Wizi wa Wauza mbao wa Buguruni

njex

Member
Jun 10, 2017
67
52
Jamani mnaotaka kujenga kuweni macho sana na wauza mbao zile treated tunazonunua kwa futi hasa hasa pale buguruni.Leo nilienda kununua mbao pale baada ya kupata vijisenti kdg ktk hali hii ngumu nikatengeneze kibanda changu ambacho kimekaa muda bila kupauliwa.Nimekaribishwa kwa sura zenye bashasha na ushawishi ukizingatia niliwahi mapema na kuwa mteja wa kwanza na usawa huu wa Magu!
Fundi wangu alinitaadharisha mapema kuwa tuwe macho sana.
1.Tape measure wanazotumia ni magumashi.hivyo na sisi tuliibeba ya kwetu.Tukaawaambia tuikague tape measure.Ilionekana haina shida.Walipoanza kupima ndo mchezo ukaanza.Mbao ya kwanza ikawa ok.Zilipoongezeka kufika tano ubao wa ft 18 au 19 unatoa ft 22 hadi 24.Tukasitisha zoezi tukatoa tape yetu.Walipokataa tukatia mkwara wa kuondoka.wakawa wapole.tukahakiki na tape yetu kila ubao ulizidi ft 2 hadi 4.
Zoezi zima likaanza upya.mimi na fundi wangu kwa kutumia tape yetu ndo tukasimamia show nzima mpk mzigo wa mbao zote ulipokamilika.
2. calculator.
Mbao zote zilikuwa 80.zilikuwa na urefu tofauti kuanzia ft 15.5 hadi 22.5.nyingi zilikuwa kati ya ft 18 na 20.Akanipa nimsomee namba halafu anajumlisha kwenye calculator.Mwishoni akanipa nihakiki kama amjumlisha sahihi.Jibu lililotoka ni kubwa huwezi kuamini.nilipopiga hesabu za haraka nilijikuta natakiwa kulipa 1.2m ziada ya ile ambayo mm na fundi tuliitarajia.Lkn tukajiuliza imekuwaje? Ukipiga hesabu za haraka kwa kutumia average haifiki hela hiyo
Uamuzi:Tukasema hatuna imani na calculator yao.Wote mm na fundi tukatoa simu zetu tukaanza kujumlisha upya.Jamaa wakaja juu kuwa tunawapoteza muda wa kuhudumia wateja wengine.Na ss tukasema basi biashara hakuna na hatulipi.Ilibidi wawe wapole.Tukapiga hesabu na kweli jibu letu likawa dogo sana.Tulipozidisha kwa gharama ya futi moja fedha tuliyotakiwa kulipa ilikuwa 1.4m less ya ile waliyokokotoa wao.
Kwa hiyo kuweni makini sana ndg zangu mnaotarajia kujenga na kununua mbao buguruni na huenda wauzaji wengine wa mbao wanafanya mtindo huo
 
Kweli mkuu maana nshapigwa hapaa
 
Wezi sana wakikukosa kukupiga kwenye tape measure zao za magumashi au kula dili na fundi uliyefuatana nae basi watakupiga kwenye mahesabu
 
Back
Top Bottom