Wauza mafuta waigomea EWURA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]MONDAY, 29 AUGUST 2011 19:27 NEWSROOM

tatus%20kaguo.jpg

NA WAANDISHI WETU GAZETI LA UHURU

BAADHI ya wafanyabiashara wamekaidi agizo la Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa kuendelea kuuza petroli na dizeli kwa bei ya zamani, badala ya elekezi iliyotolewa juzi. Bei mpya ilianza kutumika jana, ambapo petroli imeshuka kwa asilimia 2.11, dizeli asilimia 1.57 na mafuta ya taa kwa asilimia 1.28. Kutokana na punguzo hilo, mkoani Dar es Salaam, petroli inauzwa sh. 2,070, dizeli sh. 1,999 na mafuta ya taa sh. 1,980 kwa lita. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na Uhuru mjini Dar es Salaam, umebaini vituo vya kampuni ya TOTAL vimeendelea kuuza nishati hiyo kwa bei ya zamani.

EWURA katika toleo la wiki mbili zilizopita, kabla ya kutangaza bei mpya elekezi juzi, petroli ilipanda kwa sh. 100.34 (asilimia 5.51), dizeli sh. 120.47 (asilimia 6.30) na mafuta ya taa sh. 100.87 (asilimia 5.30).

Katika toleo hilo, petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa sh. 2,114, dizeli sh. 2,231 na mafuta ya taa sh. 2,005 kwa lita.

Vituo vya TOTAL vilivyopo Manispaa ya Kinondoni, maeneo ya Morocco, Shekilango na Mlimani City, mabango ya matangazo yalionyesha bei ya zamani ya sh. 2,114 kwa petroli na dizeli sh. 2,231.

Walipoulizwa wahudumu katika vituo hivyo, kwa masharti ya kutotajwa majina gazetini walisema wataendelea kuuza kwa bei hizo mpaka watakapopata maelekezo kutoka kwa maofisa wa kampuni hiyo.

Hali katika vituo vya Oryx, Oil Com, Camel Oil, TSN, Victoria na GAPCO ilikuwa tofauti, kwani mabango kwenye vituo yalionyesha bei mpya elekezi na wahudumu walikuwa wakiuza nishati hiyo.

Akitangaza bei hizo mjini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu, alisema kushuka kwa bei kunatokana na kushuka katika soko la dunia. Hata hivyo, alisema bei zingeweza kushuka zaidi kama shilingi ya Tanzania ingeimarika ikilinganishwa na dola ya Marekani.

Aliwaonya wafanyabiashara watakaokaidi bei hizo kuwa watachukuliwa hatua za kisheria. Adhabu kwa kituo kinachokiuka bei elekezi ni faini ya sh. milioni tatu papo hapo na sh. milioni moja kwa kila siku mpaka atakapotii bei elekezi.

Masebu hakupatikana jana kuzungumzia hatua zitakazochukuliwa dhidi ya TOTAL.

Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo, alisema hawajapata taarifa lakini wanafuatilia kwa kina, endapo watabaini hilo, sheria itachukua mkondo wake.

ÒKwa kawaida huwa hatufanyi operesheni mara moja baada ya kutangaza bei elekezi, hata mimi nimepita kwenye kituo kimoja asubuhi nikakuta bei hazijabadilishwa nilipohoji walisema wanasubiri maelekezo,Ó alisema.

Takriban mwezi mmoja uliopita, EWURA iliposhusha bei, wafanyabiashara waligoma na kusababisha adha kuwa nchini.

Kampuni za Engen, Oil Com na Camel Oil zilipewa onyo kutokana na mgomo huo, huku BP ambayo imefungiwa kufanya biashara imefikishwa mahakamani.

LAST UPDATED ( MONDAY, 29 AUGUST 2011 19:54 )
 
Hivi jamani watanzania tuwe na akili wakati mwingine, hivi wewe umenue bidhaa kwa shs 100, faida yako ni shs10, pamoja na vat utauza kwa shs 128, sasa unapotanzzaza akupunguza bei hata shs 5, yuo mfanyabiashara hasara nani atamfidia?
 
haya ni matunda ya ukiritimba waliouanzisha wao wenyewe EWURA wa bulk supplies.....................sasa tuwaache wavune walichopanda wao wenyewe kwa kiu yao ya kuyatumikia matumbo yao...........................ambayo kamwe hayajui kushiba au kutosheka...........................
 
Hivi jamani watanzania tuwe na akili wakati mwingine, hivi wewe umenue bidhaa kwa shs 100, faida yako ni shs10, pamoja na vat utauza kwa shs 128, sasa unapotanzzaza akupunguza bei hata shs 5, yuo mfanyabiashara hasara nani atamfidia?
<br />
<br />
mbona wakati bei ikipanda wanapandisha kwa kas?
 
Hivi jamani watanzania tuwe na akili wakati mwingine, hivi wewe umenue bidhaa kwa shs 100, faida yako ni shs10, pamoja na vat utauza kwa shs 128, sasa unapotanzzaza akupunguza bei hata shs 5, yuo mfanyabiashara hasara nani atamfidia?

mkuu mbona mfano wako hauendani na habari hii bei hazipangwi kama unavyofikiri
 
Hivi jamani watanzania tuwe na akili wakati mwingine, hivi wewe umenue bidhaa kwa shs 100, faida yako ni shs10, pamoja na vat utauza kwa shs 128, sasa unapotanzzaza akupunguza bei hata shs 5, yuo mfanyabiashara hasara nani atamfidia?

Hivi mkuu unafahamu biashara ya mafuta? Usiwatetee tu hawa jamaa bila kujua upande wa pili! Jiulize kwa nini wakati ule serikali imetangaza bungeni kupandisha kodi ya mafuta ya taa na kuondoa baadhi ya kodi kwenye petroli jamaa walipandisha bei ya mafuta ya taa bila kushusha jamii ya petroli?
Hawa wanapata faida sana na watanzania tunamuia sana, sema tumeshazoea kupigwa kama wanawake wa kikurya, tukitetewa twalalamika.
 
Hivi jamani watanzania tuwe na akili wakati mwingine, hivi wewe umenue bidhaa kwa shs 100, faida yako ni shs10, pamoja na vat utauza kwa shs 128, sasa unapotanzzaza akupunguza bei hata shs 5, yuo mfanyabiashara hasara nani atamfidia?
<br />
<br />
I// Kama wikimbili zilizopita Eura walipandisha bei nawalisha nunua mafuta hiyofaida ilienda wapi?
 
Back
Top Bottom