mij
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 1,993
- 2,128
Hivi leseni ya ualimu maana yake huwa ni nini?
Hii ni leseni/ruhusa ambayo mtu asiye na taluma ya ualimu anapewa afundishe ila kwa muda maalum then baadae anapaswa akasomee ualimu. Hivyo:
1. Kuna wale waliomaliza kidato cha 6 then walienda kozi fupi baadae wakapelekwa kwenye shule wakafundishe. Hata hivyo wakapaswa baadae waende kusomea ualimu ili wawe na sifa hiyo.
2. Pia wapo wenye shahada ambazo si za ualimu nao pia hupewa leseni ya kufundisha. Baada ya hapo lazima wakasome PGDE ili wawe waalimu.
Hivyo kama hao namba 1 na 2 walienda kusoma vyuoni lakini wakakiuka masharti yaweza kuwakuta matatizo na wapo wengi sana. Kuhusu huo waraka sina uhakika kama upo au hapana.