Watz tuimarishe uzalendo tuepuke udini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watz tuimarishe uzalendo tuepuke udini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by goodluck tesha, Apr 11, 2012.

 1. g

  goodluck tesha Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwasisi wa taifa letu mwl julius k.nyerere alisaidia sana ktk kukuza umoja wetu hivyo taifa lilijengwa vema na uzalendo ulipatikana.mwl alijitahidi kupambana na ukabila,udini,matabaka,uonevu,ukanda na ubaguzi.leo tunajionea wenyewe jinsi viongozi wetu hasa wa chama tawala mnavyomomonyoa nguzo muhimu za nchi yetu.badala ya kuhubiri mshikamano tunahubiri mfarakano tutegemee nini kama kwa sasa tunastawisha udini tunagawa watz ktk misingi ya dini.

  Rejea uchaguzi mkuu 2010,uchaguzi mdogo ubunge igunga .ninaumizwa na hii hali na ninachokiona siku za usoni si chema naamini tz haitakaa ifikwe na machafuko ya kikabila lakini machafuko ya kidini yatajatuathiri tusipochukua hatua sasa.nimefikiri sana hata kufikia hatua ya kusema laiti tusingekuwa na hizi dini za ukristo na uislamu tungeweza kuepuka mzozano wa kidini.

  Tujiulize wtz na waafrika wenzangu ukristo na uislamu si utamaduni wetu sisi tumeacha tamaduni{dini} zetu tunakimbizana na tamaduni za wazungu na waarabu.je tukianza kukwaruzana sisi kwa sisi itakuw faida ya nani?ili kuepusha hilo viongozi na serikali hakikisheni mnaepuka kutumia kwa vyovyote maneno yenye kuchochea ubaguzi.

  Dini hizi za wageni zisitugombanishe tuimarishe taifa letu tuwe wazalendo kweli.anayetugombanisha kwa msingi wa dini awe ni adui yetu sote wtz.mungu ibariki tz mungu wabariki wtz. Nawasilisha
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Nyerere alifuta mahakama za kadhi kwa kujua ni chimbuko la mifarakano ya kidini lakini JK kwa vile ni muislamu kaunda tume yenye asilimia 75 waislamu ili azirudishe na kuleta mifarakano.................na ni JK ambaye kila siku ngonjera yake ni kupiga vita udini ambao mwasisi wake ni yeye mwenyewe. Hii inanikumbusha mwizi ambaye baada ya kuiba anakuwa wa kwanza kuupiga uyowe ili kupoteza malengo...................sungura mjanja
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona unaleta mjadala mmpya!
  Kwa kukumbusha tu aliyeweka mahakama ya kashi kwenye ilani ya CCM ni mkapa sio JK
   
 4. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu,ccm bila udini kwa mgongo wa nyuma haiendi. Mi nadhani kama tunataka kuendelea na tanzania yetu yenye mshikamano tuwapuuze maaskofu, mashehe, na hata wachungaji wanaotaka kuligawa taifa letu kwa misingi ya dini zetu. Tuwaogope kama ukoma!
   
 5. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Itawagharimu sana CCM hii, na tunakoelekea wajanja wengi wameshaligundua hili ila wajinga wanahangaika nalo
   
 6. d

  dundula JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 541
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndugu mbona ukuhoji Warioba na Augustino R ila umeona la waislam kuwa wengi? ulitaka wakina nani wawe wengi? mm naona wewe ndo una udini na ubinafsi
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kwa hatua tuliyofikia mijadala ya udini haikwepeki! Haiwezekani nyie miaka yote mnakaa kimya wenzenu wanaufanya wazi wazi tena kwenye mambo yenye maslahi ya wengi. Wanafanya udini kwenye ofisi za umma. Lazima wote tuseme sasa. Nahisi wachache wakifa kwa sababu ya chokochoko hizi tutawekana kwenye mstari. Haiwezekani na haingii akilini we uwajaze watu wa aina moja kwenye kitu kinachohusisha na wapagani!
   
 8. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi sina tatizo na watu wa upande mmoja kuwa wengi! Cha msingi waepuke kuingiza maslahi ya imani zao kwenye jambo hilo, ambalo linahusu hata wasio na dini! Maana lengo la tume sio kutafuta sheikh au mchungaji. Wakiweka maslahi ya dini zao mbele walaaniwe! Tuwapuuze mashehe,maaskofu na wachungaji wanaotaka kutugawa kwa udini.
   
Loading...