bara.

Hili ni jambo zuri sana na naamini hakuna katika Wazanzibari atafurahi
kutenganishwa na Tanganyika.
Nimechoka na unafiki na pia undumila kuwili wa viongozi wa Zanzibar na hasa CCM na CUF.
 
"Hatukumuomba Rais Magufuli aingilie kati mgogoro wa Zanzibar. Ni yeye mwenyewe ndiye aliyesema alipolizindua Bunge kwamba atautatua mgogoro wa Zanzibar. Ajabu leo anayaruka maneno yake mwenyewe."

- Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

Might is not right
 
"Hatukumuomba Rais Magufuli aingilie kati mgogoro wa Zanzibar. Ni yeye mwenyewe ndiye aliyesema alipolizindua Bunge kwamba atautatua mgogoro wa Zanzibar. Ajabu leo anayaruka maneno yake mwenyewe."

- Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

Might is not right
1455453612121.jpg


Might is not right
 
HIVI Dhumuni La Kuweka Huu UZI Hapa!!!? KWANI Mleta UZI Haujui Kuwa Ni KWELI VIONGOZI Kutoka BARA Ndio Chanzo Cha Mitifuano Kule Visiwani!!!!?? WW Kwa Fikra Zako CCM ZANZIBAR Wanaweza Kuamua Au Kufanya Maamuzi Yoyote Bila Ya CCM Bara Na Taifa Kuridhia!!?? JUU Ya KATIBA Yao Kuifanyia Marekebisho Hiyo Ni Haki Yao Kikatiba, Kwani Zanzibar Ni Nchi, Na Hawakukubali Kuufuta Uzanzibar Na Utaifa Wao!! Hivyo Kufanya Marekebisho Yao Ya Kuunda Serikali Ya Umoja Wa Kitaifa, Si Lazima Ww Wa BARA KUTOA MAONI YAKO!! Wazanzibar Wenyewe NDIO WALIOTAKIWA Kutoa MAONI Yao, Kama WANAKUBALI Au WANAKATAA!! PIA Suala La TUME Huru Ya UCHAGUZI, Ni Suala Zuri La Kulipongeza, Kwani Kwa Muundo Wa Tume Hiyo Ndio Ule Mchezo Mchafu Uliyokuwa Ukidaiwa Kufanyika Na Upande Fulani Umeshindwa Kufanyika 2015!! MATOKEO Yake Wamemtumia Jecha Kufuta MATOKEO Yaliokamilika!!! HIVYO Hilo Kwao Ni Suala Muhimu Na La Kupongezwa!! HUKU BARA Mbona Tumeshindwa Kupata, TUME Walau Hiyo Unayoiponda!!!! SIDHANI Kama Ni UNAFIKI Na UNDUMILAKUWILI!! Bali Ni Moja Ya Hatua Nzuri Ya Kujenga Umoja Wao!! TATIZO Ni WABARA, Ndio Wanaoivuruga Zanzibar, Na Wenyewe Wameshalijua Hilo!!!!
Ungewataja hao wabara ingependeza ili umma uwafahamu.
 
Ni hivi matatizo ya zanzibar yalitoka tanganyika ,,yanatoka tanganyika na yataendelea kutoka tanganyika .subiri hichi ni kichwa cha kitabu kitatoka karibuni mkuu ukikisoma utaelewa vizuri mkuu
Nasubiri hicho kitabu kwa hamu
 
jeshi ya tz nchi congo au nyingine yamepitishwa kuenda kufanya kaz na UNO au AU , sasa majeshi ya TZ bara yamepitishwa na nani ? kwenda kule zenz ?

Yamepitishwa na kitengo na ni kitengo hicho hicho kilichoamua heri ya lawama ktk uchaguzi mkuu uliopita 25/10/2015
 
Back
Top Bottom