Waunguja wawabagua Wapemba

Waunguja wawabagua Wapemba

Nyerere alisema jeuri ya wazanzibar kujiita wazanzibari, inatokana na muungano. Pasipo muungano hakutakuwa na Zanzibar, badala yake kutakuwa na Unguja na Pemba. Hizi ni dalili tosha kwamba baada ya muungano kuvunjika, watabaguana tena. Kama nia yao ni kuikataa bara, kwanini wasiungane pamoja bila kujali uunguja na upemba kuikabili Tanganyika?

Mkiambia mzee ani nabii tunabisha, yanatokea sasa
 
Huu ni upuuzi tu ! Hawa wehu hatuwataki tena waende tuwe majirani tu. Hao waunguja na wapemba watajuana wao hukohuko baharini.
 
(4) Rais wa Jamuhuri awe anapotikana kwa Zamu, kipindi kimoja upande

mmoja wa muungano na kipindi chingine upande mwengine wa muungano.

Hichi ndicho kitanzi cha muungano. Wakati wa Nyerere aliweza kulazimisha hili likatokea. Sasa watu wa Tanzania bara hawalitaki hili na ndicho kinachowauma watu wa Zanzibar. Halitaweza kuingizwa kwenye katiba mpya na bila hivyo sioni Zanzibar ikiikubali hiyo katiba mpya.

Hamna cha Upemba wala Uunguja. Ni longolongo tu. The buck stops here.
hilo la rais wa zamu zamu walisahau tu ..imekula kwao...kuwabeba beab kumeshaisha...
 
heri mie sijasema jamani shule shida
 
baba unguja+mama pemba=mimi mzanzibar

hao wapuuzi waliaza UAMSHO wanavunja katiba wamefeli, kwa kuchoma makanisa ili wabadilishe mada wamefeli ,vitisho wamefeli,sasa wamekuja na vipeperushi wamefeli,tunasubiri jengine KWELI kifo cha nyani miti yote huteleza......................hahahahahahahahahaha apo apo apoo sasa, mwendo mdundo mpaka kieleweke izo chokochoko zao zimepitwa na wakati SILAHA YETU UMOJA WETU' NA HOJA YETU NI ZANZIBAR YETU jengo hili limejengwa kwa misingi madhubuti ya uelewa wetu mkubwa dhidi ya adui yetu watawala mafisadi walopania kuiteketeza zanzibar hihi ndio
ZANZIBAR POPULAR UPRISING U
''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA''

muungano hatuutaki
kura ya maoni haki yetu tupewe
katiba mpya mwisho msasani
mwimbi la sunami halizuiliki
maji ukiyazibia njia huja mitaani yakaleta mafuriko
akipiga bomu muungano byebyebye
wakimkamata shehe wetu panachimbika
hatutulii mpaka nchi tuikomboee
 
Wakimaliza kuchoma makanisa watachomana wenyewe...ndio laana ya kuua watu na kuwaletea mateso
 
kuitafuta haki kuna gharama zake ndugu zangu, yatasemwa mengi sana ya uzushi ili kudhoofisha nguvu. waswahili husema ''UKITAKA KUONEKANA MBAYA DAI CHAKO''

Inategemea mazingira na busara, kwamba hicho unachofikiri ni chako unakidai vipi!
Huu ubaguzi tunaouona leo Zenji utaendelea. Wakishamalianza kujitenga na bara wataanza wao kwa wao. Kwa sasa, common enemy ni bara, lakini wakishamaliza na common enemy wataanza ubaguzi kati ya Pemba na Unguja.
 
UVUMILIVU UNA KIWANGO .
UKIZIDI NI HATARI
Kutokana na hali mbaya ya Wapemba kuendesha .siasa chafu ndani ya "UWAMSHO" na kudai muungano hawautaki na kutaka Wabara warudi kwao bara na ilhali wao Wapemba wako wengi mno huko bara.
Na bila ya aibu wanatamka wabara warudi kwao.
Na sisi watu wa "UNGUJA" tunaiambia serikali ya maapinduzi ya Zanzibar kuwa
. .
tumechoka na hili na tunatamka "RASIMIN" Kuwa Wapemba hatuwataki tena
hatuwataki "KHASA" na warudi kwao Pemba, wakaunde serikali yao wanayoitaka na sisi tutabakia na serikali yetu ya Unguja ambayo tunahitaji kuwa
na muungano wa kweli na ndugu zetuwa Tanzania bara.
. . .
Tunasema tena sisi watu wa Unguja tunataka "Muungano" na hoja kubwa ya
watuwa Unguja:'- .
(1) Muungano waserikali mbili ya Unguja na Tanganyika na bila ya kuwemo
na Pemba.
(2) Kuwepo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar isiyo ya umoja wakitaifa.
. .
. . .
(3) Rais wa Zanzibar awe ndio makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
, (4) Rais wa Jamuhuri awe anapotikana kwa Zamu, kipindi kimoja upande
. , . . .
mmoja wa muungano na kipindi chingine upande mwengine wa muungano.
(5) Waziri mkuu atatoka Tanzania bara kwa vile ni mtendaji .
(6) Baadhi ya Rasilimali za ndani kila nchi iwe na zake kama vile madini na mafuta.
(7) Ulinzi wa nchi uwe wa pamoja
(8) Mabalozi wa Tanzania nchi zanje tuwe na magawano sawa.
(9) Mgawano Wa misaada na mambo ya maendeleo kutaka nje kuwe na uwiyano unaotambulika na kuona Zanzibar inafaidika ipasavyo.
Hivyo kwa manti ya kipeperushi hichi watu wa Unguja tunarejea kusema tena
tumechoka na Wapemba hapa Unguja na muhame mwende kwenu Pemba mkajipange kukataa muungano
Ukweli usiofichika tumeshachoka kuwa nyinyi hapa Unguja rudini kwenu Pemba. Mtuache sisi wa Unguja tukae na wenzetu wa bara wanaoishi hapa Zanzibar. Hakuna historia inayoonyesha muunganowa Unguja na Pemba bali kuna historia inayoonyesha muungano wa Unguja ha Tanganyika mwaka 1964.
Nendeni kwenu mkaunde jamhuri yenu mpya ya watu wa Pemba.
Kila sikumnajenga Unguja kwenu hapa Unguja bila ya ridhaa yetu nani mtu wa Unguja aliyejengaPemba ?
Mnajenga mpaka ndani ya viuzio vya maji.
Tunasema tokeni na hameni maramoja;
"MASSAGE SENT”
Tafadhali toa copy umpe mwenzio asome bila ya kuogopa kama vile .
"MUAMSHO~ wanavyofanya mikutano bila ya kuogopa Serikali na kutishia amani. .
ya nchi na Serikali inaona. HAKIKISHAVIMESAMBAA ZANZIBAR YOTE
 
Mukituchafua Watanganyika mutahama na Makanisa yenu Zanzibar, kama njia yakuishi Zanzibar munaona nikupandikiza chuki zidi ya Wananchi wa Zanzibar basi mutahama kwa mikwaju na Makanisa yenu Machogo.

Ikiwa W-Pemba Warudi kwao jee Shein na Aboud na Salim Salim jee mutamuingiza katika katiba yenu mpya?.
 
Nyerere alisema jeuri ya wazanzibar kujiita wazanzibari, inatokana na muungano. Pasipo muungano hakutakuwa na Zanzibar, badala yake kutakuwa na Unguja na Pemba. Hizi ni dalili tosha kwamba baada ya muungano kuvunjika, watabaguana tena. Kama nia yao ni kuikataa bara, kwanini wasiungane pamoja bila kujali uunguja na upemba kuikabili Tanganyika?

good point..wakishakua na nchi bado wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe...unguja na pemba zitaanza kupigana..na hivi walivyo hawana kazi nyingine ya kufanya...kutakua na civil war ya nguvu
 
WALIOANDIKA SIO WAZANZIBAR, naona Wameanza Siasa chafu kama walivyozusha mambo ya UDINI wakati wa Uchaguzi wa 2010
 
Haya wale wanajiita uamsho sera yao ya wazi ni kupinga muungano, na sera yao ya nyuma ya pazia ni kupambana na makanisa, baa na kufukuza wabara waishio Zanzibar.

Sasa hawa walioandika huu waraka wenye sera za kupinga wapemba kuwepo unguja ni akina nani? Kwanini na wao wasijitokeze hadharani ili kwa uchache tujue hata jina wanalotumia? Halafu mbona madai yao kuhusu aina ya muungano wanaoutaka ni yaleyale ambayo yataendeleza kero za muungano?

Mfano:-

(1) Muungano wa serikali mbili ya Unguja na Tanganyika na bila ya kuwemo
na Pemba. Muungano sahihi ni wa serikali tatu siyo huu wa mbili ambao ni kero kwa watanganyika.

(2) Kuwepo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar isiyo ya umoja wakitaifa. Haya ni mambo ya Zanzibar ambayo hayawahusu watanganyika. Huku Tanganyika tunahitaji serikali ya kizalendo (bila kujali ni ya umoja wa kitaifa au ya chama kimoja) itakayo simamia raslimali za watanganyika kwa manufaa ya watanganyika.

(3) Rais wa Zanzibar awe ndio makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapana kila nchi yaani Tanganyika na Zanzibar itakuwa na rais wake na atakuwepo rais wa muungano ambaye atasimamia wizara za mambo yanayohusu muungano pekee.

(4) Rais wa Jamuhuri awe anapotikana kwa Zamu, kipindi kimoja upande mmoja wa muungano na kipindi chingine upande mwengine wa muungano. Huu utaratibu utaihusu serikali ya Muungano pekee na huyu rais atahusika na mambo ya muungano tu. Watanganyika tutakuwa na rais wetu atakayesimamia mambo ya Tanganyika bila kuingiliwa na huyu wa muungano kwa jinsi iwayo yote.

(5) Waziri mkuu atatoka Tanzania bara kwa vile ni mtendaji. Hapana tutakuwa na rais mtendaji wa jamhuri ya watu wa Tanganyika ambaye atasimamia maslahi ya watanganyika. Muundo wa serikali ya Tanganyika utaamuliwa na watanganyika wenyewe. Hatutaki waziri mkuu kibogoyo ambaye kazi yake ni kulialia tu bila kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yoyote ya maana.

(6) Baadhi ya Rasilimali za ndani kila nchi iwe na zake kama vile madini na mafuta. Naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. Raslimali zilizo Tanganyika ni mali ya watanganyika na zilizopo Zanzibar ni mali ya wazanzibari. Hii inahusisha ajira kwenye serikali hizi mbili na haki ya kumiliki ardhi na biashara ndani ya Tanganyika na Zanzibar. Yaani mtanganyika asiruhusiwe kuajiriwa na taasisi za kizanzibari na wala asiruhusiwe kuishi, kumiliki ardhi wala biashara ndani ya Zanzibar isipokuwa kwa kibali maalumu. Vivyo hivyo mzanzibari asiruhusiwe kuajiriwa na taasisi ya kitanganyika na asiruhusiwe kumiliki ardhi wala makazi, wala biashara Tanganyika bali kwa kibali maalumu.

(7) Ulinzi wa nchi uwe wa pamoja. Ulinzi wa mipaka kwa maana ya JWTZ. Kila nchi ijitegemee kwa jeshi lake la polisi na magereza.

(8) Mabalozi wa Tanzania nchi zanje tuwe na magawano sawa. Sawa ila gharama za kuendesha hizo balozi nazo zigawanywe kwa uwiano ulio sawa. Yaani zile zinazoongozwa na wazanzibari ziligharamiwe za serikali ya Zanzibar na hali kadhalika zile zinazoongozwa na watanganyika zigharimiwe na Tanganyika.

(9) Mgawano Wa misaada na mambo ya maendeleo kutaka nje kuwe na uwiyano unaotambulika na kuona Zanzibar inafaidika ipasavyo. Naunga mkono ila mgawanyo huu utahusu ile misaada inayotolewa kwa serikali ya muungano peke yake ambapo tutagawa misaada hiyo kwenye mafungu matatu. Yaani moja la Muungano jingine la Zanzibar na jingine la Tanganyika. Kila nchi itabaki na haki na uhuru wa kukopa kivyake na kuingia makubaliano ya moja kwa moja na nchi wahisani.

Message sent and delivered.
 
Nawashangaa hao wapemba wamejazana kwenye nchi za watu shukrani hawana kama vipi wachape lapa. Nijuavyo mimi watu waunguja ni watu waastaarabu sana ndiyo maana mzee Karume hakuona shida kuungana na watanganyika sass kama vipi jamani sio lazimaa yani nyie taratibu pandeni boti kaanzisheni maduka jengeni maghorofa pemba mtakuwa mnafanya la maana. mnaleta chokochoko wakati mali zenu zote zipo Bara na Unguja mbona hamjitambui nyieee? Mtu upo bondeni unamrushia jiwe aliye mlimani?
 
Huu waraka kwa asilimia 100 haujaandikwa na UAMSHO bali umeandikwa na serikali ikishirikiana na ccm ili kuwagawa wanachi wa zanzibar katika jitihada zao za kuupinga muungano. Mimi niko Unguja na hakuna hata mkazi hata mmoja wa unguja anayeupenda muungano wao huu wa kinyonyaji.
Chunga kauli za ajabuajabu, una uhakika na hili unaloliandika? hasa hapo nilipoweka red. Usiusemee moyo wa mwenzako. Ufinyu wa kufikiri husababisha kutupa lawama kuwa shida ulizonazo zimesababishwa na mtu mwingine. Ulizaliwa tu na huna muda mrefu hapa duniani utakufa na utawaacha watu na maisha yao, usione vyaelea, vimeundwa kaka!!!!! watu walijitengenezea utaratibu wa maisha wakiumiza bongo zao, wakafanya mapinduzi na wakaunda muungano. Anyway, una fursa ya kutumia ubongo na sio maandamano ya kuvunja makanisa na kreti za bia eti umeukataa muungano, hii akili au matope, umekataa muungano na bia? jipangeni la sivyo mtaishia kupigwa virungu na kutoa machozi baada ya mabomu.
Ah,
 
dah ccm kweli mahodari kwa propaganda. jana niliziona zile karatasi zinagaiwa pale kisonge(maskani ya ccm) hao viongozi wa uamsho hakuna hata mmoja mpemba, sheikh mselem ni mdonge(unguja) juma musa aliekamatwa juzi akasababisha fujo mdonge(unguja) azzan mfenesini unguja, faridi mama yake pemba baba yake unguja. sasa sijui muamsho gani wanaosema wao! wanataka wawagawa wazenji ili wawastopishe na harakati za kudai zenji yao.

....wacha danganya watu na kuufanya ukweli kuwa urongo weye! seikh mselemu & company ni mapemba wote!
 
Hatimae baada ya kuibuka vuguvugu la kuupinga muungano visiwani zanzibar na kupelekea hali ya vurugu, wakazi wenye asili ya unguja wamepitisha vikaratasi kwenye makazi ya raia wenye asili ya pemba waliwataka waondoke mara moja maana hawana shukrani.

My take:
je maneno ya mwalimu yanatimia?

SOURCE: WAPO RADIO FM- KIPINDI YALIYOTOKEA SAA MOJA JIONI.
:violin::ranger:
 
Back
Top Bottom