barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Watu watatu waliokuwa wamekwama katika kisiwa cha Pacific kwa muda wa siku tatu waliokolewa salama siku ya Alhamisi baada ya kutumia matawi ya mitende kuandika neno “saidia” kama ishara katika mchanga, ambapo Ndege la jeshi la wanamaji liliwaona wakipunga koti za kuokoa zao kando ya ishara hilo, Mlinzi wa pwani wa Marekani alisema.
Walinzi wa pwani walisema mashua watu hao walikuwa nayo iliangushwa na wimbi mkubwa, lakini wote walikuwa wamevaa koti za kuoka na wakaweza kuogelea karibia maili mbili (karibu kilomita 3.2) ili kifika katika kisiwa.