Waweza kuzuia kichefchef? Soma hii!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,257
Waamerika wawili,Peter Murphy na John Cogan walikuwa wanafanya kazi ya kujitolea mkoani Iringa katika idara ya misitu.Walipewa nyumba moja ya kuishi wote wawili, na baada ya muda wakaamua wamwajiri mtu wa kuwasaidia kazi za pale nyumbani hasa katika upande wa jikoni .Wakampata baba mmoja, Hasani Malipula aliyekuwa na ujuzi wa mapishi ya magharibi.
Waamerika hawa hawakupenda tabia ya Hasani ya kuvuta sigara, lakini wakamvumilia.Hasani alikuwa anavuta sigara aina ya
Nyota
Bwana Murphy alikuwa mtu wa dhihaka na mizaha mingi sana, na mwenzake Bw Cogan alimwunga mkono kwenye mizaha na dhihakanyingii walizomfanyia mfanyakazi wao. Wakati fulani walinatisha malapa ya Malipula kwenye sakafu na Malipula aliposhindwa kutembea baada ya kuvaa malapa, waamerika hawa walicheka sana. Siku nyingine walimvizia Malipula akiwa amelala kwenye kiti kwa uchovu mwingi wakamfungia kwenye hicho kiti. Alipoamka,Salaleh! Hawezi kuinuka. Waamerika ni vicheko tu.Mizaha ikaendelea kwa muda.
Siku moja jioni, wakati wapo mezani wanakula, Cogan akahisi harufu ya tumbaku kwenye chakula na kumwuliza mwenzake juu ya jambo hili.Mwenzake akajibu kwamba hahisi chochote.
Jioni moja, wakamsikia Malipula jikoni akikohoa na kuvuta makohozi mazito. "Shauri ya masigara yake huyo" , alidakiaMurphy. Tunatakiwa tumfundishe kanuni za afya" aliongeza Cogan. "Pamoja na hayo,"alisema Murphy akikuna kichwa,"tuache kumfanyia mizaha, tunamfadhaisha kimawazo." "Hasa!" aliunga mkono Cogan. "Hicho ni kitu nlitaka kukuambia siku nyingi sana" Wakakubaliana kesho yake wamweleze Malipula juu ya uamuzi wao wa kuachana na mizaha.
Asubuhi yake wakamwita Malipula mazungumzo yakawa hivi:
Murphy: Malipula, tumekuita kukuarifu kwamba kuanzia leo hatutakufanyia kitendo chochote kama tuluvyokua tunakufanyia
Malipula: Yaani hamtanatisha malapa yangu sakafuni wala kunifunga kwenye kiti tena?
Murphy na Cogan: Kamwe, hatutakufanyia tena mambo kama hayo.
Malipula: (Kwa sauti ya chini lakini iliyosikika vizuri)Basi kama ni hivyo, na mimi sitatemea tena makohozi kwenye chakula chenu!


 
waamerika inabidi wamfukuze kazi bila malipo na waende hospitali kwa uchunguzi zaidi!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom