Wawindaji.. True story

Wawindaji.. True story

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,710
Reaction score
20,706
Wawindaji wawili na wauzaji maarufu wa ngozi za chui mkoani arusha walikubaliana kwenda porini kuwinda. Kufika kule, wakafikia kwenye kibanda chao walichokijenga maalum kwa kujihifadhi kipindi wakiwa huko porini.
Kesho yake asubuhi, Nanyaro alichukua bunduki na kumwambia mwenzie abaki kibandani wakati yeye akienda kuwinda.
Akiwa porini, ghafla Nanyaro anamuona chui na kumpiga risasi lakini bahati mbaya risasi inamkosa!
Kwa hasira chui yule akaanza kutimua mbio kuelekea alipo Nanyaro. Nanyaro kuona vile, akatupa bunduki na kuanza kukimbilia kwenye kile kibanda huku akimpigia mwenzie kelele " Aiseee fungua mlango..! Fungua mlango Nakufaaa..!
Bahati mbaya Nanyaro alipokaribia kwenye mlango wa kibanda akajikwaa na kuanguka. Wakati huo huo, yule chui nae akawa tayari ameruka juu ili amdake Nanyaro!
Kutokana na spidi kali ya yule chui, Nanyaro alipoanguka chui akapitiliza mlangoni na kuingia hadi ndani! Nanyaro kuona vile, akainuka haraka na kuufunga mlango kwa nje, kisha akamwambia mwenzie aliyeko ndani : " Aisee Mbise, chui wa kwanza huyo nimemleta. We anza kumchuna mi ngoja nikatafute mwingine"!
 
mh! alafu umekomalia ni ya kweli, we kakuadisia nani ama wewe ndo mwindaji2?
All in all nimecheka pekeyangu kama kichaa. Ninapo soma story huwa nina predict end of story kabla cjamaliza, lakini hii chaka mpaka mwisho.
 
Nanyaro nimtu katilisana sana wala hana huruma bora angeufungua mlango labda jamaa angepata upenyo akakimbia.
 
dah! wewe ni mkali..nimekukubali. gud one man.
Wawindaji wawili na wauzaji maarufu wa ngozi za chui mkoani arusha walikubaliana kwenda porini kuwinda. Kufika kule, wakafikia kwenye kibanda chao walichokijenga maalum kwa kujihifadhi kipindi wakiwa huko porini.
Kesho yake asubuhi, Nanyaro alichukua bunduki na kumwambia mwenzie abaki kibandani wakati yeye akienda kuwinda.
Akiwa porini, ghafla Nanyaro anamuona chui na kumpiga risasi lakini bahati mbaya risasi inamkosa!
Kwa hasira chui yule akaanza kutimua mbio kuelekea alipo Nanyaro. Nanyaro kuona vile, akatupa bunduki na kuanza kukimbilia kwenye kile kibanda huku akimpigia mwenzie kelele " Aiseee fungua mlango..! Fungua mlango Nakufaaa..!
Bahati mbaya Nanyaro alipokaribia kwenye mlango wa kibanda akajikwaa na kuanguka. Wakati huo huo, yule chui nae akawa tayari ameruka juu ili amdake Nanyaro!
Kutokana na spidi kali ya yule chui, Nanyaro alipoanguka chui akapitiliza mlangoni na kuingia hadi ndani! Nanyaro kuona vile, akainuka haraka na kuufunga mlango kwa nje, kisha akamwambia mwenzie aliyeko ndani : " Aisee Mbise, chui wa kwanza huyo nimemleta. We anza kumchuna mi ngoja nikatafute mwingine"!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom