USHUHUDA: Kuna Waganga na Waganga njaa, huyu ni Kiboko

Apr 17, 2022
97
131
Habari wana jf! Leo hii nami naomba nitoe shuhuda na vimbwanga nilivyo vikuta kwa mganga baada ya kuona hapa wanajamii f. Wanatoa shuhuda zao mbalimbali.

Nianze kwa kusema waganga wa kweli wapo na matapeli wapo tena matapeli ndo wengi zaidi.

Ilikuwa mwaka 2018 mwezi wa sita kutokana na hali ngumu ya maisha iliyo sababiswa na aliye kuwa mke wangu niliamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mkoani Tabora.
Nilifika huko Kwa kuelekezwa na mwenyeji wangu maana nilikuwa na rafiki yangu akiishi huko.

Tulifika kwa mganga jioni ya saa kumi na mbili na kwa bahati tukamkuta Yule fundi. Sikutaka ramli Bali nikimueleza shida yangu iliyo nipeleka pale, mganga akanambia pamoja na kukataa ramli ila yeye binafsi lazima anichunguze, aiseee! Alinambia mengi ya sirini hata ambayo sikumsimulia akafanya nimuamini zaidi na zaidi maana kuna vitu alivizungumza nikabaki naguna tuu.

Niwe muwazi kidogo, nilienda Kwa ajili ya kulipa kisasi kwa aliye kuwa mke wangu mambo yalikuwa mawili tuu afe au atoweke kabisaaa nisimuone machoni mwangu (maana aliolewa mazingira yaleyale niliyo kuwa nikiishi) aende kokote kule na nisikutane nae.

Jambo jingine lililonipeleka pale ni kutaka kuoshwa dawa niwe msafi nikubalike na jamii maana nilikuwa kama nina mkosi mambo yalikuwa hayaendi kabisaaa pesa niliijutia sana kwakweli.

Basi bwana mganga akaanza yake ila alinishauri kuwa kinacho sababisha mambo yangu ya yumbe na hata aliyekuwa mke wangu kunifanyia yote Yale ni sababu ya mitambiko (MIZIMU) hivyo iliamua kuniadhibu kupitia familia yangu na kunifungia ridhiki yangu.

Kutokana na hilo mganga akanishauri niachane na visasi ni focus kwanza na hiki chanzo cha matatizo, nilimuelewa lkn nikamwambia yeye atengeneze maswala hayo ya mizimu ila kisasi lazima maana niliumizwa Sana na huyo dada.

Mganga alinipatia tiba kwelikweli zilichinjwa kuku za kutosha, nilioga Dawa za kutosha kwa kweli mengi alinifanyia, tumetembea Sana maporini, tumekutana na nyoka wa kila aina na maajabu mengi sana na hatimae mganga aliniaga

Mganga aliniaga kwa staili ya kipekee siku hiyo zilipgwa ngoma juu mlimani wakatokea nyoka wawili wakubwa kiasi ,mganga alitamka maneno ambayo niliyaelewa vizuri Sana, alisema hivi, NINYI WAKUBWA WA PORI, WAHENGA NA WAHENGUZI MPENI BARAKA KIJANA HUYU HUKO AENDAKO AKAFANIKIWE, AJENGE MAJUMBA, AFUGE, ALIME, AFUNGUA MADUKA MAKUBWA, ANUNUE MAGARI n.k SIKU AKIRUDI KWANGU AJE NA ZAWADI.

Wakati anazungumza maneno hayo alikuwa ameangalia magharibi huku akiwa ameshika mikono yangu kuielekeza juu, na alipo maliza ulipita upepo mkali mbele yetu, akanambia kazi imeisha, nitafanikiwa.

Ikumbukwe nilienda kwake kwa ajili ya visasi na maisha ila kipaumbele changu ilikuwa ni kumkomesha Yule Dada kwa hiyo yeye alichukua la maisha na akanambia nikiwa na maisha mazuri wala huyo Dada siwezi kumkumbuka tena.

Nyie acheni waganga wapo na kwa sasa hali niliyo nayo sio ileee tofauti kabisaa na kwa kweli yule malaya simkumbuki japo huwa natamani nimgonge na gari, labda tuu niseme maneno ya fundi ya mwisho kabisa tukiwa kilingeni ni ,ATAKUJA MTU ATAKUPATIA FEDHA LAKI TANO NA HIYO NDIYO UTAKAYOANZIA BIASHARA, aah nisieleze sana ila baada ya mwaka alitokea mshikaji ila tulizoeana tuu kidogo akanipatia mtaji wa laki tano na nusu kiukweli, popote ulipo fundi kula tano na nitaendelea kukukumbuka Sana

Pesa hizi zina njia nyingi msione watu hawashuki kuna namna katika maisha, maisha ni sayansi kubwa Sana na yana Formula nyingi,

Ipo siku nitaeleza kisa cha huyo Malaya aliye niletea maumivu makali japo saivi anasugua tuu life gumu Kama nini upande wake saivi anaonekana mzee mweee wanawake hawaa pia nitakuja kueleza mambo mengine ya mitambiko ambapo alinigusia kuwa pamoja na biashara zangu kuwa safi ila ipo siku nitafanya kazi kama yake. WAGANGA WA KWELI WAPO NA WAGANGA NJAA WAPO,

POPOTE ULIPO MWANA WA UGOTA mungu akujalie maisha marefu.

KWA WALE WAJUAJI WA KILA JAMBO AMBAO WATASEMA HILI LABDA NI TANGAZO BASI SITOI NAMBA YA SIMU, THOUGH KUNA UZI HUMU NILITOA NAMBA YAKE.

TAFADHALI USIJE DM NA KAMA NILISHA WAHI KUKUPATIA NAMBA DM BASI ULIBAHATIKA TUU. TUKUTANE KAZINI. KAZI IENDELEE.
 
Umeisha tayari, umepewa fake hope, subiri maumivu yake.
Maumivu gani mkuu, Nina muda sasa hakuna cha maumivu wala nini,, nilisha ukataa umasikini na siutaki kila mtu na njia yake ya mafanikio, wengine kwa mwamposa, wengine kanisani, wengine kwa waganga na wengine yaani kwa kifupi kila mtu kachagua namna yake ya kuishi buda
 
Hakika MUNGU ni wahuruma Sana kwasababu yeye huwanyeshea mvua Kwa wema na wabaya hata Kwa nyie mnayopitia Kwa waganga bado yeye MUNGU ndiye mtoaji wa hizo baraka.

Kumbuka wengi wanaenda Huko Kwa waganga na hawafanikiwi.... MUNGU bado anakupenda anatamani kukuona unageuka na kuacha njia zako mbaya
 
TAFADHALI USIJE DM NA KAMA NILISHA WAHI KUKUPATIA NAMBA DM BASI ULIBAHATIKA TUU. TUKUTANE KAZINI. KAZI IENDELEE.
Kawaida ya binadamu kusema no na huku kumbe moyoni anaomba ama anajua kuwa ukweli Ni yes so huwezi kuongoza akili zetu namna ya kuwaza.kuna haja gani kumtaja.

Hebu tuambie jina lako na uonyeshe hapa hata kadi za magari ambayo hayapungui matano,pia uonyeshe listi za malipo shule za maana za wanao wanaposoma ,pia uonyeshe hapa screenshot ya bank balance.

Pia uonyeshe miamala ya maana ya biashara unayokuwa unaifanya. Tuone hata unalipa wazo hill cement unalipa kitu like unanunua sementi semi Kama 50 Kama sio njaa Kama zangu unakuja kupigia promo uganga.

Cha kushangaza huo ukoo wa mganga wako ni masikini ujue
 
Kawaida ya binadamu kusema no na huku kumbe moyoni anaomba ama anajua kuwa ukweli Ni yes so huwezi kuongoza akili zetu namna ya kuwaza.kuna haja gani kumtaja. Hebu tuambie jina lako na uonyeshe hapa hata kadi za magari ambayo hayapungui matano,pia uonyeshe listi za malipo shule za maana za wanao wanaposoma ,pia uonyeshe hapa screenshot ya bank balance ,pia uonyeshe miamala ya maana ya biashara unayokuwa unaifanya. Tuone hata unalipa wazo hill cement unalipa kitu like unanunua sementi semi Kama 50 Kama sio njaa Kama zangu unakuja kupigia promo uganga.


Cha kushangaza huo ukoo wa mganga wako Ni masikini ujue
Nikupe tuu pole na sihitaji kukupinga, kama nilikuwa sina uwezo wa kununua gari, kujenga nyumba, kula nacho kitaka Leo hii navipata kwa nini nisiheshimu na kuamini kuwa mganga katenda afu usilolijua ni kuwa mganga anaweza kuwa masikini ila akatoa Dawa ya maana na mtu akatoboa kimaisha, Tulia hivyohivyo mkuu kila mtu na njia zake za maisha
 
Tatizo ndo hili la WaTz Mimi sijipigii Promo nimezungumzia uhalisia na nilicho kutana nacho na kukiona, anyway pambana kwa njia zako mkuu
Waliopewa dawa wakatoboa huwa hawasemagi wanakuambia kuwa kazi kwa bidii labda wawaambie marafiki ama rafiki mmoja tu usitake kudanganya.

Na ndio Mana huwezi tuma hapa nilivyokuambia. Yaani uko kwa Hali ya kutangaza biashara. Hebu lete statement ya benki ya akaunti yako ili tukuamini
 
Waliopewa dawa wakatoboa huwa hawasemagi wanakuambia kuwa kazi kwa bidii labda wawaambie marafiki ama rafiki mmoja tu usitake kudanganya.

Na ndio Mana huwezi tuma hapa nilivyokuambia. Yaani uko kwa Hali ya kutangaza biashara. Hebu lete statement ya benki ya akaunti yako ili tukuamini
Aya nimekubali ni tangazo! Amini unacho kiamini
 
Back
Top Bottom