Elimu muhimu kwa mashabiki na wapenda wa mpira

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,318
12,622
Mpira ni ajira na burudani kama burudani nyingine. Mpira ni ajira kwa kuwa Kuna watu wanapata pesa kutokana na mpira kama mishahara ya moja kwa moja na wengine hupata pesa kwa kuwauzia bidhaa (jezi, vuvuzela, maji, pombe, juice, vyakula, tiketi, usafirishaji wa wanaoenda na kutoka kwenye mpira, nk) wapenda mpira, na wengine kutangaza bidhaa zao kupitia timu za mpira, wengine ni walinzi, wafanya usafi, watunza viwanja kwenye viwanja. Hapa lazima kila mpenda mpira ajitahidi kupata pesa kupitia mpira kwa njia mbali mbali badala ya kuwa shabiki TU,

Mpira ni burudani kama burudani nyingine kama kunywa pombe, music, ngono, na uraibu mwingine.. hivyo hakikisha kuwa wewe kijana
1. Unapata fedha kutokana na mpira, uza vifaa vya mpira au vitu vingine hata kama ni karanga kwa wapenda mpira. Kumbuka akina Azam media, GSM, mo, sp, m-bet, wachambuzi wa mpira, wakata tiketi, wauza jezi, wamiliki wa mitandao kama you tube, Instagram, mpenja, Millard, nk wote hao wanapata pesa ya mpira kasoro wewe TU mjinga.

2.Hakikisha kuwa unatumia asilimia ndogo sana (0.005%) kwenye starehe ya mpira ili usije kujuta uzeeni kwa pesa uliyotumia kwenye uraibu wa mpira.
3. Kama unapenda sana mpira punguza aina nyingine za uraibu ili kupunguza gharama za starehe.
4. Fikiria kuwa na nyumba na vitega uchumi kwaajili ya siku za uzeeni.
5. Mpira na starehe zako ziwe nyuma ya Vipaumbele vingine kama vile ada ya watoto, kuwa na nyumba, kuwa na ardhi/shamba vkuhudumia familia, finali ni uzeeni.
6. Kama Timu zikiuza hisa kwa wanachama nunua hisa ili upate faida kama timu itatengeneza faida.

Usijesema sikukuambia kuhusu hili, pale kwetu alikuwapo mtu fulani alikuwa dereva wa kiwanda Cha mbolea TFC, alikuwa shabiki wa kutuowa wa coastal union na Simba, alikuwa hakosi kwenda kuangalia mechi za hizi timu popote pale hata kwa kutoroka kazini, kusingizia ugonjwa au likizo bila malipo, alikuwa ananunua jezz za timu zake zote na Ile ya lMan U aliyokuwa anaishabikia, kila siku ilikuwa ni lazima anunue rundo la magazeti ili asome habari za michezo ya ndani na nje. Kipindi Cha mizecho TBC zamani RTD saa 1.45 usiku lazima aache kazi zote asikilize kipindi Cha michezo kwanza. Yeye alikuwa dereva TU pale kazini lakini alitumia sehemu ya kipato chake kwa kusafiri kwenda kwenye mechi, viingilio, jezi na magezeti, Alipostaafu kipato kilipungua sana hivyo hakuwa na fedha tena ya kugharamia aina Ile ya starehe, hakujenga nyumba, Wala kuwa na kitegauchumi chochote na hata watoto hakuwapa kipaumbele sana kwenye matunzo Wala vocational training. Mzee yule alijutia pesa na muda wake alioupoteza kwenye starehe Ile. Hakuchukua muda akaugua Sonona na kuiaga dunia baada ya kumaliza kuuza vifaa na nguo zake.
Usione hawa wazee akina Akilimali, Kilomoni na wengine wanang'ang'ana na Yanga na Simba hata uzeeni kiasi Cha kuficha hata hati za majengo, ukweli ni kwamba walipoteza Mali zao nyingi sana kweñye hizi timu, wanajutia ndio maana hawataki mabadiliko ya kuwaingiza viongozi wengine na utaratibu mwingine unaowafungia wao nje. Mwina alidai chapati zake alizowanunulia wachezaji wakati huoo. Hawa wanaojiita wazee wa Yanga na Simba ni sehemu ya watu hao waliopoteza pesa zao nyingi kiboyaboya wakati huo, wanajutia muda, fedha, nguvu na rasilimali zao nyingine walizotumia kwenye ushabiki wa mpira.

Fanyeni kwa kiasi (responsibility). Kuna lofa anaweka reheni hata mkewe, nyumba yake kwaajili ya mpira!!¡
 
Kabla hujaweka pesa yoyote kwenye mpira na starehe ingine jiulize kwanza kama kibatali chako kina mafuta ya kutosha: ada ya mtoto umelipa? pocket money ya mtoto umempa? mzazi wako amekula? Uzeeni hutakuwa mzingo kwa wengine? Kuna mtu anaitumikia timu kwa nguvu zake zote ujanani lakini uzeeni anataka huruma za watu na timu zimtafutie matibabu, malazi na chakula, hiyo sio sawa, shabikia timu yako responsibly.

Mpira huu ni lazima ukupe fedha pia hata kama wewe sio mchezaji Wala kiongozi wa timu. Fanya biahara yoyote Ile yenye uhusiano na mpira.
 
Kula Ulaya Mifumo Yao matunzo uzeeni inafanya kazi kwelikweli, Huku kwetu sio, Kuna vikokotoo vya kiwiziwizi uzeeni.
 
Elimu hii ya mpira kwa wadau wote wa mpira usiipuuze tafadhali. Baada ya mpira kuna maisha mengine. Ona hapa, ajali imetokea kwa bahati mbaya kwenye mpira, lakini wanafamilia wanatafuta msaada wa kifedha kutoka timu ya Yanga kana kwamba Yanga ndio imemuua shabiki.

 
Back
Top Bottom