Mama Naa
JF-Expert Member
- Aug 31, 2020
- 385
- 950
Habari wana jamvi,
Hazina mna utaratibu wenu wa kutoa mikopo kwa Watumishi wa halmashauri zilizopo pembezoni kitu ambacho ni kizuri.
Utaratibu wa kuomba mwanzoni ulikuwa ni kupitia halmashauri lakini mwaka huu mmekuja na mifumo. Watumishi wengi waliomba mikopo kupitia mfumo kumbe bado haitoshi ni lazima tena uombe kupitia makaratasi huko halmashauri.
Sasa kwa nini mmekuja na mfumo ambao hamuuamini mpaka mnarudi tena kuomba kupitia barua na viambata vingine?
Watumishi wengi wamekosa hiyo mikopo yenu kwa sababu baadhi ya halmashauri kama Maswa hawakutoa taarifa kwa Watumishi kuhusu kuomba kupitia barua na viambata vingine hivyo kuwakosesha kwa makusudi mikopo.
Hazina na serikali kwa ujumla, halmashauri nyingi zimeoza kiutendaji hivyo linapokuja suala la mifumo ni bora iwe inajitosheleza, sio mara mifumo mara makaratasi halafu hamtoi taarifa.
Ahsante.
Halmashauri ya Maswa Simiyu.