Wauza magazeti siku zao kulala na njaa zimekaribia

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,318
2,000
Kutokana na kukua kwa teknolojia na watu kutaka kupata habari kwa haraka sana. Magazeti yameonekana yapo nyuma ya wakati.

Hebu piga hesabu habari iliyoandikwa kwenye gazeti leo, mimi niliisoma jana kwenye mtandao au nilisilikiza kwenye televisheni. Hapo mtu ataangaika kununua gazeti la nini.

Na watu vilevile watu wamechoka kutembea na makaratasi miaka yote.
Kama jinsi mnavyojua kitu chochote kinavyokua basi ujue kingine kinakufa.

Wauza magazeti wamejitahi kutumia vichwa vya habari vyenye maneno makali halafu unakuta kilichoandikwa ndani ni tofauti na hii imechangia kwa kiasi kikubwa watu kupunguza imani kwa magazeti.

Na kwa hili wauza magazeti siwezi kuwalaumu labda sometime ni njaa inakuwa inawauma. Ila nawashauri kuandika habari za uongo na zenye maelezo marefu. Ili mtu kumshawishi mtu anunue gazeti, hilo sio jibu lake.

Cha msingi someni nyakati na namuangalie ni namna gani nyingine mtakavyoweza kufanya kazi ya habari ili kuendana na wakati.
 

Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
552
1,000
Unawaongelea Wauza magazeti au Waandishi(Wazalishaji) wa magazeti. Muuaji nafikir hana kosa anaweza badil biashar ila Waandishi ndo wataisoma namba
 

mareeTZ

Senior Member
Jun 4, 2015
171
250
katika vitu vinawaharibia biashara ni hizi radio kuyachambua magazeti asubuhi. zinaingiza mamilioni kwa uchambuzi huku zikimaliza wateja coz mtu akishaskiza asomi tena. pia kuna baadhi ya account kwenye social media hupost magazet hii pia haipo sawa. mtu anaanza kutamani kununua gazet anapofika kubandani lakini unakuta ameshasoma vichwa vyote vya habari hats haendi tena kwenye banda la magazeti.
 

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,355
2,000
Ingekuwa hivo ingeanza huko duniani ambako tekenelojia ndiko ilikoanzia.
Labda tu kama hufuatilii swala la tasnia ya habari, huko duniani unaposema magazeti mengi yamepunguza wafanyakazi na mengi sasa yanapata kipato kwa kutumia online publication, mwaka 2016 printing versions yalikumbwa na recession ya 9%, USA magazeti zaidi ya zaidi 160 tangu 2008 yameacha kutoa printing version ya magazeti
The U.S. Has Lost More Than 166 Print Newspapers Since 2008
Jamaa wa magazeti ya the sun yy ameamua kukomaa wala hakupunguza wafanyakazi hakuna sehemu magazeti yana wakati mgumu kama huko duniani. Hata TZ ni swala la muda tu.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
173,757
2,000
Usiponunua wewe wengine watanunua. Watu wengi wana miliki smartphone ila hawazitumii kusomea magazeti mtandaon wala habari.
 

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,254
2,000
Si yupo na tayari amekiri yule bosi wa yale magazeti pendwa na SHILAWADU kuwa hali kiuchumi imeshuka...!!? Kaisoma namba.....maana yeye bila kuchochea BIFU za wasanii....bila kumuandika Diamond na Kiba au bila kumsakama WEMA kwake hauzi kabisa GAZETI...!!
 

Snipes

JF-Expert Member
Jul 2, 2013
8,574
2,000
katika vitu vinawaharibia biashara ni hizi radio kuyachambua magazeti asubuhi. zinaingiza mamilioni kwa uchambuzi huku zikimaliza wateja coz mtu akishaskiza asomi tena. pia kuna baadhi ya account kwenye social media hupost magazet hii pia haipo sawa. mtu anaanza kutamani kununua gazet anapofika kubandani lakini unakuta ameshasoma vichwa vyote vya habari hats haendi tena kwenye banda la magazeti.
Hii sidhani kama ni sababu kwa sababu wao wenyewe wana pages za magazeti yao na wanaweka hvy vichwa vya habari, binafsi naona ni njia ya kupata wateja kwa kutumia hzo headlines
 

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,355
2,000
Hii sidhani kama ni sababu kwa sababu wao wenyewe wana pages za magazeti yao na wanaweka hvy vichwa vya habari, binafsi naona ni njia ya kupata wateja kwa kutumia hzo headlines
Hapana hii ni sababu moja wapo unakuta kuna redio inasoma habari nzima na wanachambua ukurasa karibu zote.
 

Third Eye

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
364
250
Nakubaliana na mtoa mada, hata nchi zilizoendelea hiyo imekuwa challenge kubwa. Kwa hapa nchini pia taratibu tunahamia kwenye dijitali. Mfano kuna application flan inaitwa mpaper unaweza kuiona hapa, ni ya Vodacom nadhani. Unasoma gazeti lote toka mwanzo hadi mwisho kwenye computer au simu na wanauza kwa nusu ya bei ya gazeti. Mfano gazeti linauzwa 800 wao wanauza 400. Nadhani ni moja ya njia za kukabiliana na hali hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom