Waturuki wai 'HACK' website ya microsoft | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waturuki wai 'HACK' website ya microsoft

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 24, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Kakwola Rajabu

  Kundi hilo linalojulikana kama “Terrorist crew” liliiteka kwa masaa kadhaa website ya Microsoft maalumu kwa nchi ya Ireland na kuwaachia wadau wa website hiyo salamu za idi Mubarak.

  Mwaka 2006 kundi jingine la waturuki liliiteka website ya Microsoft ya Ufaransa na kuwaachia wadau wa Microsoft ujumbe huu:

  "Hi Master :) Your System 0wned By Turkish Hackers! redLine ownz y0u! Special Thanx And Gretz RudeBoy |SacRedSeer| The_Bekir And All Turkish HacKers next target: microsoft.com date: 18/06/2006 @ 19:06 WE WERE HERE...."

  Kundi la vijana wa kituruki limekuwa likishindana na kundi la vijana wengine wa Urusi katika kuziteka tovuti mbali mbali duniani.

  Mwaka 2005 kundi hilo lilifanikiwa kuziteka computer za vyombo vikubwa vya habari vya marekani kama vile CNN, New York Times, ABD News na vinginevyo na kufanikiwa kutuma virusi kibao ambavyo vilivuruga mitambo yao.

  Mojawapo ya tovuti zilizowahi kutekwa na kundi la waturuki ni tovuti ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uraisi wa Marekani kupitia chama cha Republican Duncan Hunter,tovuti ya chama cha soka cha Denmark ,tovuti ya NGO moja ya kupambana na ukimwi nchini Ufaransa ya Solydays.

  Katika tukio la jana vijana hao waliwashangaza wadau wa Microsoft waliotembelea tovuti hiyo jumanne asubuhi kwa kukuta meseji ya EID MUBARAK na meseji yao ya kujipongeza kwa kuiteka website hiyo.

  Hata hivyo wataalamu wa microsoft walifanikiwa kurekebisha tatizo hilo ingawa liliwachukua masaa kadhaa.

  Msemaji wa Microsoft Ireland alisema "Hakukuwa na ubadhirifu wowote uliofanyika kutokana na tukio hilo".

  "Kulikuwa na mapungufu katika ulinzi wa tovuti yatu ,Wataalamu wetu wanashughulikia tatizo hili ili lisitokee tena " aliongeza msemaji huyo.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hongera sana
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Eeeh huo ndio mpango mzima!!!
   
 4. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Aminia mwana hiyo kazi naipenda saana

  Pia kuna kingine kilete Web ya FA kinaitwa KKP kama sikosei wakaweka piacha ya maradona kavaa jez ya brazil
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  zat iz f*kin siriaz jobu. nafurahia sana mtu anapoumiza misuli ya ubongo na kujipima kwa mastaa! ila ukitoka madokyument na mafweza ya watu sooo!
  kip it up bwayz!! hiyo ni kuwaalat tu kuwa ze maximam sekyuadi iz noti sekyua, the teh!
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  Hili bandiko limeandikwa bila kuelezea chanzo cha habari. Limeandikwa kana kwamba tukio limetokea jana au siku chache zilizopita kuendana na sikukuu ya Eid. Jambo ambalo linaonekana si kweli. Nimeangalia matukio mengi kuhusiana na hacking ya hivi karibuni kwa MS Ireland, yote hayaoneshi tukio hili kwa mwaka 2009. Tukio linaloelezeka hapa as if limetokea hivi majuzi nadhani ni lile lililotokea mwaka jana, December 2008.

  Kama habari hii imeandikwa kwa makusudi ili kutoonyesha vyanzo vya habari na tarehe ya tukio, basi kiujumla habari itakuwa na dhamira ya upotoshaji.

  Kama unapata muda, angalia link zifuatazo: http://www.theregister.co.uk/2008/12/09/ms_ireland_redirection_defacement/
  na hii: http://www.neowin.net/news/main/08/12/09/microsoft-ireland-website-defaced

  SteveD.
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Juzi tu walihack website ya KIATO
   
Loading...