Wauzaji wa mbao Buguruni: Janga la taifa

Wauzaji wa mbao Buguruni: Janga la taifa

Verily Verily

Senior Member
Joined
Jan 4, 2007
Posts
192
Reaction score
148
Buguruni ni sehemu maarufu kwa vifaa vya ujenzi hasa mbao na sementi.

Ila nimeona nitoe tahadhari kwa mtu yeyote anaefikiria kwenda kununua mbao sehemu ile.

Wauzaji wa pale ni wezi kuanzia futi kamba (tape measure),mahesabu na bei zao na treatment ya mbao zenyewe.

Kwa mfano duka moja wana tape measure inayoanzia na FT 6 mark ikimaanisha kuwa kila ubao wanaiba ft 5. Ukija na tape measure yako wanakuwa wakali na wanpandisha bei hapo hapo.

Taarifa ni kuwa wamewaliza watu wengi sana.

Tafadhali sana jihadhari na wezi hawa.
 
ndugu pale ni wezi tangu zamani, ulipaswa uwe na fundi hodari na mzoefu wa maeneo yale, na pia uhakikishe uwe na tape yako, wakati wao wanapima kisha nawe unapima, iliyopungua wanakubadilishia.
ukilegea imekula kwako....!
 
pale wamejaa madalali na matapeli tu!ukienda nenda na tape yako maana utalizwa vibaya sana
 
Hilo nafikiri ni janga la Buguruni na si la Taifa kwa sababu sie wengine tupo mikoani !!
 
Kwani mbao hizo ni lazima kununua hapo tu...
 
Buguruni ni sehemu maarufu kwa vifaa vya ujenzi hasa mbao na sementi.

Ila nimeona nitoe tahadhari kwa mtu yeyote anaefikiria kwenda kununua mbao sehemu ile.

Wauzaji wa pale ni wezi kuanzia futi kamba (tape measure),mahesabu na bei zao na treatment ya mbao zenyewe.

Kwa mfano duka moja wana tape measure inayoanzia na FT 6 mark ikimaanisha kuwa kila ubao wanaiba ft 5. Ukija na tape measure yako wanakuwa wakali na wanpandisha bei hapo hapo.

Taarifa ni kuwa wamewaliza watu wengi sana.

Tafadhali sana jihadhari na wezi hawa.

ahsante kwa taarifa mkuu,hata wauza makapet wa pale karibu na shule ya sekondari benjamin mkapa wana tabia hiyo,wamechakachua tape measure zao,halafu zimechakaaa,namba hazionekani vizuri
 
Kwa mfano duka moja wana tape measure inayoanzia na FT 6 mark ikimaanisha kuwa kila ubao wanaiba ft 5.
Kama tape measure inaanzia kwenye alama ya futi sita inamaanisha kila ubao unaibiwa futi sita, sio tano! Isije ikawa wewe ndio hujui hesabu ndo maana unaibiwa ibiwa.

Ukija na tape measure yako wanakuwa wakali na wanpandisha bei hapo hapo.
Kama unajua kabisa kwamba ukija na tape measure yako bei inabadilishwa then tunachofanya ni kupatana bei KABLA ya kutoa tape measure yako.

Isije ikawa wewe ndio mgeni hapa Buguruni usiyeelewa biashara ya kuogelea na papa bila kumezwa.
 
Back
Top Bottom