Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,744
- 2,611
Baadhi ya wananchi wamevamia eneo la bonde la Buyuni Kata ya Buyuni wilayani Ilala- Dar es Salaam na kupima viwanja kinyume na utaratibu.
Eneo hilo lipo ndani ya Mradi wa Viwanja 20,000 Buyuni. Ni bonde linalotenganisha mtaa wa Serikali Buyuni na Kigezi na ni bonde ambalo lipo nyuma ya Zahanati Buyuni na nyuma ya madarasa ya Shule ya Msingi Buyuni.
Eneo hilo limetengwa kwa ajili ya kulinda mazingira baada ya kupima viwanja vya Serikali kwa kuwa ni la bondeni na hupitisha maji wakati wa mvua.
Mdau anayeishi eneo hilo amesema kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa likinyemelewa na watu wenye uchu na fedha na kuanza kuuza viwanja, jambo ambalo ni uharibifu wa mazingira.
Soma pia: Vitendo viovu vimekuwa kero Mtaa wa Nyeburu, Kata ya Buyuni - Chanika (Wilaya ya Ilala)